Wito: Maji na Umeme; Pesa za EPA zitunusuru!

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,530
Kuna mtu katoa tamko kuwa pesa za EPA zi inusuru TANESCO, nafikiri ni Slaa.

Nakubaliana naye kabisa, ili kuikwamua nchi yetu kutoka janga la kuangamia kiuchumi na hata kuumia kwa wananchi kutokana na kubebeshwa mzigo wa madeni na mikataba mibovu ya Tanesco, Serikali kwa kupitia BOT, itumie pesa zote inazozikusanya kutoka urudishwaji wa mchoto wa EPA kuinusuru Tanesco na kuipatia zana na uwezo wa kutoa umeme bila kokoro na kupunguza gharama hizi kwa wananchi.

Benki Kuu ya Marekani na kupitia Serikali yake, imewahi mara kadhaa kutoa fadhila za kusaidia makampuni na mashirika yasiangamie au kubebesha mzigo wananchi wake kwa kuongeza gharama. Baada ya 9/11. Serikali ilitoa fungu la pesa na mipango ya kiuchumi kusaidia mashirika ya ndege ya Marekani.

Wiki iliyopita, serikali hiyo hiyo kupitia Benki Kuu (Federal Reserve Bank) imelinusuru lile benki la uwekezaji na maendeleo Bear Stearns kutoka kufilisika na hivyo kuokoa japo kiduchu, ajira za wafanyakazi, pensheni zao na mali za wote wenye hisa.

Je inatushindwa nini kwa BOT kutoa msaada kama huu kwa Tanesco na Mamlaka za maji?

Ikiwa pesa za EPA ni Bilioni 133, na hizo nyingine za Buhemba ni Bilioni 155, ukiongeza CIS na upupu mwingine, inawezekana pesa zinazotomiwa hovyo na kuhujumiwa ni karibu Bilioni 500, kwa nini basi tusiipe Tanesco pesa za mtaji kufufua mitambo yote na kununua mipya, kuwasamehe Tanesco kodi au madeni kwa Serikali kwa miaka 5 ili Tanesco iweze kuweka tija na juhudi zake kuzalisha umeme (kwa bei ambayo Wananchi wanaweza kuimudu kutokana na hali halisi ya maisha na vipato), huku mikataba bomu iliyofanyika ya IPTL na RDC ikivunjwa?

Je Serikali imeshajiuliza gharama za Taifa kukosa uzalishaji kutokana na uhaba wa Umeme au maji?

Kwenye mambo ya maji, suala si Dar Es Salaam pekee, bali ni nchi nzima, MPanda wanahitaji Bilioni 20 kuboresha kilimo cha imwagiliaji, sehemu ingine nafikiri ni Mtwara wanahitaji Milioni 500, je kwa nini tusitoe kipaumbele kwa kuhakikisha kuwa maji yanapatikana ili wananchi waachane na taabu na adha za kutafuta maji safi (afya) na umwagiliaji (uzalishaji mali)?

Narudia tena, ikiwa tulikuwa na pesa nyingi kiasi hicho cha kulipia madeni hewa na kuruhusu uhujumu, kwa nini basi tusitumie pesa hizo kusaidia vitu muhimu kwa nchi yetu kutuondosha katika umasikini na maradhi na kuendelea kuwa omba omba?

Hapo bado hatujagusia elimu wala afya! ni maji na umeme tu!
 
Back
Top Bottom