Nimepita juzi hapo Temeke Magorofani nikakuta watu wanauza matunda kilichonishtua ni mtu ameweka mananasi yaliyokatwa vipande vipande juu ya meza halafu nzi wa chooni wale nzi wakubwa wenye rangi ya gold wamejaa kwenye hayo mananasi na muuzaji hana habari.
Wizara ya Afya ichukue tahadhari mapema kwa kuwalazimisha watu Wanaouza matunda au vyakula kuwa na makabati ya vioo yasiyoweza kupitisha nzi, la sivyo kwa hali ile kipindupindu kitazuka.
kwa kweli kama hana elimu juu ya nzi vs kuhara hata iweje ni kazi bure, kuna wale wanaotumia izo kabati ( maeneo ya chipsi) na bado unakuta nzi kibao wako 'trapped' mle ndani na hajali,
Wanunuzi wa Dar huwa hawajali usafi, ukiwa unauza vipande vya matikiti maji kando ya barabara ingiza mkono ndani ya suruali yako sehemu ya zipu jikune ashua zako endelea kukata matikiti walaji hawatakuhoji wataendelea kuyala. Huyu anayehoji ya Temeke angefika Kariakoo wanaouza matunda yaliyokatwa angezimia kama si kufariki maana huko ni jalala na watu wanakula. Wiki mbili zilizopita wauzaji wa matunda yaliyokatwa Kariakoo walionywa lakini wapi mtindo ni uleule.