Wimbo wa taifa; tuwafunze wanetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wimbo wa taifa; tuwafunze wanetu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Amoeba, Aug 3, 2010.

 1. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Mungu ibariki Afrika
  1.
  Mungu ibariki Africa
  Wabariki Viongozi wake
  Hekima Umoja na Amani
  Hizi ni ngao zetu
  Afrika na watu wake.
  Chorus:
  Ibariki Afrika
  Ibariki Afrika
  Tubariki watoto wa Afrika.
  2.
  Mungu ibariki Tanzania
  Dumisha uhuru na Umoja
  Wake kwa Waume na Watoto
  Mungu Ibariki,
  Tanzania na watu wake.
  Chorus:
  Ibariki Tanzania
  Ibariki Tanzania
  Tubariki watoto wa Tanzania.


  Asilimia tisini ya maneno yaliyopo katika wimbo wetu wa TAIFA ni Mungu ibariki!!!!!!!!!!
  Mimi nadhani kwa wimbo huu ndy maaana tumwkuwa kwa kudra za mwenyezi mungu, destiny yetu tumeikabidhi mno kwa Mungu!!! hakuna sehemu sisi tunashiriki katika lolote, hakuna mlengo wowote wa kuwapa mshawasha vijana wetu! Wimbo wa Taifa ni Nembo muhimu na mhuri wa moto wa kuonesha nini malengo na kila mtu afanye nini ili kufikia malengo! Mimi naona wimbo huu unahitaji review mapema iwezekanavyo!
   
 2. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Si afadhali na huo mie ule wa Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote ndio unanichefua na sidhani kama nitawafundisha wanangu waujue hasa kile kipengele NILALAPO NAKUOTA WEWE NIAMKAPO NI HERI MAMA WEEEEEEEEEEE !!! Kha! jamani sijui nisemeje lol!
   
 3. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tusisingizie wimbo wataifa. these are just words, have nothing to do with development.
   
 4. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2010
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hii inaweza ikawastua wengi, lakini ukweli ni kuwa watu wengi sana hawayajui maneno ya wimbo wa taifa, hasa watoto wetu waliosoma baada ya trade liberalization, ambapo mambo ya chipukizi, halaiki na hata JKT ilisimama kwa muda. Kosa la kawaida ni kuchanganya maneno ya ubeti wa pili na wa kwanza. Sitashangaa kabisa kama vijana wa miaka ishirini mpaka ishirini na tano hivi hawajui maneno ya wimbo huu.

  Natafuta nafasi nizipate nyimbo zote patriotic tusipoangalia tutazipoteza. Natafuta kuwasha mwenge, tazama ramani, na Tanzania tanzania nakupenda kwa moyo wote. Yes Nilalapo naiota Tanzania ( whats wrong with that?) Nafikiria tulikotoka tulipo sasa hivi na tuendako. Niamkapo ni heri kwa sababu mambo yalivyo sasa ndoto nyingi ni nightmare.
  Nadhani saa nyingi maneno yanatuumiza kwa sababu tunayatafsiri kutokana na uelewa wetu wa mambo.

  Mungu Ibariki Tanzania. I will love Tanzania forever despite being discouraged by mafisadi.
   
 5. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Huwa naona aibu kuimba wimbo wa taifa. Kwa sababu ni copy ya wimbo wa taifa wa Afrika kusini. Wimbo wetu wa taifa unatakiwa kuwa "Tazama ramani". Huwa naona aibu watu wanaposema huu ni wimbo wa ANC, so sad hatuwezi hata kuwa na wimbo wetu wa taifa, tunaiga tu.
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Huo nao walitunga wachina 1966
   
 7. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2010
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na wewe Tazama ramani ni wimbo mzuri sana baadhi ya beti zake huwa zinanichoma sana. Kutokana na wimbo huu huwa ninaiita Tanzania chem chem ya furaha,{ like in Chem chem ya furaha ama nipe tumaini.} I have similar reservations to the current national anthem. I heard that either Zimbabwe or Zambia changed its anthem ( I know I can very easily check this.)
   
 8. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Unataka kusema wimbo wa taifa hauna maana? Lengo wala si kuzingizia wimbo wa taifa, lengo ni kuwa tayari tunao wimbo lakini wimbo huo sioni unawafundisha nini wanetu! sioni unawahimiza nini katika kulenga maendeleo. Kama ulishawahi kuwa karibu na watu wanaofanya kazi ngumu (wakulima, wafungwa, makuli) utakubaliana na mimi kuwa wimbo unatia hamasa watu kufanya kazi kwa Moyo, Mtu unaweza kuwa na "Knowledge" na Skills, lakini usipokuwa na Attitude towards kazi, hautafika mbali,au unaweza hata kusahau mlengo wako.
   
Loading...