Wireless Mouse.

g.n.n

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2010
Posts
407
Reaction score
49
Wadau, kwa aliye wahi kutumia hizi wire-less mouse naomba anijuze uimara wake maana kuna sister hapa chuo anaziuza zinaitwa Gmax kwa sh 15000 so sijawaha sure sana zinaweza kudumu kwa mda gani.
 
Kuna moja nilinunua ilikaa kwa saa kadhaa kama 4hrs ikafa,kuwa makini tu ndugu. Tafuta za HP ni nzuri.
 
Wadau, kwa aliye wahi kutumia hizi wire-less mouse naomba anijuze uimara wake maana kuna sister hapa chuo anaziuza zinaitwa Gmax kwa sh 15000 so sijawaha sure sana zinaweza kudumu kwa mda gani.

Bora ununue usb mousr hizo za wireless utakua unaingia gharama za battery
 
Bora ununue usb mousr hizo za wireless utakua unaingia gharama za battery

Ni kweli ghalama ya Betry ipo, lakini pia ni nzuri kwa kua unaweza kucontrol kama remote control haswa sisi watu tuopenda muvie. Halafu betry ni 200tu bado sijaona kama ni ghalama.
 
Mimi natumia Wireless Mouse mwaka wa tatu sasa, na haijawahi kuniangusha. Very potable and all. Hii inaitwa ''4TECH''. Nikinunua battery mbili Duracell zinalkaa zaidi ya mwezi
 
Huwa hazina tabu we angalia brand nzuri wala hutojuta.Mimi natumia mwaka wa nne sasa na hakuna issue yoyote. Kazi ni kununua betri tu.
 
Wadau, kwa aliye wahi kutumia hizi wire-less mouse naomba anijuze uimara wake maana kuna sister hapa chuo anaziuza zinaitwa Gmax kwa sh 15000 so sijawaha sure sana zinaweza kudumu kwa mda gani.

ziko poa tu ila betri tumia zaidi zile alkaline betri zinadumu sana ndio huwa natumia mie.. huu ni mwezi wa kumi sasa..
 
Nunua utumie uone inakuwaje kwani wakati mwingine tunajifunza kutokana na makosa .
 
Mimi nakushauri kama huna mzuka nazo uzipotezee tu manake hazina lolote zinakera sanaa yani ni zinasumbua sana.
 
hapo lazima utumie duracell sungura mjanja lakini ukitumia betri za mchina kila siku utakua unanunu betri
 
Zipo imara sasa inategemea na mambo ya kawaida lipa bei che tegemea u che.

Mimi natumia kwa kilasiku na laptop na notebook na hata wireless keyboard zinadumu natumia logitech sababu nazipenda.

Hiyo uliyoisema siijui ilaunaweza ingia online kama google sechi weka jina la product etc na neno review mengi huja utasoma. Ila kama ukitype jina na vimodel unaona haviji basi hapo shtuka kujua sio vingi vitumikavyo.

Mara nyingi bora kuongeza pesa kidogo na kupata kitu imara kisicho feki, kuna brand ingine nadhani ni logik nayo poa na etc
 
Nimewasoma wadau, sema kama nishanunu Mouse-Apple, imekaa mpango shape yake ipo poa, nimehisi wireless itanisumbua baadae, sema yenyewe ni nyeusi, nimechukua kwa 10 kariakoo pale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…