Ofisi ya Rais Utumishi imetoa vibali vya ajira zaidi ya 9000 kwa ajili ya kuajiri watumishi mbalimbali wa kada za Afya nchi nzima tangu mwezi Septemba 2015
Kuidhinishwa kwa vibali hivyo vya ajira inaashiria kuwa tayari Serikali imeshapitisha bajeti za mishahara za watumishi hao katika mwaka wa fedha 2015/16 ambao nao unaelekea kuisha.
Kwanini nasema Rais atumbue jipu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto ambayo ndio inajukumu la kupanga Watumishi wa kada za Afya kwa Waajiri mabalimbali kama Mikoani na kwenye Halmashauri.
1. Watendaji katika Wizara hiyo wanafanya kazi kwa mazoea na kufata mikumbo na mihemuko na kusahau wajibu wa wizara hiyo wa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.
2. Ni uzembe wa hali ya juu kwa Wizara ya Afya kukaa na vibali vya ajira toka mwezi wa tisa wakati Hospitali, vituo vya Afya na Zahanati zote nchini zinakabiliwa na upungufu wa watumishi kwa 49%
3. Ni uzembe wa hali ya juu kwa Wizara kuwaacha watalaam wa fani mbalimbali za afya kuzagaa mitaani toka Julai mwaka jana walipo hitimu na kufaulu katika taaluma wakati vibali vya kuajiri vipo na mahitaji ya watumishi hayo yapo kwani baadhi ya zahanati zetu zinaongozwa na wahudumu wa Afya.
4. Ni uzembe wa hali ya juu kwa Wizara ya Afya inayosema inatekeleza mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN) ambao moja ya maeneo ya vipaumbele katika BRN ni Human Resource for Health kushindwa kutekeleza kwa vitendo BRN kwa kuhakikisha inapanga watumishi kwa wakati kila inapopata kibali cha kuajiri toka Ofisi ya Rais Utumishi
5. Wizara ya Afya imeitia hasara serikali kwa kufanya Mabilioni ya Pesa yalitongwa kwa ajili ya kuajiri nakulipa mishahara ya watumshi wa kada za afya toka Julai 2015 kukaa Hazina bila kutumika na mwaka wa fedha unaelekea kuisha bila fedha hizo kutumika
Rais Tumbua jipu pale Wizara ya Afya na pale Ofisi ya Rais TAMISEMI (AFYA) kwani inaonekana viongozi hawatambui majukumu yao na kufanya kazi kwa vitendo. Umewavumilia kuhusu Muhimbili na kuwaelekeza jinsi ya kujiongeza na kutumia rasilimali zilizopo kwa ufanisi lakini bado hawana ubunifu na kushindwa kufanya kazi ndogo tu ya kupanga wataalam ambao wapo katika soko la ajira na vibali vya ajira vipo.
Mr Emmy- nataka kuona sekta ya Afya inabadilika kwa haraka ktk Tanzania Mpya ya Magufuli.