Wivu Umemuua!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wivu Umemuua!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kigarama, Jan 7, 2012.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Jana ilikuwa ni siku ya mwisho kwa dada yetu mpendwa kuwa naye hapa Ulimwenguni baada ya miaka zaidi ya 20 ya mateso makubwa ya kimwili na kisaikolojia.

  Miaka zaidi 20 iliyopita dada huyu alikuwa ni Bank Teller kwenye Bank ya NBC, na Mumewe alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa kwa kiwango cha wakati ule. Kwa sasa anamiliki Duka la Hardware kariakoo jijini Dar. Mumewe alikuwa anaamini yeye ni "Handsome" wa Kitaa na hakuna mwanamke anayeweza kumkataa kama akimtaka.

  Tabia yake ilivuka mipaka mpaka kutembea na wake za watu hata marafiki zake aliokuwa anafanya nao Biashara. Lakini huyu jamaa alikuwa ana wivu wa kupindukia kwa mkewe. Alikuwa anamchunga Mkewe kuliko mtu anavyolinda fedha zake mfukoni akipita mitaa ya mateja.

  kuna wakati Mumewe huyu dada alitembea na mke wa mfanyabiashara mwenzake na isitoshe akaita na marafiki wenzake kumwingilia yule mwanamke baada ya kumlewesha. Tukio hilo halikubakia siri hatimaye mume wa yule mwanamke akajua alichotendewa mkewe na kuapa kulipiza.

  Kila jamaa akimtuma mtu kuweka fedha benki basi ni lazima ampe na shilingi 2000 (it was back in 1990s) za kwenda kumpa yule binti kama hela ya "lunch". Mwisho wa siku jamaa akatoka naye kwenda Disko. Wakiwa Disko shemeji yake na yule binti akamuona yuko na jamaa na kwa kuwa anaijua tabia ya wivu ya kaka yake akamuomba warudi nyumbani. lakini yule binti akakataa. Alirudi mwenyewe nyumbani usiku wa manane. Kama waliishia kucheza muziki tu au kuna kilichoendelea kati yake na yule jamaa hakuna anayejua hadi leo.

  Siku moja mumewe akawa anajigamba kwa wenzie kwamba yeye anao uwezo wa kuchukua mwanamke yeyote lakini hakuna mtu anayeweza kumchukua mkewe. Rafiki yake mmoja akamwambia kimafumbo "usilolijua ni usiku wa kiza" mazungumzo yao yaliishia kwa kwa jamaa kujua kumbe alipokuwa Dar kufunga mzingo huku nyuma mkewe alikwenda Disko na "adui" yake na hata mdogo wake anajua kwamba mkewe alikuwa Disko.

  Jamaa ghadhabu ikampanda akamfuata mkewe Saluni alikokuwa anasuka na kumchukua nusu kichwa kasukwa nusu kichwa bado, hadi nyumbani kwao na kumuingiza chumbani na kuanza kupiga kwa kutumia Isuzu Spring Bar. Juhudi za kumsihi aache kumpiga mkewe na afungue mlango zilishindikana mpaka pale mama yake mzazi aliposema "kama ukiendelea kumpiga mkeo mimi nakwenda kujinyonga" Jamaa akafungua mlango.

  Mlango ulipofunguliwa mkewe alikuwa kalala chini hajitambui na chumba chote kimetapakaa damu. Alipopelekwa Hospitali aligundulika mguu wake wa Kushoto umevunjika na mshipa mkubwa unaopitisha damu nao pia umekatika. Tangu hapo akawa mlemavu asiyeweza kutembea bila magongo na mraibu (Addict) wa madawa ya kutuliza maumivu.

  Kwa miaka zaidi ya Ishirini ameishi maisha hayo na mara ya mwisho nilikutana naye Agha Khan Hospital alikokuwa amekwenda kufanya Blood Detoxification (kusafisha damu) kutokana na kutumia kwa wingi dawa za kutuliza maumivu. Aliniambia "maisha yangu yako mikononi mwa mungu" siku zake za mwisho aliongozwa na imani yake kwa mungu.

  Kama si wivu wa mumewe huyu binti asingemalizia maisha yake hapa duniani kwa mateso namna ile. Bila shaka atasafirishwa Kesho kwenda Bukoba kwa Mazishi.

  Rest In Peace Dear Sister Flora!!

  UPDATE:
  Leo10/12/2005 Flora anazikwa kijijni kwao Bugandika nje kidogo ya Bukoba!!
   
 2. T

  TUMY JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni hadithi ama ni true story, kwani imekaa kama hadithi zaidi.
   
 3. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wivu mbaya sana.

  R.I.P Flora.
   
 4. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,659
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Ndivyo binadamu tulivyo..mtenda anapotendwa huona kaonewa.

  Imemuuma kujua mkewe nae ana kajamaa,wakati yeye ana dozen ya wanawake..womanizer!! Mungu amlaze mahali pema huyo dada..Poleni sana!
   
 5. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #5
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  mambo ya kweli hayo mkuu,ndio hivyo tena R.I.P Dada F
   
 6. nimie

  nimie JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ndo matatizo ya wanaume malimbukeni, ujinga wa kujifanya mafundi kwenye miili ya watu. Samahani, na huyo shemejio ni wa huko huko home kwenu? Haya maelezo yamenigusa sana. Poleni sana!
   
 7. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  tragic.....rip flora
   
 8. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ni kisa cha kweli kabisa kilichomtokea mtu ninayemfahamu kwa miaka mingi sana. Msiba uko Kijitonyama nyumbani kwake. Nimetumia neno "dada" kwa sababu nilimheshimu hivyo siku zote na yeye alinichukulia hivyo hivyo kuwa ni kaka yake. Ameacha watoto wawili wa kiume mmoja yuko Chuo Kikuu na mwingine anatarajia kusomea Comm. Dev pale kijitonyama.
   
 9. client3

  client3 JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2012
  Joined: Aug 6, 2007
  Messages: 742
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  mh yaani kama hadithi
  hii yaweza zua thread ingine kwa nini wanaume wa aina hii wakitendwa huwa mbogo,wengi wetu tungefikiri angebalance reaction yake kwa kuangalia yake
   
 10. h

  heshima nicholaus Member

  #10
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  its hurt,
   
 11. u

  utantambua JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha habari hii
   
 12. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #12
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ​huuuuuuuuuuuuhhhh...........................R.I.P dada Flora
   
 13. BRO LEE

  BRO LEE JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Kwa ukatili huo, huyo jamaa anatakiwa afumaniwe halafu wamkate, Pu@**#bu zake.

  Shwaiiini kabisaaa.
   
 14. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #14
  Jan 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  r.i.p dada flora
   
 15. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #15
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkuu nataka kuelewa baada ya tukio hilo jamaa aliachwq hivi au sheria ilichukua mkondo wake!!! RIP dada Flora.
   
 16. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #16
  Jan 7, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  inauma sana!

  Wanawake nao wanatakiwa wajiondoe kwenye ndoa/mahusiano ya namna hiyo
   
 17. H

  HHH Member

  #17
  Jan 7, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani hii imenigusa sana.
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  Jan 7, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  SAD. RIP Flora.
  Hopefully huyo bwana aliishia jela.
   
 19. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #19
  Jan 7, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,300
  Likes Received: 22,102
  Trophy Points: 280
  ANAITWA Flora nani, sema basi tujue ni kwa jinsi gani tutamuwajibisha mumewe
   
 20. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #20
  Jan 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  U a wrong Lizzy. Jamaa yuko Kitaa na anafanya biashara ya Hardware mitaa ya Kariakoo. Hajawahi hata kukamatwa kwa kosa hilo. Kitu pekee ninachokijua aliubeba mzigo wa matibabu ya mkewe hadi mwisho. Kuanzia Malago Hospitali Kuu ya Uganda hadi Kwa T.B. Joshua gharama zote hizo pamoja na zile za Blood Detoxification (280,000 Kwa wiki) jamaa alizibeba yeye. Hapo katikati alizaa mtoto na mwanamke mwingine!!

  Mikono ya sheria haikuwahi kumfikia!!
   
Loading...