Wilson Mukama :UNAKUMBUKA haya??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wilson Mukama :UNAKUMBUKA haya???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngoshwe, Dec 11, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,073
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  HAYA YAMECHAPISHWA KATIKA TOVUTI YA CCM, NI SEHEMU YA KAULI YA BW. WILSON MKAMA AMBAYO HADI SASA UTEKELEZAJI WAKE UMEKUWA NI KIGUGUMIZI NDANI YA CCM!!!


  Mafisadi CCM lazima wavue gamba  Kutoka Gazeti la Habarileo

  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, amesema yeye ni sawa na mtu aliyeteuliwa kufanya kazi ya kunyonga mkosaji aliyehukumiwa adhabu hiyo na Mahakama, hivyo hawezi kuogopa kutekeleza hukumu hiyo.

  Akifafanua kauli hiyo jana mjini Morogro, Mukama alisema uamuzi wa ngazi za juu wa CCM ukishatolewa kuhusu kuvua gamba watuhumiwa wa ufisadi, hakuna kiongozi atakayepuuza kuutekeleza.

  "Ufisadi unasemwa dhahiri na wananchi kwa kuwataja watuhumiwa hadharani wakiwahusisha ana EPA (Akaunti ya Malipo ya Nje ya Benki Kuu), Dowans, ununuzi wa rada na Richmond … na vikao vya chama vimetoa uamuzi.

  "Kilichobaki ni utekelezaji tu…na hukumu ikishatolewa na Mahakama hakuna njia nyingine isipokuwa kutekeleza agizo hilo," alisema Katibu Mkuu huyo alipokuwa akizungumzia madai, kwamba anaogopa kutoa barua za kujivua gamba kwa watuhumiwa wa ufisadi.

  Akihutubia mahafali ya wanafunzi wanachama wa CCM wanaomaliza Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro, Mukama alisema hataogopa kusimamia kikamilifu uamuzi wa chama hicho wa kuwatosa watuhumiwa hao.

  Alisema vitendo vyao vimesababisha CCM na Serikali ichafuke mbele ya Watanzania.

  Mbali na kuwavua gamba, Mukama alisema CCM pia itashughulikia suala la wafanyabiashara wasio waadilifu wanaojipenyeza ndani ya chama hicho, na itapambana na saratani ya kujilimbikizia madaraka na kukiondoa chama hicho katika utegemezi wa matajiri na wahisani wanaokiweka pabaya.

  Alisema, hakuna mwananchi asiyejua kuwa ndani ya CCM wapo viongozi wenye nyadhifa kubwa wanaotuhumiwa kwa ufisadi kuanzia wa EPA, Richmond, Dowans, Rada na kashfa nyingine.

  Katibu Mkuu huyo alisisitiza kwamba ili kukisafisha chama hicho mbele ya jamii na kukifanya kikubalike katika uchaguzi wowote, ni lazima watuhumiwa hao watoswe ili kurudisha imani kwa Watanzania.

  Mukama alionesha katuni aliyodai imemchora hivi karibuni, akiwa na barua mkononi ikionesha kuwa ameshindwa kutoa uamuzi na kusisitiza kuwa uamuzi huo ni wa chama, hivyo utatekelezwa kama ilivyopangwa.

  Awali katika risala ya wanafunzi hao, walitaka viongozi wote wa CCM kujikita kuwaletea maendeleo wananchi, ili baadaye wapimwe kwa kazi zao.

  Wanachama hao waliwataka viongozi wahubiri amani badala ya kuendeleza malumbano na vyama vya upinzani na kuwataka watumishi wa Serikali kuachana na siasa wakati wakiwa watumishi wa umma.  Imetayarishwa...

  11:28:00 28.06.2011
  Website Rasmi ya Chama Cha Mapinduzi - CCM
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,292
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Mkuu atakumbuka wapi wakati tayari ashalambishwa? Mkapa alipoingia aliahidi katika hotuba yake ya kwanza bungeni kuwa atawashughulikia wala rushwa,matokeo yake ndo akawakumbatia haswa.JK aliahidi kurejesha nyumba za serikali lakini muulize sasa kama anakumbuka?
   
 3. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,328
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 160
  Kumbukumbu huwa zinawatoka pale wanapoanza kutumia masaburi! huwa wanazikataa hata kauli walizozitoa wenyewe!
  Period!
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,014
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Hata kama akiyakumbuka, hivi ana uchaguzi wa kufanya anachokitaka kukifanya? CCM imeshashikwa pabaya, na kama atajifanya kijogoo na kufanya hayo, basi atakuwa anahatarisha na nafasi yake. Yupo tayari kufanya hivyo?
   
 5. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #5
  Dec 11, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,596
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  ukiwa ccm ni kama mchawi unaweza loga hata majirani na watoto wako
   
 6. MD24

  MD24 JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 747
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Tumechoka na hizi habari za MAGAMBA. Now, lets talk other business!
   
 7. babad

  babad Member

  #7
  Dec 11, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawana lolote la maana zaidi ya uhuni wa kisiasa tu
   
 8. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #8
  Dec 11, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,640
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  si nafasi tu,hata maisha yake!
   
 9. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #9
  Dec 11, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,073
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkama Ukatibu Mkuu ni kama walimpachika..ilie nafasi ilifaa mtu wa staili ya porojo kama Makamba..mdanganyifu na asiejali kudharaulika..kwa Mkama itampotezea heshima...
   
 10. w

  watundawangu JF-Expert Member

  #10
  Dec 12, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 250
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Ebu aondoe ujinga wake hapa, tumechoka na upuuzi huu. haya ni maneno matupu yasiyoweza kuwasitua usingizini mafisadi. Hivi tangia muanze hii falsafa ya kuvua magamba ni wangapi mmeshawaondoa? Mafisadi wote bado wapo. R. A. alijiondokea mwenyewe, laiti angekuwa na moyo wa Farao angebaki mbunge wa Igunga hadi leo hii. Akina Luhanjo pamoja na madudu yote walioufanya ya kumtetea mhuni Jairo bado wanapeta, japo wapo ndani ya ofisi moja na mwenyekiti wa CCM.. aibu!Mi nasema kama mpo bado vijana wa kitanzania hasa nyie wasomi, tena nyie mnaomaliza vyuoni, mnaotegemea CCM, mkapimwe akili. Hivi ni lini mtatambua kuwa mnadanganywa?Poleni sana wasomi wetu.. heri ya sisi tusioenda shule ambao sasa tunaweza kupambanua uwongo wa CCM kuliko nyie mnaoendelea kuwaalika na kuwasikiliza na kuwasomea risala.. poleni sana.
   
 11. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #11
  Dec 12, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,490
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  anayakumbuka ila anyapotezea aaah no hayajui kwani risala anaandaliwa
   
Loading...