Wilaya ya Pangani yawavutia wanachuo

Wilaya ya Pangani yawavutia wanachuo

MASIGA

Senior Member
Joined
Aug 29, 2015
Posts
130
Reaction score
282
Mapema leo wilaya ya Pangani tumeupokea ugeni wa asasi ya vijana toka vyuo vikuu wakiwakilishwa na wenzao toka chuo cha UDSM na Ustawi wa Jamii wakiwa na malengo ya kuja kujifunza na zaidi kufanya kazi yao ya uhamasishaji na sehemu ya miradi yao wilayani hapa baada ya kuvutiwa na kasi ya utendaji kazi ya Pangani nao kutoa mchango wao kuunga mkonokwa sehemu yao juhudi hizi za maendeleo ya wananchi.

Zaidi wamepokelewa leo na Katika Tawala wa Wilaya ya Pangani Mwl.Nyange na kukutana na Mkurugenzi wa Wilaya Bwana Daud Mlahagwa na baadae kukabidhiwa kwa Kiongozi kijana mwenyeji wa eneo watalokua Katibu Tarafa Pangani mjini Bi Zuhura Rashid.

Asasi hii kwa jina la BINTI MAKINI inaundwa na mabinti wa Vyuo na Vyuo Vikuu Chini ya Mwenyekiti Janet John na Katibu Salma Mohammed toka UDSM.

Ambapo tumewapokea vijana hawa na watakaa kwa siku sita kuanzia tarehe 4 mpaka tarehe 10.Oct. wakiwa Lengo lao ni kupita mashuleni kutoa elimu kwa wanafunzi hasa wakike kuwahamasisha kusoma kwa bidii, kuhusu afya ya uzazi,kujitambua, magonjwa, uzalendo, umuhimu wa elimu na maadili.

Ni faraja kwetu kua Wameichagua Pangani ili kuweza kuwapa wanafunzi wetu wa shule za msingi na sekondari ari,morari na hamasa juu ya kupenda elimu na kuipenda nchi yao,wameamua kutumia elimu yao kwa manufaa ya jamii ya watanzania na tunaamini kwa umri wao mdogo wataelewana kwa urahisi na wenzao na zaidi ni rahisi wanafunzi wetu kuwaelewewa vijana wenzao toka nje ya Pangani zaidi ya kua wakiwaskia wazawa ama watu wa hapa pekee.

Kama ofisi ya mkuu wa Wilaya pamoja na udogo wa ugeni huu ila kwa thamani na kuvutiwa kwao na Wilaya yetu tutawasaidia kila kitu kwa muda wote watakapokua hapa kwa maana ya malazi,chakula na usafiri zaidi kwa kushirikiana na ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Pangani.

#PanganiKumenoga.
IMG-20181005-WA0062.jpeg
IMG-20181005-WA0061.jpeg
 
Pangani imewavutia wana chuo baada ya kufika huko au imewavutia kutokana na uhitaji juu ya suala la binti kutotilia mkazo masomo na kuwafanya waje huko kuhamasisha?
 
Back
Top Bottom