Wingi wa maarifa na hatari YA sonona

YASIYOSEMWA

Member
Joined
Jun 1, 2026
Posts
68
Reaction score
149
Simple observation nilioifanya Naona watu wenye maarifa kiduchu na taarifa chache juu ya ulimwengu na hekaheka zake wanafuraha kuliko wasomi na wajuvi wa mambo.

Wao masuala kama YA Vita na mashindano YA geopolitics hawana habari nayo,mambo YA ushabiki wa Mpira,Maisha mlinganisho YA mitandaoni Kwao Hayana nafasi

Kwao thamani YA MTU Ni utu na thamani YA kitu Ni kutimizwa Kwa haja.
Mfano hawatofautishi Jackdaniel na gongo ili mradi myumbo.
Katambuga na jordani vyote viatu tu Kwao.

Nyumba YA tembe na ghorofa zote Ni nyumba na usingizi Ni uleule
 
Taarifa nyingi na maarifa mengi yasiyotumika yanausumisha ubongo na kuharibu namna tunavyofikiri ndo maana
Mazingira yanatushinda kuyatawala ukilinganisha na vizazi vilivyopita wakati ambapo MTU alipata taarifa na maarifa YA muhimu na YA lazima ili kumudu mazingira yake tu.
 
😀😀😀 ni kweli, jitahidini kutafuta vya kukufutahisha ili usipate hiyo sonona.

Unless you are a researcher, you don’t need much informations about something.
 
Hii ni kweli kabisa, kadri unavyotafuta maarifa ndivyo unazidi kuchanganyikiwa
 
Yaaniii,pia ubaya ni kua the more unajua vitu vingi the more unajikuta Kuna vingi hunifahamu kwahiyo ubongo unataka zaidi.
Mimi sipendi kujua mengi mfano kusima vitabu 10 vya kitu kimoja tu hilo suala lilinishinda. Nataka kuelewa basics tu halafu mengine nitajiongeza mwenyewe. Huwa naamini taarifa za vitabuni zipo outdated. Kuanzia mwandishi anapata wazo la kuandika kitabu, anakichapisha, anakiingiza sokoni inaweza kuchukua hata mwaka mzima, kipindi ambacho unakuta alichokiandika kinakua tayari kishapotwa na wakati. Kwahiyo napenda kujua basics tu yanayobaki nita-observe na kufanya analysis mimi mwenyewe kulingana na dunia inavyoenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…