Wizara ya Afya: Taarifa kwa umma kuhusu ugonjwa wa homa ya Dengue

Joyce%20Msumba-May20-2014.jpg

Afisa uhusiano wa Manispaa ya Temeke,Joyce Msumba

Zaidi ya wagonjwa 60 kutoka wilaya za mkoa wa Lindi wanahofiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa dengue.

Kutokana na hali hiyo, wanatarajiwa kuchuliwa vipimo na kufanyiwa uchunguzi kwenye maabara ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kutokana na hospitali ya mkoa huo kukosa vifaa vya kutambua ugonjwa huo.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Dk. Theophil Malibiche, alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.Dk. Malibiche watachukua wagonjwa wanaoonyesha dalili za dengue.

Alisema hadi sasa hakuna mtu aliyebainika kuwa na homa hiyo wala aliyefariki na kwamba mkoa umejipanga kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya katika wilaya zote za mkoa huo.

Aliwaomba wananchi mkoani humo kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo kwa kufanya usafi wa mazingira na kuangamiza maeneo ya mazalia ya mbu wakati utaratibu wa kupata madawa za chanjo na kinga ukisubiriwa.

Wakati huo huo, idadi ya wagonjwa waliogundulika na ugonjwa huo katika Hospitali ya Amana, jijini Dar es Salaam, sasa imefikia 79 tangu ugonjwa huo uibuke.

Akizungumza na NIPASHE, Daktari Kiongozi wa Hospitali hiyo, Andrew Method, alisema kati ya wagonjwa hao 73 waliruhusiwa na sita bado wamelazwa.

Aidha, Dk. Method alisema katika hospitali hiyo hakuna kifo kilichotokana na ugonjwa huo.

Katika Hospitali ya Temeke idadi ya wagonjwa ambao wameugua ugonjwa huo tangu kuibuka mwaka huu ni 72 na kati ya hao, 62 wameruhusiwa.

Afisa uhusiano wa Manispaa ya Temeke, Joyce Msumba, alisema wagonjwa 10 bado wamelazwa na kuwa kati ya hao, sita ni wanawake na wanne ni wanaume.

Msumba alisema pia hospitali hiyo inachukua tahadhari ya kuendelea kupuliza dawa na wagonjwa kulazwa ndani ya vyandarua kwa ajili ya kuzuia kuambukiza wengine.

Katika Hospitali ya Mwananyamala, idadi ya wagonjwa mpaka imefikia 144, wapya ni wanne na mmoja ndiye amelazwa, kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk. Faustinias Ngonyani.

Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, hadi jana hapakuwapo na mgonjwa wa dengue.

Imeandikwa na Elizabeth Zaya, Jimmy Mfuru, Hussein Ndubikile, Dar na Hamisi Abdelehemani, Lindi.

CHANZO: NIPASHE

ni upepo tu unaelekea kwisha saivi watu washapiga hela na wananchi washasahau mambo muhmu...
 
ni upepo tu unaelekea kwisha saivi watu washapiga hela na wananchi washasahau mambo muhmu...

Daaaa jamaa una akili wewe na ukichanganya na zile bilioni 200 kuna kawimbo walikianzisha juzi madini samunge yaani hii nchi kweli mazoba tupo wengi
 
Daaaa jamaa una akili wewe na ukichanganya na zile bilioni 200 kuna kawimbo walikianzisha juzi madini samunge yaani hii nchi kweli mazoba tupo wengi

wizi wa bilion 200+300 za ewura+kifo cha utata mkurugenzi ewura+serikali 2 au 3....kimyaaaaa
 
wizi wa bilion 200+300 za ewura+kifo cha utata mkurugenzi ewura+serikali 2 au 3....kimyaaaaa

Yaani ndo tunajiuliza hapa na jamaa zangu hawa mafisadi wanauchungu na nawanalinda maslahi yao kwa gharama zozote hata kutoa uhai wa mtu lakini sie maskini walalahoi tunao ibiwa hatuna habari kabisaaaaa najiliza hii ni laana tuliachiwa na babu zetu au ndio tunaangamia kwa kukosa maarifa?
 
zindiko la mwenge hilo kaka na alituzindika wa kwanza ni nyerere kwanza
MWENGE unapofunikwa usizime WANAFUNIKA VICHWA NA AKILI ZETU TUSIELEWE WANAYOTUFANYIA AU HATA TUKIELEWA TUSITE KUCHUKUA MAAMUZI......
 
Halafu nimeshitukia haya magazeti ya tanzania siku hizi yanatumika vibaya kwa maslahi ya wachache wenye kuelewa wataelewa tu unakuta kuna jambo kama wizi huu tunaofanyiwa wananchi kila uchao hawautilii mkazo kuwaelezea wananchi kinagaubaga kama wanavyoshadadia mambo mengine yaani kuzaliwa tanzania ni shida.
 
zindiko la mwenge hilo kaka na alituzindika wa kwanza ni nyerere kwanza
MWENGE unapofunikwa usizime WANAFUNIKA VICHWA NA AKILI ZETU TUSIELEWE WANAYOTUFANYIA AU HATA TUKIELEWA TUSITE KUCHUKUA MAAMUZI......

Aisee ukiniambia hiyo kitu naweza kubali mimi toka niwe na akili sijawahi kuufukuzia mwenge wala sijawahi hudhuria mkutano wowote wa ccm nawala siwezagi kutizama matukio au hotuba yeyote hakuna kitu wanaweza ongea ikaniingia akilini sijui wenzangu hotuba nilizokuwa nasikiliza ama kutizama ni za mwlm Nyerere tu basi Mungu amlaze apumzike kwa amani yule baba alikuwa na utu na alikuwa na hofu ya Mungu wapo watakaopinga kwa kusema alikuwa na mapungufu lakini binadamu hatujakamilika kwa yote ila naiona mbele freedom is coming.
 
Habari wakuu,.

Kwa taarifa zisizo rasmi ni kwamba sampuli mbili za damu katika hospitali ya KCMC zimegundulika kuwa na homa ya Dengue.

My Take: Serikali inapaswa kuchukua hatua za makusudi na za haraka ili kudhibiti ugonjwa huu hatari unaoelekea kusambaa nchi nzima sasa.

Source: Rafiki yangu anayefanya kazi maabara Hospitali ya KCMC.
 
Hakuna dengue wala ndugu yake dengue. Hizi ni mbinu tu za magamba za kutaka kuchota mabilioni ya pesa chini ya mwavuli wa dengue. Ccm kuweni na huruma na wananchi.
 
Habari wakuu,.

Kwa taarifa zisizo rasmi ni kwamba sampuli mbili za damu katika hospitali ya KCMC zimegundulika kuwa na homa ya Dengue.

My Take: Serikali inapaswa kuchukua hatua za makusudi na za haraka ili kudhibiti ugonjwa huu hatari unaoelekea kusambaa nchi nzima sasa.

Source: Rafiki yangu anayefanya kazi maabara Hospitali ya KCMC.

acha ujinga hakuna ugonjwa wa dengue
 
Back
Top Bottom