Wito kwa vijana wote na wazee wanaojitambua juu ya kuipata katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Say no to actors

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
638
1,000
Ndugu wadau habari zenu...
Pasipo kupoteza muda nianze kwa kujitambulisha kuwa mm ni mtanzania halisi, mzalendo wa kweli na mwenye nia njema ya kupata taifa lenye malengo, maadili, na maendeleo kwa ujumla wake.

Katika kipindi cha kwanza cha awamu ya NNE kuna kundi kubwa la watu liliibuka kudai katiba mpya na nia njema aliyekuwa rais kipindi hicho alikubali kusikiliza hilo hitaji la watanzania na kuamua kuunda tume ya kukusanya maoni maarufu kama tume ya warioba.

Time ilifanya kazi yake vizuri kama tulivyoshuhudia lakini baadaye watu wachache kwa maslahi yao binafsi waliingilia mchakato na kuamua kukanyaga maoni ya watanzania walio wengi.

Leo hii rais amesema katika orodha ya vipaumbele vyake hakuna kitu kinachoitwa Katiba mpya na kwa mantiki hiyo hata tume huru ya uchaguzi kwa Tanzania tusitegemee. Kwa kusema hayo nawaomba vijana wote wenye vyama na wasiokuwa na vyama na pasipokujali tofauti za vyama vyetu tuungane pamoja kama MOVEMENT ya kudai katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi.

Tunapenda Magufuri ajue kuwa katiba tunayohitaji hatuhitaji kama hisani kutoka kwake bali ni lazima tuipate apende na au asipende hiyo ni lazima.

Tunaitaka tume huru ya uchaguzi na wala isiwe husani kutoka kwake ni lazima tulifie taifa kuliko kukifia chama.

Ndugu yangu polepole nakuomba hasa kama wewe si mnafika jiunge na movement hii rudia na uyakumbuke maneno yako ya zamani kuhusu maoni ya wananchi.

Mzee wangu Warioba kama kweli wewe si mnafiki basi ni wakati sasa kuidai katiba ulioisimamia na tume huru ya uchaguzi.

Prof Kabudi huko TIB hakuna katiba mpya unahitajika sana katika mapambano Haya. Kwa kijana yeyote ambaye yuko tiyari kwa kujiunga na movement hii anicheck inbox. Ahsanteni
 

mpiga domo

JF-Expert Member
Apr 30, 2013
835
1,000
Ulianza vizuri ila mwishoni umeharibu ulivyomtaja Pole Pole, kama hamkuweza kujua nia yake tangu mwanzo basi hamna budi kufanyiwa haya mnayofanyiwa sasa.
 

Madam Mwajuma

Verified Member
Sep 13, 2014
6,964
2,000
Naomba kwanza ubainishe vifungu vya katiba ya zamani ambavyo ni vibaya vinahitaji marekebisho usijekuwa unakataa kitu ambacho hukijui.
 

Kibstec

JF-Expert Member
May 21, 2016
1,205
2,000
Ndugu wadau habari zenu...
Pasipo kupoteza muda nianze kwa kujitambulisha kuwa mm ni mtanzania halisi, mzalendo wa kweli na mwenye nia njema ya kupata taifa lenye malengo, maadili, na maendeleo kwa ujumla wake. Katika kipindi cha kwanza cha awamu ya NNE kuna kundi kubwa la watu liliibuka kudai katiba mpya na nia njema aliyekuwa rais kipindi hicho alikubali kusikiliza hilo hitaji la watanzania na kuamua kuunda tume ya kukusanya maoni maarufu kama tume ya warioba. Time ilifanya kazi yake vizuri kama tulivyoshuhudia lakini baadaye watu wachache kwa maslahi yao binafsi waliingilia mchakato na kuamua kukanyaga maoni ya watanzania walio wengi. Leo hii rais amesema katika orodha ya vipaumbele vyake hakuna kitu kinachoitwa Katiba mpya na kwa mantiki hiyo hata tume huru ya uchaguzi kwa Tanzania tusitegemee. Kwa kusema hayo nawaomba vijana wote wenye vyama na wasiokuwa na vyama na pasipokujali tofauti za vyama vyetu tuungane pamoja kama MOVEMENT ya kudai katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi. Tunapenda Magufuri ajue kuwa katiba tunayohitaji hatuhitaji kama hisani kutoka kwake bali ni lazima tuipate apende na au asipende hiyo ni lazima. Tunaitaka tume huru ya uchaguzi na wala isiwe husani kutoka kwake ni lazima tulifie taifa kuliko kukifia chama. Ndugu yangu polepole nakuomba hasa kama wewe si mnafika jiunge na movement hii rudia na uyakumbuke maneno yako ya zamani kuhusu maoni ya wananchi. Mzee wangu Warioba kama kweli wewe si mnafiki basi ni wakati sasa kuidai katiba ulioisimamia na tume huru ya uchaguzi. Prof Kabudi huko TIB hakuna katiba mpya unahitajika sana katika mapambano Haya. Kwa kijana yeyote ambaye yuko tiyari kwa kujiunga na movement hii anicheck inbox. Ahsanteni
HUU TUNAITA UNAFIKI...kama kweli una nia ya DHATI EXPOSE YOUR TRUE IDENTITY ili usiwafanye watu wawe waoga hata kukufata huko INBOX.......maaana jambo unalotakiwa kulipigania si jambo dogo HIVYO TOKA HUKO SHIMONI...Eti wakufate inbox tutakuamini vipi???....
 

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,374
2,000
Katiba iliyopo inatosha. Halafu shida yetu kubwa ilikuwa ni ufisadi sio katibaa.
Sasa unajua mafisadi ni akina nani? ESCROW, LUGUMI, RICHMOND ---unawajua hawa pamoja na mitandao yao?

Unajua kwa nini Serikali ya CCM haitaki kumpeleka LOWASSA mahakamani?

Unajua kwa nini ESCROW waliochota pesa kwa magunia na masalphate majina yao yamefichwa?

Ni Ukweli KATIBA ina Matatizo:

A - Tume huru ya Uchaguzi

B- Mamlaka ya Raisi

C- Vyombo vya dola kuingiliwa na wanasiasa

D - Elimu na Afya vimedorora
 

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,096
2,000
Sasa unajua mafisadi ni akina nani? ESCROW, LUGUMI, RICHMOND ---unawajua hawa pamoja na mitandao yao?

Unajua kwa nini Serikali ya CCM haitaki kumpeleka LOWASSA mahakamani?

Unajua kwa nini ESCROW waliochota pesa kwa magunia na masalphate majina yao yamefichwa?

Ni Ukweli KATIBA ina Matatizo:

A - Tume huru ya Uchaguzi

B- Mamlaka ya Raisi

C- Vyombo vya dola kuingiliwa na wanasiasa

D - Elimu na Afya vimedorora
Achana nae huyu hajui asemacho!!
 

Say no to actors

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
638
1,000
Naomba kwanza ubainishe vifungu vya katiba ya zamani ambavyo ni vibaya vinahitaji marekebisho usijekuwa unakataa kitu ambacho hukijui.
Naomba kutaja orodha ya mabaya ktk katiba iliyopo:
1. Kukosa ushiriki wakati wa kuandika
2. Uchache na ufinyu wa haki za binadamu
3. Ubovu wa tume ya uchaguzi
4. Uchaguzi wa rais kutokuhojiwa na mahakama
5. Kujataliwa kwa mgombea guru
6. Kukosekana dira na dhima ya taifa
7. Kupuuza haki ya kumiliki ardhi
8.Katiba kutokumtambua Mungu
9. Kulimbikiza madaraka kwa raise
10.Utata kuhusu muungano
11. Kukosekana kikomo cha muda wa uwaziri na ubunge
12.Kutopambanua mfumo na mwelekeo wa uchumi wa taifa
13. Kuunganisha serikali na binge , ni.
 

ChamaDola

JF-Expert Member
Dec 23, 2016
3,436
2,000
Mie Nasubiria Hio Movement Ianze,Nione Kama Maandishi Yako Hapo Juu Yataakisi Matendo!
Maana Porojo Zimezidi!
 

Mndali ndanyelakakomu

JF-Expert Member
Dec 14, 2016
12,965
2,000
Vijana tunachanganywa na wana siasa kama katiba itatungwa nje na wanasiasa tutafanikiwa lakini kama wale walio pitisha katiba mbovu na wale walio susia katiba watakuwepo basi katiba mpya tusahau.
 

Say no to actors

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
638
1,000
N
Vijana tunachanganywa na wana siasa kama katiba itatungwa nje na wanasiasa tutafanikiwa lakini kama wale walio pitisha katiba mbovu na wale walio susia katiba watakuwepo basi katiba mpya tusahau.
Ndo maana sijasema wanasiasa japokuwa naona ni wadau wakubwa lakini jambo la msingi ni kuwa kijana ndiye nguzo ya mabadiliko kamwe tusitegemee wazee kwa hili tushikamane haswaa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom