Kitaja
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 2,836
- 1,382
Ndugu wana JF habari za mchana,
Ningependa kutoa maoni yangu na ushauri kwa serikali yetu sikivu kuhusu umuhimu wa kuwa na online database ikionyesha wasifu ama CV za viongozi wetu wa kisiasa hasa wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na mawaziri. Jambo hili si tu kuwa litarahisisha wananchi kuwajua viongozi wao bali pia zitasaidia mamlaka za uteuzi kupata taarifa muhimu za wateuliwa wao. Hivi sasa nchi yetu iko katika vita kubwa kusaka na kutokomeza watumishi hewa sambamba na ukaguzi wa vyeti feki. Jambo hili hufanyika kw watumishi wa kada za chini tu ilihali wale wakubwa wakubwa wnazidi kupeta na vyeti vya kufoji. Kama ilivyo bungeni kuna kwenye tovuti yao kuna wasifu wa wabunge wote.Hii imerhisisha wananchi kupata taarifa za mbunge husika pale zinapohitajika. Jambo hili likifanikiwa pia litasaidia kuondoa "kiwingu" kwa viongozi wetu wandamizi wanotuhumiwa kuwa walifoji vyeti ama walinunua majina ya watu wengine,n.k.
Ni hayo tu kwa leo, karibuni kwa maoni.