Wimbo wa kizalendo "Tanzania nakupenda" umefanyiwa editing?

PRINCEd

JF-Expert Member
Dec 14, 2015
850
586
Habari za wakati wanajamvi.....

Leo katika pita pita zangu nikapita karibu na shule moja ya msingi hapa Tanzania, nikasikia wanafunzi wakiimba huu wimbo wa Kizalendo.... "TANZANIA NAKUPENDA."

Katika kujikumbusha maisha yangu ya shule nikajikuta naenda nao beti kwa beti, kilichonishangaza ni kuona huu wimbo wanaoimba sasa na tulioimba zaman kuna utofauti mkubwa!!!!

Kuna vitu vimeongezwa mfano msitari unaozungunzia " siasa yako nzuri na desturi vilituletea uhuru" wakati ile mingine unayozungumzia walowezi imenyofolewa...

Kingine huu wimbo naona kama umekuwa mfupi sana ukilinganisha na ule wa Zamani..

Swali langu...

Je, huu wimbo waliufanyia uhariri "editing" na kama waliufanyia ilikuwa lini na malengo yalikuwa yapi???

Naomba Kuwasilisha.....
 
Kwa bahati nzuri Mimi nimeziimba zote mbili kuanzia shule ya msingi nimeimba ule wa mwanzo lakini ulikuja kubadilishwa 2014 nikiwa form five hata sisi tulimuuliza mwalim akasema umebadilishwa.wimbo kweli umefupishwa ule wa mwa mwanzo ulikuwa na stanza nne wa sasa unazo tatu ila stanza ya kwanza na ya Pili ndo zilezile ila ya tatu na ya nne zimeondolewa ikaundwa mpya.sababu za kubadili sijui sana ila nadhani lengo ni kuufanya uendane na mazingira ya sasa kwa sababu kuna mambo kama ya walowezi sijui nowadays hsyapo tena
 
Hebu uweke wa sasa tuusikilize mkuu ama tuusome
 
original version ilikua na maneno makali yakionyesha misimamo yetu hasa uzalendo,ujamaa,walowezi na ubeberu wamebadili baadhi ya maneno na pia hata mapigo yake nahisi waimbaji tofauti tofauti wamebadili yale mapigo ili kukidhi mahitaji yao
 
Nani alikaa akaamua kuubadili tu bila wananchi kupiga kura
 
Kuna wakati nilikaa nakufikiri huu wimbo wa Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote ndio wangeugeuza uwe wimbo wa Taifa kwa kufanya editing kidogo na kuongeza maneno kama Mungu na Afrika.

Ni wimbo mtamu sana na haukeli kuimba, tofauti na huu wa taifa aiseee.
 
Mi nauimba sana na upo moyoni kiukweli haujabadilishwa ila katika kuuimba mnaweza mkawa mnachagua muimbe wote au msimalizie beti zote. Kwa ufafanuzi pale maktaba ya taifa utaelezwa na waheshimiwa waliopo pale
 
Hebu uweke wa sasa tuusikilize mkuu ama tuusome
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote
Nchi yangu Tanzania
Jina lako ni tamu sana
Nilalapo nakuota wewe
Niamkapo ni heri mama wee
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote

Tanzania Tanzania
Ninapokwenda safarini
Kutazama maajabu Biashara nayo makazi
Sitaweza kusahau mimi mambo mema ya kwetu kabisa
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote

Tanzani Tanzania
Watu wako ni wema sana
Nchi nyingi za kuota nuru yako hakuna tena
Na wageni wa kukimbilia ngome yako imara kweli wee
Tanzania Tanzania
Heri yako kwa mataifa

Tanzania Tanzania
Karibu wasio na kwao
Wenye shida na taabu
Hukimbizwa na walo wezi
Tanzania yawakaribisha
Tuungane kiume chema wee
Tanzania Tanzania
Mola awe na we daima.
 
Hiiii ndo Old Version......
 
WIMBO WA UZALENDO

Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote,

Nchi yangu Tanzania, Jina lako ni tamu sana,

Nilalapo nakuota wewe, Niamkapo ni heri mama wee,

Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote.

Tanzania, Tanzania, Ninapokwenda safarini,

Kutazama maajabu, Biashara nayo makazi,

Sitaweza kusahau mimi, mambo mema ya kwetu kabisa,

Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote.

Tanzania, Tanzania, Watu wengi wanakusifu,

Siasa yako na desturi, Ilikuletea uhuru,

Hatuwezi kusahau sisi, Mambo mema ya kwetu hakika,

Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote

Hiii hapa New Version
 
Sasa mijadala inakaribishwaaaaa

Back
Top Bottom