Wivu, hasira, zinanisumbua

Mleta mada umenifanya niwe na :frusty: WIVU HASIRAAA :mad2:. . . .:rant:
****************Kudadadeki***************
 
Hilo Tatizo lako ni ugonjwa kama magonjwa mengine. Waone wataalam wa masuala ya saikolojia na pengine hudhuria kliniki za mapenzi zitakusaidia.
 
Jifunze kuweka subira katika kila kitu, akikuudhi mpenzi baada ya kugombana toka nje nenda kwa washikaji ukale stori, usiupe muda kuwa kwenye negativity na mtu. Ondoa mambo ya dhana pia yanazidi wivu, jaribu kuamini unachoelezwa sio kudhani dhani unless kama ni uwongo mweupe.....its practise.

Jifunze kuepuka au kuignore mgongano midogo midogo Eduin
 
Last edited by a moderator:
Eduin

0713 123 ... na kuendelea ni code number za full time employees wa tigo. Na ni mali ya tigo ukiacha kazi lazima uirudishe. We ni mfanyakazi wa tigo au unamuuzia mtu msala hapa??
 
Last edited by a moderator:
:coffee:Tuliza moyo mzee,,, sometimes tamaa mbaya,, kaa chini panga mipango yako ya kimaendeleo, ishu za wanawake achana nazo kwa sasa hivi... Jishughulishe na mambo ya maana vingine vitafuata man... Lastly jifunze kuzuia hasira yako!!:A S-coffee:
 
Wivu na hasira zako vina chanzo na kwa jinsi ulivyoandika, kuna uwezekano unasumbuliwa na kati ya mambo haya; Huridhiki na mwonekano wako, huridhiki na hali ya kiuchumi uliyonayo wakati unajiona unastahili kuwa na hali ya juu zaidi usiyoifikia pamoja na jitihada nyingi unazozifanya, Umezungukwa na watu waliokuzidi uwezo na huna la kufanya. Angalia pia mambo mengine ambayo yanakufanya usijiamini uyarekebishe kwani wivu na hasira mara nyingi huwa yanaletwa na kutojiamini ingawa kwa upande wa hasira inaweza kuletwa na factors nyingine nyingi pia.
Mfano, unaweza kuwa mbishi, mgumu wa kusikiliza wengine na usieshaurika, watu watadhani wewe ni mkali na mkorofi wakati kumbe kinachokusumbua ni hofu ya kudharaulika inayosababishwa na kutojiamini kutokana na kudhani kuwa watu wanakudharau kwa ufupi wa kimo chako, rangi ya ngozi, sura mbaya n.k na hivyo unakuwa mtu wa kujihami kwa kutanguliza hasira.
Si lazima uangukie katika hayo niliyotaja kwani kuna sababu nyingi nyingine zinaweza kusababisha hilo na anaezifahamu vyema ni wewe.
So jiulize ni kipi kinachokutia wasiwasi na kutojiamini ukirekebishe.
 
Namba ya simu uliyoweka ni ya makampuni ya ulinzi,zilitolewa katika siries za staff wa kampuni ya 0713
zote zilianza na 123.. baada ya code
sasa kwa hasira hizo na kampuni zenu si utakuja kuua kwa kirungu?

Hizo namba pia wanatumia Staff wa Tigo,so anaweza pia kuwa mfanyakazi wao.
Ok,Kujua tatizo lako ni nusu ya kulitatua,sasa basi usiwe unafuatilia mambo ya girl frend wako hasa simu yake,pia jitahidi kupuuzia mambo,nathani itasaidia lakini kama wewe ni Mkurya au Mhehe,basi Mungu aweke rehema zake tu,hiyo tabia ni by default. Am out,Enjoy ur lunch
 
good job! huyu jamaa kaandika km mtoto wa chekechea?What's ths?

Ameandika kama mdogo wangu wa form one akiwa shuleni ananitumia msg, " hlw ma C* naomba ni2mie elf 10 nina xhida nayo".
Huwa ananiudhi namjibu andika msg vizuri ndipo nikutumie hela yangu.
 
Uzur ushajua tatizo lako... Jaribu kuji-control uone matokeo
Utakapohisi WIVU au HASIRA assume ujaona wala ujui kinachoendelea...
 
yani wewe, huna huruma kweli..si unajua ana hasira, unaweza kuta amefura huko aliko na mtu ameshapata kibano, cause hiyo hasira yake najua sio kwa gf peke yake

Huyu ana vingi vya kufundishwa mkuu..mi nimejitolea hivyo
 
Hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu. Hayo ni maneno kwenye kitabu kitakatifu.
Je tangia umeanza kuwa na hasira imekusaidia kutatua matatizo au kuongeza? Hapo unajitaftia matatizo yasiyo na lazma. Jifunze kukubaliana na hali zilivo na kutokupaniki
ila wanawake kwenye mahusiano sometimes mnatia hasira sana
 
Back
Top Bottom