Wilaya za Mwanga na Same zimekamilika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wilaya za Mwanga na Same zimekamilika?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by babalao 2, Apr 14, 2012.

 1. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,218
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Wanaukombozi hapa pamekaaje maana katika wilaya hizi mkoani kilimanjaro zimekua ni ngome ya ccm kwa miaka mingi na bado ni masikini, je nini kifanyike kuwakomboa watu hawa wakae mkao wa kimabadiliko?
   
 2. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Nimepata kutembelea hizo wilaya mara kadhaa.Ni kweli ni miongoni mwa wilaya maskini kabisa hapa nchini..kuna matatizo ya maji hasa maeneo ya tambarare,na bado hizi bado ni ngome imara za CCM.Wengi wa wananchi wake wanajivunia wilaya hizo kuwahi kutoa viongozi wakuu wa kitaifa kama vile David Msuya,Peter Kisumo,Dkt Asha Rose Migiro ,Nicodemus Banduka na wengine wengi.Wanajisikia fahari sana kuwa na watu hawa,wanaona namna bora ya 'kuwaenzi' watu hawa ni kuendelea kuiunga mkono CCM.Ndugu zetu hawa wanahitaji kuhamasishwa ili wajitambue,wabadilike na waachane na CCM.Jirani zao Rombo na Vunjo wamethubutu kwa nini isiwe wao?
  Kwa sababu ya umaskini wa maeneo haya,kiwango cha uhamaji 'emmigration' kipo juu na kiwango cha uhamiaji 'immigration' kipo chini.
  Vile vile,maeneo mengi ya vijijini yana huduma za jamii kama vile maji na barabara na moja ya matokeo ya hali hii ni kuwa na kiwango kidogo cha umijinishaji 'urbanization' ambayo ni determinants katika mabadiliko ya kifakra,mitazamo na hulka kutokana na muingiliano wa wanajamii.
   
 3. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,569
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Labda uende na bakola huko, Mmmmh! ni wabishi na waelewaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Bakola sawa la si hivyo thithi ni wa thithiemu na wakubwa ni thithi na wadogo ni thithi!
   
 4. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe 100%. Wilaya hizo zina uwezo mkubwa sana wa maendeleo bali watu wake wamekosa msukumo wa kisiasa. Kuna haja ya kuanza harakati za kukomboa wilaya hizo hasa kwa kuanzia wale wenyeji wake waliomo humu jamvini ambao wana mwamko wa kuleta mabadiliko.
   
 5. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2012
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Wanaamini siku moja Msuya ataupata tena Uwaziri Mkuu

  Mkuu uliyoyanena ni kweli kabisa, hizi wilayani maskini na wakaazi wa hizo wilaya ni wavivu kupita maelezo
  kuna sehemu kubwa kulikuwa na mashamba ya katani wakati wenzao wa nashinikiza hayo maeneo yarudishwe kwa mafukara wananchi wao walihamua kumzawahia Mbunge wa Singida mjini.

  siku hawa jamaa watakapo amka itakuwa too late for them
   
 6. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kwa mfano tu, tatizo la maji limekuwa sugu kwa muda mrefu sana. Mimi nilisoma Same Secondary miaka ya mwanzo ya 70 na hapo ndio tatizo lilipoanza. Mpaka leo hapajapatiwa ufumbuzi wowote licha ya kuwa na maji mengi ardhini. Kule upande wa Stirling kuna visima vya maji, ila vimezibwa kwa ukosefu wa pump! Pale karibu na hospitali kuna bwawa linahifadhi maji kutoka mlima Vumari ambalo linahitaji kuboreshwa. Mbunge wa Same uko wapi? Wananchi mko wapi? Mbona mnawachagua hao hao kila mwaka???
   
 7. M

  MELODY Member

  #7
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inawezekana wakakombolewa kwani hata Igunga ilikuwa ngome ya Magamba lakini kama si uchakachuaji ilikuwa tuokomboe kwenye uchaguzi mdogo. Mie si mgeni wa maeneo hayo kinachotakiwa CDM wapitishe jina la mtu anayekubalika na watu na wawe na mpango wa muda mrefu wa kufungua matawi na kuimarisha chama maeneo husika. Kwa mwendo huo ukombozi utafanikiwa.
   
 8. b

  bansenbana Member

  #8
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wapare wana msimamo na sio flip floppers kama wachaga. Enzi za RUWA wa wachaga, Mrema na NCCR wote walichagua wabunge wa NCCR kwa kuamini kuwa huyu Mangi angekuwa rais na mambo yao kuwanyookea. Lakini ilivyokula kwa Mangi wakaanza kurudisha majimbo CCM moja baada ya jingine, mpaka likabaki moja tu la Moshi Mjini (NDESA). Walivyoona juzi kuwa akina Mbowe na CDM wanaweza kuingia madarakani wakatimkia CDM. Ila safari hii wakawa smart. Usmart unakuja hivi, yale majimbo yote yenye Mawaziri mfano Moshi vijijini (Cyril Chami) na Siha (Aggrey Mwanri) wakayaacha yabaki ccm ili ikitokea CDM isiposhinda wasije wakakosa bara na pwani kama ilivyotokea mwaka 1995 to 2000. Rombo baada ya kuona Mramba hawezi tena kupewa hata Ukuu wa wilaya wakampiga chini. Hao ndio unaowaita wanamageuzi, ni wana maslahi
   
 9. A

  Akilimali2001 Member

  #9
  Aug 20, 2012
  Joined: May 11, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shika adabu na ukae kimya! Wachaga hawataki mutu goigoi asiyeleweka. Nani kakwambia wachaga wako tayari kukumbatia wezi? Au vibaraka wa CCM?
   
 10. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,068
  Likes Received: 4,000
  Trophy Points: 280
  get ur facts right Rombo, Karatu na Kigoma mjini ni vitovu vya mabadiliko tangu 1992-1995 na si kwamba eti wamethubutu! ila wana uzoefu na siasa! unajua historia ya mageuzi ya CHADEMA nchini hapa au unaropoka tu!? huwezi kufananisha majimbo hayo na Same au Mwanga
   
 11. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  hahahahaaaaaaa thithiemu imetudhaa bana tukiichagua chadema nchi itaingia vitani,
   
 12. b

  bangusule Senior Member

  #12
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 185
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  siyo kweli kwamba Same na Mwanga hawana uelewa au hawataki mabadiliko. jambo la kwanza, wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakibadilisha wabunge wao mara kwa mara. jambo la pili, vyama vya upinzani havijawahi kufanya uhamasishaji wa maana katika maeneo hayo sasa wananchi wasipochagua upinzani siyo kitu cha ajabu. tatu, kwa muda mrefu ccm imekuwa ikipeleka wagombea ambao wanaonekana kuwa ni bora kuliko wale wa upinzani.

  labda nitoe mfano wa jimbo moja la same mashariki. wana ccm walimkataa waziri Daniel Yona na kuwapa kura wanawake wawili, Anna Kilango na Naghenjwa Kaboyoka. baadaye Kaboyoka alihamia Chadema kwa hivyo ktk uchaguzi mkuu jimbo lilipiganiwa na wagombea wanawake. nitajieni ni jimbo gani ktk Tanzania yetu wanaweza kutoa nafasi kwa wanawake kama walivyofanya wananchi wa same mashariki?? kabla ya hapo same magharibi ilikuwa inawakilishwa na gladness mziray. mnaotulinganisha na rombo, mmesahau kwamba watani wetu walingangana na basil mramba hata wakati wanajua ana kesi ya ufisadi mahakamani.

  ushauri wangu kwa vyama vya upinzani wafanye kazi ya uenezi na pia wapeleke wagombea wenye elimu na wanaochagulika. mkipeleka wagombea wasioaminika kama anna senkoro basi wananchi wa same hawatakuwa na jinsi bali kuchagua ccm.
   
 13. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Mwanga wamekuwa na minong`ono kuwa prof anawatukana sana na kuwaambia kuwa hawajasoma ila wanampa kura.Watu na lugha zao bwana.Na walianza lalama longo time kabla jamaa hajaingia ipi hiki.
   
Loading...