Wivu hausaidii ngoja niandike tu nilichojifunza kitusaidie wote

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,558
3,466
Hakika naandika haya katika hali ya kuhakikisha kuwa tunatoka gizani na kuutazana ulimwengu katika mawanda mapana zaidi ya mazoea. Ninachakika tukitoka kwenye mazoea tutaitwa watu wa tofauti lakini tofauti hiyo ndiyo itakayotusaidia.

Natamani sana kila mmoja wetu kufikia hatua ya kuacha kupuuzia Kwa faida yake na vizazi vijavyo. Moja Kwa moja kwenye mada ni kwamba, maisha huanzia katika ulimwengu wa roho. Huanzia huko, hukamilika huko kisha huachiliwa kuwa kitu kinachojidjihirisha katika ulimwengu wa vitu "material world".

Kila kitu ufanyacho au uwazacho huachiliwa mimba katika ulimwengu wa roho na mwisho wa siku vitu halisi hujitokeza katika ulimwengu wa kawaida tunazoishi. Kanuni hii ya kiroho haikosei, ni sheria isiyopingwa wala kubadilika. Kuna vitu vina athari kubwa sana katika maisha yetu na tunavipuuzia hali inayosababisha kuendeleza katika mzunguko wa namna ileile bila kutoka nje ya mstari.

Mifumo ya elimu haituandai kuulewa ulimwengu wa roho na kuufanyia kazi kama ulivyo ulimwengu wa vitu. Elimu inayotolewa inatusaudia kuelewa vinavyoinekana anbavyo Kwa kweli ni vivuli tu au ishara ya vitu halisi vilivyopo katika ulimwengu wa roho. Mifumo michache inayotoa maarifa ya kukuza uelewa wa mwanadamu kiroho haitiliwi uzito sana na inaonekana kama aina fulani ya elimu au maarifa yasiyo na uhakika kutokana na imani kuwa " ukweli wa kitu au uhalisia wa kitu ni kuonekana kwake katika hali ya kitu". Tabia hii imekuwa ni kawaida na kawaida huzaa kawaida, jambo linaloifanya jamii ya binadamu kutoinuka zaidi ya inapopaona.

Ulimwengu wa roho ni halisi na unafanya kazi. Angalia mfano huu wa kawaida kabisa hisia kama upendo, chuki, huweza kuathiri mwili wa mwanadamu, lakini tujiulize je hisia zinaonekana? Hisia zipo wapi? Tunaweza kuzigusa kama vitu vingine?. Na, ni Kwa namna gani kitu kisicho cha kifizikali " kinachoonekana" huathiri kinachoonekana?. Sayansi hapa Inaweza ikajikita katika mkabala wa vitu na kutia majibu kama hisia ni tokeo la uwiano usio sawa wa kemikali za kimwili "imbalance of chemicals" lakini tukijiuliza ni nini lipo nyuma ya kukosekana kwa uwiano huo kuna mahali tutafika na kukosa jibu la kitu kionekanacho.

Leo tuna jamii isiyotaka kabisa kujua nyuma ya kinachoonekana na jambo la kusikitisha kabisa ni kule kuridhika na hali ilivyo. Akitokea mtu anazunhumzia maarifa yaliyo nje ya ulimwengu wa vitu huonekana ni kama mzimu au anatumiwa na nguvu nyingine isiyo ya kibinadamu.

Ipo haja ya kujali vitu fulani anbavyo haviogopwi, haviheshimiwi Waka havionekani Kwa sababu ndivyo vinavyozaa vinavyoinekana.

being-controlled_24381-897.jpg
 
Back
Top Bottom