Wizara ya Ardhi haitaki kuwalipa wataalamu wake?

Jambo Kubwa

Senior Member
Jan 21, 2017
149
204
Habarini ndugu jamaa na marafiki..
Poleni na hongereni na kazi na majukumu ya kila siku.

Nisiwachoshe sana na salaam naomba niende kwenye mada husika.

Mnamo tarehe 26/03/2022 Wizara ya ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi, ilitangaza nafasi 1448 za ajira ya muda wa miezi 3 (siku 90) (tangazo kumbu. Na JA.9/259/01/A/61) kwa kada tofauti kama vile mipango miji, wapima ardhi, wasanifu ramani, maafisa ardhi n.k kwa ajili ya kufanya na kufanikisha zoezi la data conversion yaani kubadili taarifa za ardhi kutoka analojia kwenda dijitali ili kuendana na mifumo ya sasa ya TEHAMA.

Kazi hii ilianza mnamo tarehe 09/05/2022, kwa wataalamu waliopata nafasi hizo kupangiwa mikoa tofauti ili kuanza na kumaliza kazi kwa haraka kuendana na muda uliopangwa.

Katika kuanza kazi hii, wataalamu hawa walipewa mikataba inayoelezea mchanganuo wa kazi watayofanya na malipo yake, ambapo malipo yalikua ni kiasi cha shilingi 60,000/= kwa siku na yatalipwa kwa kila baada ya siku 7 (yaani kama kazi imeanza siku ya jumatatu basi siku ya jumapili malipo inabidi yafanyike).

Pia waliapishwa kiapo cha utii na cha kutunza SIRI. (Naomba nisiende sana uko) Kazi ilianza kwa hari, nguvu na kasi ya ajabu kwa vijana hawa wazalendo kutimiza majukumu yao zaidi ya ilivyotarajiwa.

Changamoto ilianza kujitokeza kwenye masuala ya malipo wiki mbili tu baada ya kazi kuanza, ila maelezo yalitolewa changamoto hizo ni kutokana na mfumo wa fedha kwa kuwa mwaka wa fedha unaelekea mwisho na kuanza mwaka mwingine, hivo changamoto za malipo haziepukiki tunaomba uvumilivu.

Wataalamu wakavumilia na baada ya muda malipo yalitoka kidogo kidogo na kuwapa nguvu wataalamu kuendelea na kazi hadi muda wa kazi kulingana na mkataba ulipomalizika mnamo tarehe 06/08/2022.

Hadi kufikia tarehe ya mwisho wa kazi, tarehe 06/08/2022 wataalam walikua wameshalipwa siku 70, kati ya siku 90 za mkataba hivyo bado wanadai siku 20. (Ijapokua wapo wanaodai zaidi ya siku tajwa, 20)

Uvumilivu wa wataalam haukuishia tu wakati wa kazi la hasha, hata baada ya kazi kukamilika maana walivumilia kumaliza kazi kwa uweledi na uzalendo ilihali bado wanadai siku 20 na zaidi.
Hivi sasa ni zaidi ya mwezi mmoja, tangu mkataba wa kazi ukamilike, lakini malipo ya wataalamu kwa siku zilizobaki bado hayajafanyika, hata kama ni uvumilivu uo ni uvumilivu wa aina gani..?

Hata kama ni uzalendo huo ni uzalendo wa aina gani..?
Tukumbuke;
1. Vijana hawa wamefanya kazi katika mazingira ya ugenini na magumu, hivo kuishi kwao kulitegemea pesa aliyokuwanayo mfukoni hivo wengi wakaingia mikopo kwa ndugu jamaa na marafiki ili waweze kukamilisha kazi wakiamini watalipwa kwa wakati na kurejesha mikopo io, lakini mambo yamekuwa tofauti.

2. Vijana hawa hawajamaliza vyuo mwaka 1 au 2 iliopita kama inavyodhaniwa na viongozi wa wizara, wapo waliomaliza zaidi ya miaka 7 iliopita kiasi kwamba kama wangepata ajira kwa wakati sasa hivi wangeshakua wataalam wa daraja la 1 au waandamizi (seniors) kabisa, ila kutokana na changamoto za ajira katika nchi yetu hasa kusahaulika kwa kada za ardhi inapelekea kuwepo kwa watu hawa mtaani na kuendesha maisha na familia zao kwa shughuli tofauti kabisa na walizosomea ilihali serikali ilitumia gharama kubwa kuwasomesha.

Sasa inapotokea fursa yoyote ya kuonyesha utaalam wao katika kazi hawasiti kuitumia fursa io, lakini kwa bahati mbaya kwa kazi hii ya data conversion 'fursa' imegeuka kuwa 'kucha' kwa kuwakwarua wataalam kuwatoa damu na kuwaachia maumivu makali.

3. Kwa wataalamu waliokua wanafanya kazi za utambuzi uwandani (site), walikua wanafanya kazi na wajumbe wa serikali za mitaa. Wajumbe hawa pia hawajalipwa stahiki zao hadi leo, je hii inaleta tafsiri gani kwa Serikali yao (inashangaza kwa kweli).

Mvumilivu hula mbivu, lakini uvumilivu ukizidi hata hizo mbivu utakuta zimeharibika.

Mheshimiwa Waziri, alinukuliwa katika chombo flani cha habari katika kipindi cha asubuhi, akijibu swali kuhusu malipo ya wataalamu wa muda waliofanya hii kazi, alisema "Ni ukweli kulikua na changamoto za malipo kutokana na mfumo wa malipo kusumbua pindi mwaka fedha unapokua mwishoni, lakini baada ya kukaa sawa wataalamu walilipwa"
Kauli hii ilifanya moyo uvuje damu na kujiuliza ni kwamba Waziri ameamua kutotoa taarifa sahihi, au watendaji wake wa chini wamempa taarifa ambazo sio sahihi..?

Kwa kumalizia, naomba Wizara ifanye malipo kwa wataalamu kwa siku zao zote zilizobaki, jambo hili lifanyike ili kuendelea kulinda imani waliokuwa nayo kwa Serikali yetu Tukufu na pia waweze kushiriki kwa moyo mmoja endapo itatokea Wizara kuwahitaji kwa kazi nyingine.

Wataalamu wana majukumu wana familia wanategemea kutumia fedha hizo kutimiza mahitaji mengine ya muhimu.

Wengine wanataka watumie kama mitaji wafungue biashara waweze kuendesha maisha lakini mnawakwamisha na kuikoseha serikali mapato kwani wakifungua biashara watalipa kodi.

Tunaomba msisimamishe shughuli za uzalishaji na mzunguko wa uchumi.
Tumechoka kusubiri, tunaomba tulipwe stahiki zetu.

Wako katika ujenzi wa Taifa,
TP. Raia Mtanzania
 
Umenena vema mkuu_kuna kila sababu wizara ya ardhi chini ya Serikali Tukufu ilitafakari hili na kutenda utu kwa vijana 👋
 
Shida ya serikali hasa viongozi wa wizara ya ardhi inaamini vijana hawana majukumu ndo maana wameamua kukaa na fedha zao makusudi mpaka sasa

Kwanza kazi ilifanyika katika mazingira magumu saana, ugenini, bila mapumziko kwa siku zoote 90 (kiufupi vijana walipiga kazi kama punda), kuna waliokopa wkununua vifaa vya kazi wakiamini watapata pesa walipe lakn ndo hivyo vijana wamegeuka fursa kwa wapigaji wa wizara
 
Ni huzuni inayo sikitisha sana kwa wizara yetu ya ardhi. Inapunguza imani kwa vijana ikitokea kazi tena ya mda kama hiyo.
 
TP. Raia Mtanzania na wewe ni mmojawapo wa Mlio Pigwa hapa au we ni Mwana Habari reporter Mwema?
 
Shida ya serikali hasa viongozi wa wizara ya ardhi inaamini vijana hawana majukumu ndo maana wameamua kukaa na fedha zao makusudi mpaka sasa

Kwanza kazi ilifanyika katika mazingira magumu saana, ugenini, bila mapumziko kwa siku zoote 90 (kiufupi vijana walipiga kazi kama punda), kuna waliokopa wkununua vifaa vya kazi wakiamini watapata pesa walipe lakn ndo hivyo vijana wamegeuka fursa kwa wapigaji wa wizara
Ziko bank mkuu wanasubr zimachue
 
Kiukwel wizara hapa imefanya wataaalam waone wao ni waswahili...ikumbukwe wataalam walioenda kwny huo mradi wengi wao ni kutoka familia za hali za chini na hiyo ilikuwa sehem ya kujipatia walau mitaji ila ndo imekuja kuwaangamiza zaidi ya walivokuwa mitaani
 
Wamewajibu Tena kwa Walaka ila hawataja Tarehe wamesema tu wiki ijayo Sasa sijui ndio inayo anzia Kesho au inayo anzia jtatu ijayo
IMG-20220918-WA0019.jpg
IMG-20220918-WA0019.jpg
 
Nchi ngumu sana hii, watu wanasoma kwa shida, ajira mtaani hakuna, na hata ikitokea nafasi ndogo at least ya vijana kujikwamua serikali ndio inakua kikwazo cha kwanza.
 
So Sad!! Mtukufu Rais (Nina Imani kwa Mkono wako Mrefu; haya yanakufikia) Liangalie hili kwa Jicho la Huruma,Vijana walijitoa kwa Umahiri,Uweledi na Bidii kufanya Kazi hii, lakini wanachofanyiwa si Haki kwa Kweli. Yaone Machozi yao ya Damu,Wanaelekea kukata Tamaa. WASAIDIE NA WAOKOE!!
 
HATIMAE WAMELIPA.
AHSANTE KWA WOTE WALIOSAIDIA KUPAZA SAUTI.
AHSANTE KWA SERIKALI KWA KUSIKILIZA NA KUFANYIA KAZI MALALAMIKO.
 
Back
Top Bottom