Habari wana MMU,
Wakuu hebu naombeni mawazo namna ya kupunguza kuwa na wivu, seriously nimechoka na nahisi hili ni tatizo kubwa si kwangu tu bali hata kwa mpenz wangu. Hajawah kuniambia moja kwa moja but I can feel it namnyima furaha sana.
Natamani ajiskie namuamini sana, tatizo linakuja kila ninapojaribu hata kumuacha tu atoke na wafanyakazi wenzake kwa jinsi nitakavyoteseka kwa hayo masaa machache anaweza kunikuta nishakufa kabisa hivyo huwa naona bora nisogee tu hilo eneo hata nimuone kwa mbali. Kuna siku nlikuwa nae kwenye gari ghafla ule wimbo wa 'Kuchapiwa ni siri ya ndani' ukapigwa redioni yani kile kitendo cha yeye kuufatiza tu ule wimbo nikajikuta nimegonga gari iliyokuwa mbele yangu kwa mshtuko.
Analijua tatizo langu na anajitahidi sana kuishi ninavyotaka na najua ananivumila sana, amepunguza sana marafiki kwa ajili yangu, hata kwenye groups hz za wasap kajitoa, fb ndio hata ile app tu kwenye sim yake haipo tena na hata akitaka kuingia anaingia kwa sim yangu.
Kilichonifanya nije kwenu ni baada jana usiku kumgombeza kwa kupigiwa simu na mwanaume akimtakia usiku mwema ilikuwa sa tatu tu usiku, hata sijui ilikuwaje lkn nikajikuta nishaanza kulalama, alisema sorry na kisha akampigia sim huyo jamaa na kumwambia asirudie tena kumpigia simu usiku.
Nimejiskia vibaya sana baada ya yeye kufanya hivyo, japokuwa bado naonyesha ukauzu bt deep inside nimenyong'onyea mbaya kabisa. Najiona mwanaume nisie na shukrani kabisa.
I really want to change nipunguze tu kidogo nibakie na kale ka wivu ka kumuonyesha najali, tatizo sijui cha kufanya pia sijui ntawezaje.
Please wana MMU nisaidien mawazo mrudishe furaha ya mrembo wa watu na amani ya moyo wangu. Nimeeleza kwa kirefu ili at least muone ukubwa wa tatizo, michango ya aina zote inakaribishwa.
[h=2]What is domestic and intimate partner violence?[/h]Domestic violence is when one person in a relationship purposely hurts another person physically or emotionally. Domestic violence is also called intimate partner violence because it often is caused by a husband, ex-husband, boyfriend, or ex-boyfriend. Women also can be abusers.
People of all races, education levels, and ages experience domestic abuse. In the United States, more than 5 million women are abused by an intimate partner each year.
Domestic violence includes:
- Physical abuse like hitting, shoving, kicking, biting, or throwing things
- Emotional abuse like yelling, controlling what you do, or threatening to cause serious problems for you
- Sexual abuse like forcing you to do something sexual you don't want to do
Emotional Abuse ndio inayowahusu zaidi na mwenzio Evelyn Salt
[h=1]Emotional abuse[/h]More information on emotional abuseYou may feel like if you're not being hurt physically, you are not being abused. But attempts to scare, isolate, or control you also are abuse. They can affect your physical and emotional well-being. And they often are a sign that physical abuse will follow.
You may be experiencing emotional abuse if someone:
- Monitors what you're doing all the time
- Unfairly accuses you of being unfaithful all the time
- Prevents or discourages you from seeing friends or family
- Tries to stop you from going to work or school
- Gets angry in a way that is frightening to you
- Controls how you spend your money
- Humiliates you in front of others
- Threatens to hurt you or people you care about
- Threatens to harm himself or herself when upset with you
- Says things like, "If I can't have you then no one can."
- Decides things for you that you should decide (like what to wear or eat)
Goodluck!
Mmmhhhh!!!
Wanaume wenye wivu ni watamu sana lol....
cc asakuta same
Kilichokufanya uni-CC ni nini wewe mwanamke?
Nimekukumbuka kaka angu sijakuona muda....
mi nahisi huyo mpenzi wako atakua na tiba halisi,mtafute sehemu tulivu mwende mkae mkumbushane good times ununue na zawad,afu mwambie hili tatizo kwa namna ulivyosema hapa !you will solve this problem together!
Aaah kuna raha bana asikuambie mtu
napendaga zaidi ile napigiwa simu "upo wapi? Rudi nyumbani upesi"
nawaacha mashost konyagi mezani huyoooo nduki nyumbani.
He he he, na mie napenda anayekaba hadi penati.
Ukimwambia unatoka roho yake juu kama Airforce 1
Ha ha ha ha uuuh mbavu zangu....
Kufatiliwa ni raha bana yani kuna raha ya ajabu hujui tu....sasa hili linakufurahishaje , badala ya kuwa kero?
Kongosho hebu nipe siri ya kupenda kufanyiwa hivyo........
Mi napenda mtu mwenye wivu....
Sijui, labda nimekulia kwenye mfumo dume kiasi kwamba umeathiri jinsi yangu ya kutizama mambo, (masculine culture).
Mwanamme mzembe mzembe na mdiplomasia sana ntamzarau. Napenda mtu analinda mipaka yake, nakasirika na kununa, ila kimapenzi zaidi.
Mkuu tatizo dogo sana hilo, hata mimi nilikuwa nalo lakini baadaye liliisha, cha msingi fanya hivi.
Kipindi akiwa anatoka na marafiki zake, paka pilipili machoni itakusaidia kutokufikiria mabaya juu yake na badala yake utakuwa busy kusikilizia utamu jichoni, maumivu yakiisha atakuwa kasharudi.
NB: Maumivu ya macho hayauwi, ila ya moyo yatakuua.
I appreciate your comment mkuu!KULA "LIKE" X90000000! What a nice advice! Tatizo siku zote linahitaji ushirikishwaji wa namna kama hii ulioeleza. I like your good strategy!congrats