masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,173
- 13,776
Kwa kweli Wilaya ya Rungwe kutengewa shs 920mil kwa barabara ni utani mbaya!
Tshs 920mil ni sawa na kujenga kilometa MOJA ya barabara ya lami.
Na kwa wilaya hii tayoifahamu ina milima na miinuko mingi, fedha hizi zaweza kujenga nusu kilometa tu.
Naibu waziri Suleiman Jafo ametamka bungeni kuwa kwa mwaka 2016/2017 fedha hiyo ndiyo iliyotengwa kwa wilaya hii.
Jafo alikuwa akimjibu mbunge wa viti maalum kupitia chadema, Sophia Mwakagenda.
Jafo aliendekea kusema mwaka 2015/16 zilipelekwa tshs 157.9 mil!
(Nipashe pg 10)
Barabara iliyokuwa inajengwa toka Mnara wa mzunguko kuelekea Masoko imekoma bila kuendelea miaka sasa.
TANROADS ni kama wameagizwa kutoigusa wilaya hii, licha ya ahadi lukuki wakati wa kampeni.
Barabara ya mzunguko Katumba~Mwakaleli~Busokelo~Mbambo~Masoko~Tukuyu yenye urefu wa takriban kilometa 100, imekuwa wimbo unaoimbwa tu wakati wa kampeni toka wakati wa Mkapa hadi hivi sasa.
Wananchi wa sehemu hiyo tunaanza kuvunjika moyo, wakati tunajua kuwa kuna sehemu za Mwanza kwa mfano, fedha zina fukuzia ziwekezwe wapi kwa mabilioni.
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.