Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,103
- 128,718
Wanabodi,
Hii ni makala yangu kwenye gazeti la Nipashe la leo
Leo, naanza kwa maneno ya nyimbo mbili za zamani za muziki wa dansi, wa kwanza ni wimbo Fukara Hapendeki ulioimbwa na mwanamuzi Shabani Dede na bendi ya muziki ya Juwata Jazz Bend, JJB, wana Msondo Ngoma na wimbo wa pili ni Pesa Sabuni ya Roho wa Jabali la Muziki, Marijani Rajabu na Dar International.
Wimbo wa Fukara Hapendeki una maneno haya
“Nimekumbuka yangu ya dunia,
Maneno baba aliyoniambia,
Fukara hapendeki mbele za watu hata kidogo
Lolote asemalo wao watacheka,
Na kumuona bure tena hayawani,
Hata lenye maana watadharau na kupuuza,
Mola akikujalia na kazi ukipata,
Maisha raha sana, watakuona wa maana
Dharau haifai, na tena mbaya sana,
Muone kama mtu sio mpaka awe na kitu
Chorous
“Utu ni tabia njema, na wala sio pesa
Ada ya mja hunena, muungwaana ni kitendo”
View: https://youtu.be/rJ3G4fNRybw?si=N1VbM4vhbOelv7_j
Kisha nikamkumbuka Jabali la Muziki, Marijani Rajab, kwenye wimbo wake, Pesa Sabuni ya Roho, baadhi ya maneno ya wimbo huo ni
"Umasikini, japo hutokea kwa wananadamu,
lakini hakuna anayeupenda
Mli mradi mtu ufanyeje,
Huna la kufanya aha maua,
Oh masikini mie…
Hukufanya uwe mnyonge siku hadi siku,
Mnyonge pia huwa hana haki,
Mpaka mwenye nguvu apende.
Nalia mwana maua,
Oh masikini mie…
Chorous
“ Pesa pesa, pesa ndio sabuni ya roho
mwenye pesa, mwenye pesa sio mwenzio, nasema… x 2
kila penye uzia wewe penyeza rupia, jamani pesa ohh, ilivunja ng’ombe na milima, wakale walisema,
Chorous
Mwenye pesa akifika, watu wote husimama, kila analolisema watu hulipa uzito, pesa pesa,
View: https://youtu.be/dRc5I3GnErM?si=zkyBPWlSJgV0JplF
Nimeyakumbuka maneno haya, kufuatilia mchaka mchaka wa harakati za vyama vya siasa kujiandaa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, japo lengo kuu la uchaguzi ni kupata viongozi bora, na sio bora viongozi, na hakuna ubishi, kuhusu umuhimu wa fedha za kugharimia kampeni za uchaguzi, enzi zetu za zamani, enzi zile za TANU, namna ya kuwaita watu kwenye mikutano ya hadhara, ilikuwa ni inapigwa tuu mbiu, au lamgambo likilia, watu wanakusanyika, wakijua kuna jambo, watu walikuwa wanachangishwa senti tano tano, senti kumi, senti 20, thumuni na shilingi moja!, enzi hizi kulikuwa na noti ya silingi tano!.
Enzi hizo, sifa kuu za uongozi ni uwezo wa mtu na kujituma kwake kutumikia jamii, na sio fedha, Chama cha TANU na baadae CCM ni chama cha makabwela, ni chama cha wanyonge, ni chama cha wakulima na wafanyakazi.
Baada ya TANU kutangaza siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, pia kiliweka miiko ya uongozi, utajiri ulikuwa ni disqualification, matajiri walikuwa ni ama wafanyabiashara walioitwa, mabepari, ama wamiliki wa aridhi na mashamba makubwa walioitwa makabaila, ama wamiliki wa majumba walioitwa ma bwanyenye. Mwalimu Nyerere akatoa ile misingi minne ya ili tuendelee tunahitaji vitu vinne, Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora, fedha sii msingi, fedha ni matokeo!.
Kufuatia maendeleo na mabadiliko ya usasa, mambo yakabadilika, maisha nayo yamebadilika, maisha ya zamani yalikuwa maisha ya ukweli, kuliko maisha ya vitu, kwa kizungu “life wa more realistic than materialistic”, lakini sasa maisha ni kama unakitu, yaani “life is more materialistic than realistic”, thamani ya mtu sio tena ule utu wake bali anaangaliwa ana nini?, kama hana kitu, wewe ni lofa tuu!. Heshima ya mtu sasa sio utu ni pesa!, sasa pesa imekuwa ndio kila kitu!.
CCM nayo ikabadilika, Azimio la Arusha likazikwa, likaibuka Azimio la Zanzibar, likaifuta ile miiko ya uongozi, siasa zikageuzwa fedha, viongozi wakaanza kuwa majajiri na ukitaka uongozi, sasa kipimo cha kwanza ni sio tena sifa za uongozi, bali sasa ni fedha!. Zamani fomu za uongozi ni bure, leo fomu za uongozi ni fedha, Udiwani laki, ubunge, milioni, urais milioni 5!. Akina pangu pakavu tia mchuzi, kama huna pesa, huna chako, mkono mtupu haulambwi!. Ungozi wa kisasa ni uongozi wa kununua, lazima uwe na fedha za kununua fomu!.
Siku hizi, pesa ndio sifa ya kwanza ya kugombea uongozi, hivyo wakati vyama vinachangisha fedha kugarimia uchaguzi, tumeshuhudia matajiri wakijitokeza kwa wingi kugharimia harambee ya chama cha siasa, na shilingi bilioni 100, zimepatikana ndani ya siku moja!. Nilishiriki ile kampeni ta TEA kutafuta michango ya kusaidia elimu, au michango ya kuchangia huduma za afya na hata kunapotokea majanga mbalimbali jinsi watu na taasisi wanavyojitokeza kwa kusuasua, na kuchangia siasa, bilioni 100 fasta ndani ya siku moja!. Hii maana yake siasa zetu za kisasa ni siasa za fedha!, mwenye nacho anaongezewa, na asianacho ananyanganywa hata kile kidogo alichonacho!.
Pesa ndefu kwa lugha ya watoto wa mjini, inaitwa ‘kisu’, mwenye kisu kikali ndio anakula nyama!,
Ombi kwa Vyama, Wanasiasa na Wananchi, japo siasa zetu sasa siasa za pesa mbele, natoa wito “Tusitumie pesa kama fimbo” ya kuwachapia, vyama visivyo na pesa na viongozi wazuri wasio na pesa, kwa kutokuwachagua kutokana na kutokuwa na pesa, mafukara au kuwa na mkono mtupu!. Kuna watu wana pesa ndefu lakini ni viongozi mabomu, na kuna watu hawana kitu kabisa lakini ni viongozi wazuri. Tusitumie pesa kama fimbo ya kuwachagua wenye nazo na kuwachapia wasio nazo!.
Wananchi, wanasiasa, wenye nazo, wakimwaga pesa, wananchi, chukueni!, vyama vikigawa takrima, tshet, kofia, khanga na vitenge, pokeeni, watakao walisha watu ubwabwa, biryani na pilau, kuleni, lakini siku ya uchaguzi, nenda kachague kiongozi bora, hata kama hana kitu!. Uongozi ni uwezo wa kiongozi kutuletea maendeleo na sio uwezo wa kiongozi au chama kutumwagia mapesa!.
Tukachague viongozi bora na sio tukachague viongozi mli mradi ni kiongozi, yaani bora kiongozi kwasababu tuu ana pesa, na amemwaga pesa!.
Japo TAKUKURU ipo, lakini amini nakuambia, Takukuru hamna kitu kwa kinachoendelea!. Kama mchago tuu kutachingia chama, watu wamemwaga mabilioni, bila kujua yametoka wapi, TRA kimya, Takukuru ataweza kufanya nini?!.
Mungu Ibariki Tanzania!.
Paskali.