Wimbo mpya wa diamond

Wimbo mpya wa diamond

kidunula1

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2016
Posts
6,305
Reaction score
6,351
Salamu kwenu wapenda maendeleo!

Nataka tushirikiane kimawazo wadau, Hivi huu wimbo umeleak ukiwa haujakamilika au ndiyo tayari umekamilika hapo? Kwa maoni yangu naona bado una dosari kubwa,na unatuangusha sisi tuliokuwa tuna matarajio makubwa sana na huu wimbo. Mimi binafsi mara ya kwanza nilipousikia walipouimba huku Mwanza kwenye Jembeka Festival nilifurahi sana na nikawaambia wadau kwamba huu wimbo hakika utapenya hadi chati za billboard. Ila nikiusikiliza huu unaosemekana umeleak naona una dosari kubwa zitazofanya huu wimbo ufikie kwenye kiwango ulikostahili. Naamini Mixing hajakamilika cz sauti bado ni kama hazijawa balanced vema,wimbo unakatwakatwa hovyo ktk kuunga kipande kimoja na kingine, kutoka kwenye verse kuingia kwenye korasi hakuna uelewano. Naombea iwe umeleak kweli ukiwa hajakamilika,ila kama ndio tayari basi Diamond umeniangusha sana japo nitaupenda hivyohivyo cz ni collabo nzuri sn! Sijui wadau wenzangu mnaonaje!!
 
Wametengeneza kiki tu ili tuwe makini kusubiri hiyo iliyokamilika.
 
Wametengeneza kiki tu ili tuwe makini kusubiri hiyo iliyokamilika.
Asee maneno yako yakitimia nitafurahi sana. Huu wimbo ni mkali bwana wasiufanyie sport sport! Lakini pamoja na hiyo, haoni kama watu tutakuwa tumeshausikiliza vya kutosha huu huu ulio na upungufu na kufanya huo uliokamili kukosa vibe ya kutosha! Manake naamini instrumental ni hii hii, mashairi ni hayahaya na melodi ni hizihizi!
 
Ubora
 
Back
Top Bottom