Wivu unanimaliza!

Wivu unanimaliza!

Zorrander

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
438
Reaction score
233
Habari wana MMU,

Wakuu hebu naombeni mawazo namna ya kupunguza kuwa na wivu, seriously nimechoka na nahisi hili ni tatizo kubwa si kwangu tu bali hata kwa mpenz wangu. Hajawah kuniambia moja kwa moja but I can feel it namnyima furaha sana.

Natamani ajiskie namuamini sana, tatizo linakuja kila ninapojaribu hata kumuacha tu atoke na wafanyakazi wenzake kwa jinsi nitakavyoteseka kwa hayo masaa machache anaweza kunikuta nishakufa kabisa hivyo huwa naona bora nisogee tu hilo eneo hata nimuone kwa mbali. Kuna siku nlikuwa nae kwenye gari ghafla ule wimbo wa 'Kuchapiwa ni siri ya ndani' ukapigwa redioni yani kile kitendo cha yeye kuufatiza tu ule wimbo nikajikuta nimegonga gari iliyokuwa mbele yangu kwa mshtuko.

Analijua tatizo langu na anajitahidi sana kuishi ninavyotaka na najua ananivumila sana, amepunguza sana marafiki kwa ajili yangu, hata kwenye groups hz za wasap kajitoa, fb ndio hata ile app tu kwenye sim yake haipo tena na hata akitaka kuingia anaingia kwa sim yangu.

Kilichonifanya nije kwenu ni baada jana usiku kumgombeza kwa kupigiwa simu na mwanaume akimtakia usiku mwema ilikuwa sa tatu tu usiku, hata sijui ilikuwaje lkn nikajikuta nishaanza kulalama, alisema sorry na kisha akampigia sim huyo jamaa na kumwambia asirudie tena kumpigia simu usiku.

Nimejiskia vibaya sana baada ya yeye kufanya hivyo, japokuwa bado naonyesha ukauzu bt deep inside nimenyong'onyea mbaya kabisa. Najiona mwanaume nisie na shukrani kabisa.

I really want to change nipunguze tu kidogo nibakie na kale ka wivu ka kumuonyesha najali, tatizo sijui cha kufanya pia sijui ntawezaje.

Please wana MMU nisaidien mawazo mrudishe furaha ya mrembo wa watu na amani ya moyo wangu. Nimeeleza kwa kirefu ili at least muone ukubwa wa tatizo, michango ya aina zote inakaribishwa.
 
Mmmh sijui ndo wewe?? Loh! Yawezekana hivyo ndo ulivyo sidhani kama waweza change ila kwa vile umejitambua yaweza kuwa solution moja wapo cha msingi muamini kama yeye anavyokuamini wivu ukizidi sana kwa mwenzi wako ni karaha .
 
Pole sana kwa kile kinachokusumbua lakin pia nakupa hongera kwa kufahamu kosa na kugundua kuwa wewe ndio mwenye tatizo.

Nadhani ni vile unapenda mpenzi wako hata hvyo wivu ni mbaya sana tena kidonda chenye maumivu makali ktk hilo uguza kipone.

Unachotakiwa ni kupunguza wivu kwa vitu ambavyo ni vya kawaida sana. sasa hapa czijui njia zipi zitakufanya upunguze wivu kwa anayezifahamu aweze kumuelewesha kijana.

Wivu huleta hasira, chuki na kupoteza uaminifu kwa mtu. akiwa kama mpenz wako anakuwa hawi huru hata kama hafanyi kitu kibaya lakin kila atakachofanya lazima awe na woga. maana anajua wewe hautokipenda hiko kitu. angalia amepunguza marafik yote ni kwasababu yako uwe na aman na furaha lakin wivu bado haukuishi.

mmmh wivu ni kidonda ugua pole ndugu.
 
Back
Top Bottom