Wizara ya Afya: Vituo vya Afya vya private Kuna ukiritimba unaendelea

Wizara ya Afya: Vituo vya Afya vya private Kuna ukiritimba unaendelea

Mlundilwa Jr

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2019
Posts
3,465
Reaction score
5,439
Mambo zenu
Jamani Hawa wamiliki wa hizi hospital dhamira yao nini hasa au wanataka kutuua?

Kuna Mzee nilikutana naye zahanati ya serikali akidai yakwamba alienda hospitali ya private kupima maralia ila baada ya kufanyiwa vpimo akaambiwa Hana Malaria na ukicheki dalili zote za ugonjwa wa malaria alikuwa nazo

Aliamua kwenda zahanati ya government alipofanyiwa vpimo alikutwa na malaria hari iliyofanya ataharuki

Sasa hili limenikuta Mimi mwenyewe, ni baada ya kuhisi homa na kukosa hamu yakula na baridi kali, nikasema wacha niende kwenye kituo Cha private kwani niliamini naweza pata huduma fasta kuliko kwenda zahanati ya government ambako ningepanga foleni mwishowe nijifie nikiwa kwenye foleni

Nilifanyiwa vipimo then nikaambiwa subiri majibu,
Wakati huo nilikuwa nishadungwa sindano ya kutuliza homa
Majibu yanakuja naambiwa Sina malaria ila Nina UTI

Wakanipa pcm na vidonge gani sijui na wakanipa maelekezo

ila Cha kushangaza hali ilizidi kuwa mbaya hasa ilipofika usiku ndipo rafiki yangu akaniambia jaribu kutumia mualovera
Nilikunywa mualovera nikahisi nafuu

Ila naamini ilikuwa ni malaria ila wao wakaniambia Nina UTI na wakanilazimisha ninunue dawa zao ambazo sikuona msaada wowote zaidi ya kupoza makali

Wizara ya Afya fanyeni uchunguzi kuanzia kwa Hawa madaktari mpaka vfaa vyao vya kutendea kazi, naona wanacheza na rasilimali watu hawa wanataka kutuuwa au wanafikiri na sisi ni akina masumbuko Mzee wa malaria yangu huanzia tumboni.
 
.....wakanilazimisha ninunue dawa zao..... Here is where the problem is i.e. if not a wrong diagnosis/incompetence then it's all about diagnozing and prescribing based on what we have in stock and not to mention polypharmacy/irrational prescribing practices solely aiming at financial gains.
 
Mbona vipimo vya malaria siku hizi ni rapid ambacho hakihitaji utaalamu sana MRDt hata wewe mwenyewe unaweza kujipima ingekua Bs sawa tutambue kuna Diagnosis na Differential DX UTi Kali ina homa na dalili zote za malaria esp Pyelonephritis,Pneumonia,Typhoid,Brucellosis,Mafua makali,Tonsillitis etc.
 
Ungetumia Lugha ya Nyerere ingekuwa poa sana mkuu anyway kitu ambacho hukijui nikwamba hizi hospitli za watu binafsi wanaangalia pesa kuliko ugonjwa ulio nao.

Hajali unaumwa vipi ila wapo radhi wakulimbikize magonjwa ili wakupige vzri
 
Mbona vipimo vya malaria siku hizi ni rapid ambacho hakihitaji utaalamu sana MRDt hata wewe mwenyewe unaweza kujipima ingekua Bs sawa tutambue kuna Diagnosis na Differential DX UTi Kali ina homa na dalili zote za malaria esp Pyelonephritis,Pneumonia,Typhoid,Brucellosis,Mafua makali,Tonsillitis etc.
Mimi malaria yangu huanzia tumboni[emoji16][emoji16] anyway nipe Darasa mkuu nawezaje
 
Pole, ni afadhali kwenda hospital zenye vifaa vya kutosha pamoja na wahudumu wenye taaluma yakutosha
Kabisa mkuu
Manaake wengine ukute alipata D ya bios ila kwakua mjomba ana dispensary anaamua kumuweka kitengo Cha Laboratory

Wenyewe wanasema utajifunzia hukohuko kazini, na chaajabu hizo nafasi wamewaweka Mabinti na si men
Kuna walakini
 
Wagonjwa wengi mnalazisha muambiwe mnaumwa ugonjwa mliokuja mkifikiria kichwani. Sasa wewe unajua kuliko kipimo? Magonjwa mengi dalili zinafanana. UTI Ina symptoms just like Malaria or typhoid. So unapopima na kuambiwa una ugonjwa fulani waamini wahudumu wa afya.

Halafu dawa sio unatumia siku 1 then unataka upone same day, No! Hiyo sio pain killer, vimelea huuwawa stagewise plus proper concentration of drug used per time.

Yes, Kuna wanaozingua but mainly wazinguaji zaidi ni wagonjwa wanaojifanya wajuaji zaidi.

Anyway, pole ndugu, recover soon!
 
Ungetumia Lugha ya Nyerere ingekuwa poa sana mkuu anyway kitu ambacho hukijui nikwamba hizi hospitli za watu binafsi wanaangalia pesa kuliko ugonjwa ulio nao
Hajali unaumwa vipi ila wapo radhi wakulimbikize magonjwa ili wakupige vzri
Mkuu siyo za binafsi tuu hata baadhi ya Hospital za serikali. Mfano Hospital ya BOMBO huko Tanga yaani huduma mbovu sana, nilipeleka mgonjwa akakaa wiki nzima hakuna huduma, wakataka laki mbili ili apate eti huduma ya fast track, tukawapa (no receipt given hapo) but hakuna kilichoendelea mpaka ikabidi tulazimishe waandike rufaa.
 
Pole Sana mkuu
Tatizo nini?
Mishara midogo ama wanafanya kwakulazimishwa
 
Mambo zenu
Jamani Hawa wamiliki wa hizi hospital dhamira yao nini hasa au wanataka kutuua?...
Mbona kama maelezo ni vice versa?

Sie tukienda vituo vya afya Mwananyamala,sinza,Tandale au Magomeni vipimo vinasema huna maralia ila mkojo mchafu na ukiandikiwa dose hupati nafuu.

Ukitoka huko na kwenda private unaambiwa una maralia 2..... nadhani hizi rapid test kit hazipo vizuri ukilinganisha na microscope
 
Ninachojua Mimi zahanati za Serikali watu watu wanakwepa foleni ila kuhusu vipimo wapo vizuri
 
Jambo ambalo watu wanatakiwa kujua ni kwamba huduma zetu za kiafya zina presha kubwa sana kutokana na kuongezeka kwa wagonjwa, pia kutokana na kuanzishwa kwa utitiri wa vyuo ambavyo havijari ubora wa taaluma, wahitimu wengi sana hawako competent kuweza kufanya maamuzi sahihi kulingana na dalili ambazo anaonyesha mgonjwa zaidi ya kutegemea majibu ya maabara na pia kutotoa matibabu sahihi kulingana na dalili na hali au hatua za ugonjwa wenyewe. Ndo maana kwa sasa msisitizo unatakiwa uwe kwenye kuthibiti magonjwa badala ya kutibu.​
 
Back
Top Bottom