Wito: Mjadala fao la kujitoa urudiwe

Wito: Mjadala fao la kujitoa urudiwe

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
651
Reaction score
854
Kama Mtanzania na kama raia wengine wa taifa hili ninayo haki kikatiba ya kutoa maoni kuhusu jambo lolote linalohusu jamii yangu kwa maslahi mapana ya taifa. Kwa hivyo basi, napenda kuchukua nafasi hii kutoa wito wangu ili mjadala kuhusu fao la kujitoa uanzishwe kwa kushirikisha wadau muhimu katika suala hili.

Itakumbukwa kwamba, mwezi Februari, 2018 kulikuwa na mjadala kuhusu marekebisho ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambapo fao la kujitoa lilikuwa sehemu ya mjadala huo. Hadi mwisho wa siku, maamuzi yalifuta utaratibu wa fao la kujitoa.

Kwa nini natoa wito kwa jambo hili?

Tangu wakati wa mjadala huo hadi hivi sasa baada ya muswada huo kupitishwa na bunge kwa kufuta fao la kujitoa, kumekuwa na maoni ambayo yanakinzana na maamuzi ya kufutwa fao la kujitoa. Tuliambiwa kwamba, vyama vya wafanyakazi vilishirikishwa katika hatua muhimu za jambo hili hadi kufika hapa lilipo. Ila ukiuliza maoni ya wengi ambao kimsingi ndiyo wenye fedha hizo kwenye mifuko ya jamii, utagundua kuwa, maoni yao hayakufanyiwa kazi au yalipuuzwa, kitu ambacho kwa mtazamo wangu haikuwa sahihi. Kwa hali hii, hata kama vyama vya wafanyakazi vilishirikishwa, basi havikuwasilisha maoni sahihi na halisi, au matakwa na mapendekezo ya wafanyakazi ambao ndiyo wenye fedha hizo. Kwa sababu hii, kuna umuhimu wa kuanzisha mjadala mpana utakaowashirikisha wadau wote muhimu kwa maana ya wafanyakazi moja kwa moja, na wengineo ili mwisho wa siku kila mmoja aondoke akiwa karidhika.

Nawasilisha.
 
  • Thanks
Reactions: 454
tumeshachelewa ndugu.... ngoma imeshafutwa hiyoo

Laws are not curved in stone ndugu. Kama kuna watu huenda mahakamani ku-challenge sheria zilizopo na wanapata ushindi, kwa nini hili lisiwezekane?
 
Hawajapitisha kwa bahati mbaya au sio kwamba hawajui kua "nyie wenye hela zenu" hamjaridhika ???Hapana,

Wamepitisha makusudi na hakuna kitakachobadilika.


Poleni
 
tumeshachelewa ndugu.... ngoma imeshafutwa hiyoo
2012 walipitisha lakini baadae walirudi tena bungeni na kurudisha upya kisha tukaanza kuvuta...yaani nikiona neno fao la kujitoa mapigo ya moyo yanaenda kasi
 
Mambo kama haya ndio sisi wengine yanatuumizaga tu mtu unafanyakazi kwa mhindi miezi 3 fao la kujitoa miaka55 kweli? na kazi zetu zimeadimika sana
 
Laws are not curved in stone ndugu. Kama kuna watu huenda mahakamani ku-challenge sheria zilizopo na wanapata ushindi, kwa nini hili lisiwezekane?
Wakilirudisha pesa za kuhonga kina MTULIA na kurudia chaguzi uchwara watazitoa wapi ?
 
Hoja hii ulikiunganishwa kwenye madai ya Mange aisee fao linatolewa fasta tu mbona
 
umeusoma huo muswada?? ni wapi wamesema watalipa hadi ufikishe hyo miaka 55??
mm nimeusoma line by line, kiukwel tatizo ni uelewa wa watu aisee! niulize swali lolote kuhusu huo muswada ntakujibu!
Kama hawatalipa baada ya mfanyakazi kufika miaka 55 je ukweli ni upi!?

Inawezekana mimi kulipwa sasa fao la kujitoa!!

Naomba ufafanuzi kwako uliesoma line kwa line, utaratibu ukoje!?
 
Tatizo moja la sisi watanzania ni kutokujua kuwa Fao la kujitoa halipo na halijawahi kuwepo wala halitakaa liwepo.Unaweza kusema urudishiwe michango yako yote hilo hawawezi kuzuia hata kwa sheria kwa sababu social security sio universal yaani si kwamba kila mtu analipwa pensheni ya uzeeni wanaolipwa ni wale wanaochangia na kutimiza vigezo na masharti.Kwa sababu hiyo basi unapohitaji kujitoa nenda NSSF au kwenye mfuko wowote wambie unataka kurudishiwa michango yako.Wakikataa kukrudishia nenda mahakamani ufungue kesi ya madai dhidi ya NSSF kwamba wanataka kudhulumu.Hakikisha una sababu za maana na msingi.Na mahakama itakupa hki yako kwani hizo pesa sio mali ya mfuko ni mali ya wanachama.Mfuko ni wasimamizi tu
 
Maana mimi naelekea uko kukosa ajira maana kila mwisho wa mwezi majina kwenye ubao sasa hii habari hinazidi kunichanganya tu
 
hakuna fao LA kujitoa badala yake lipo fao la ukosefu wa ajira ambalo kila kitu ni kama ilivyokuwa kwenye fao LA kujitoa!
Countrywide, unaposema kuwa 'kila kitu ni kama ilivyokuwa kwenye fao la kujitoa' una uhakika au na wewe umesikia fununu tu? Si kweli kwamba kila kitu kipo kama ilivyo kwenye fao la kujitoa. Ukweli ni kwamba, kwa miezi sita utalipwa asilimia 33 ya mshahara wako, baada ya hapo kama haujapata ajira, itabidi tena usubiri miezi kumi na nane ndipo upewe salio lako lililobaki toka sehemu ya nusu ya michango yako yote, zingatia kuwa, umekuwa ukichukua asilimia 33 kwa miezi sita. Kwa hivyo basi, kama michango yako ni milioni 10, basi gawanya mara mbili. Hivyo ni sawa na kusema, milioni 5 kutoa asilimia 33 ya mshahara wako kwa miezi sita, hapo utapata jibu. Kwa maelezo yangu hayo kwa mujibu wa muswada huo kama ilivyofafanuliwa na wabunge, fao la kukosa ajira si sawa na fao la kujitoa. Sarakasi tu zimejaa.
 
hakuna fao LA kujitoa badala yake lipo fao la ukosefu wa ajira ambalo kila kitu ni kama ilivyokuwa kwenye fao LA kujitoa!
Ww huna akili..PPF walikuja kazini kwetu kutudadavulia..na walipigilia musmari kuwa fao la kujitoa tutalipwa mpaka ufike miaka 55 ..hapo tulipngea na direct wafanyakazi wa Ppf..

Kilichobaki ni mbwmbwe.kuzunguka mbuyu tu. ..

Zamani ulikuwa ukiachishwa kazi au uki.termninate contract unaenda kuchuku mafao yako maana ni haki yako

Narudia tena...unapoacha kazi hutopata hela yako mpaka ufike miaka 55..huu ni wizi kama wizi mwingine
 
hivi ni nani aliyewaambia mtalipwa baada ya miaka 55?? huo muswafa wote mbona upo wazi, ulisomwa bungeni na umewekwa pia kwenye tovuti ya bunge!
Nenda PPF utapata majibu..mimi na rafiki yangu ameacha kazi since 2016.. hadi leo hajapewa hela na PPf tena ana zaidi ya milion 19 ...halafu ww unaleta siasa kwenye mambo magumu.

Inauma mtu kukaa mtaani huna deal au mkataba wako umekuwa termited.then unanyimwa hela yako...huku una matatizo lukuki yanakuzunguka
 
sio kweli! tatzo letu wabongo ni wavivu sana kusoma na kufatilia, ingia tovuti ya bunge tafuta huo muswada alafu uusone tena!
Kikubwa ni hela ..acha mambo ya bungeni...

Ww unasema niende kusoma tovuti ya bunge huku.kukiwa na mtu ana miaka miwili kanyimwa hela yake 19 mio kutokana na sheria hiyo kandamizi

Zamani..mfanyakazi akiacha kaZi 'alikuwa anakaa mwezi mmoja anapata hela yake

But now.mfano ofice yangu..wafanyakazi kibao wa toka mwaka 2016,June hawajapata hata sh.kumi toka implementation ya sheria hii

Sasa hilo andiko la bunge litasaidia nini wakati mimi nataka hela..sijui nitakula hiyo nakala
 
Countrywide, basi tufanye sijausoma. Nisaidie unasemaje muswada huo. Maana tusiandikie mate ilihali wino upo.
Mfano PPF toka 2016 hawajatoa hela..sasa huo muswada unakuwa na msaada gani kwa mtu wa kati ambaye hata tovuti haijui ya bunge...

Mifano ipo mingi...watu kibao wanalia kutopata stahiki zao
 
Back
Top Bottom