Wito kwa madereva wa IST jiji Dar es salaam

gudJohnson

Member
Aug 24, 2015
33
54
Habari za leo ndugu madereva mnaoendesha gari aina ya Toyota IST hapa jijini Dar na kwingineko kote Tanzania.

Awali ya yote niwapongeze kwa hatua ya kumiliki usafiri ambao unawawezesha kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa wakati. Hiyo ni hatua muhimu ya maisha ambayo kila mmoja angetamani kuifikia.

Dhumuni la waraka huu ni kuwaomba sana muwe makini mnapokua barabarani. Baadhi yenu mmekua na tabia mbaya sana muwapo barabarani na kujiona kwamba nyie ndo mna haraka sana kuliko watumiaji wengine wa barabara.

Kumekua na matukio mengi ya ku-overtake bila umakini (recklessly) na kupelekea kero kwa watumiaji wengine barabarani. Yani unakuta kajamaa kamejikunja kwenye ka-IST kake, halafu kanajifanya ndio kana haraka kuliko wengine. Jamani, sio kwamba huto tugari twenu ndo tunakimbia kuliko haya ma Ford Ranger yetu. Nawaomba sana muwe wastaarabu kwenye uendeshaji wa tugari twenu jamani.

Wito wangu kwenu ni kwamba muwe na adabu na nidhamu mnapokua barabarani ili sote kwa pamoja tutumie barabara zetu kwa uhuru.

Naomba kuwasilisha.
 
Duh nilifikiri ni mimi peke yangu ndio nimeona tabia za ajabu ajabu za madereva wa IST! Nimejiuliza sana kwanini au ndio kama bodaboda ukishapanda unapata uchizi?! Kusema ukweli madereva wanaoongoza kwa fujo barabarani ni IST, labda wanasumbuliwa na SMS-short man syndrome.
 
Kabisa mkuu halaf ikitokea amekukwangua anakua mdogo kama piriton maana hana hela ya kukulipa.....tuungane kuwakemea
 
Hili jambo ni kweli kabisa kuna siku nilipanda IST moja hadi nikamuuliza dereva leo una haraka sana enh? Maana IST mtu ana rev mpaka kwenye 3-4 hadi unashangaa nini tatizo
 
Hahahahaha, unakuta jamaa/jimama mnene na mzito kuliko kigari chenyewe.
Halafu wana rafu sana barabarani.

Hivi vigari vinavumilia mengi kama wake zetu wanavyovumilia harufu kama ya kopo la chooni sababu ya harufu ya matapu tapu/henkein/ndovu tunayogida kila siku.

Jamaa una dharau wewe na range rover lako.

Hivyo vigari wanahongwa akina nani eti?

Kidding
 
Hzo gari nyingi za biashara ya usafirishaji so mtu anakimbizana na muda ili asipate hasara.
Sio IST tu peke yake bali gari zoote za biashara hasa hasa Uber na Taxfy huwezi kuta dereva analaza damu hata mara moja mana unakuta amebeba abiria halafu zinaingia request nyingine kama tatu hivi sasa unategemea atembee mwendo gani kama sio wa haraka akushushe ili amuwahi mteja mwingine.
Tusiwalaumu ni nature ya kazi inawalazimu kuwa shapu muda wote wakiwa kazini.
 
Kwamba IST zote hapa mjini zinafanya biashara?
 
Wanafujo hao hata hawatuangaliagi watembea kwa miguu wao nikukimbia tu hata sehemu zisizotakiwa kukimbia, hata sehemu kama city mule ndani mtu anakimbia mpaka unashangaa jamani
 
Hujakosea kabisa....madereva wa IST mnatukosa kosa mno barabarani.....chondechonde....ghafla nazo madereva mukichwa wanaendesha yale makubwa ya serekale....
 
Back
Top Bottom