Wilaya ya Misungwi inadhulumu ardhi za wananchi

Entim

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
4,021
2,253
Mhe. William Lukuvi, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, "ARDHI YA WANYONGE IMEPORWA NA TUNALAZIMIKA KULIPIA UPIMAJI SHIRIKISHI"

Mhe. Kwanza tunakupongeza kwa kwa juhudi zako za kuhakikisha zoezi la upimaji shirikishi linaendeshwa kwa gharama nafuu na sisi wananchi wa Misungwi DC tumeitikia wito, tumekubali maeneo yetu yapimwe na tumeuza mifugo na mazao na tumenza kulipia kwa mujibu wa sheria.

Mhe. Lukuvi; kwa niaba wa wananchi wa Misungwi, leo ninaomba kuleta malalamiko ya wakazi, haswa wazawa wa maeneo ya Idetemya, Fela, Ngudama, Bukumbi, Ng'ombe nk.

Mhe. Waziri wa Ardhi; Miaka ya nyuma tuliwalalamikia ufisadi unaofanywa na akina Magesa na Nyasebwa (watumishi wa Idara ya ardhi Misungwi DC), na mmoja alinusurika kuuwawa kwa kupora ardhi

Mhe. Lukuvi; Miaka ya nyuma, idara ya ardhi ya Misungwi DC wakiongozwa na mafisadi hawa niliowataja
walipita kwenye maeneo yetu na kuyapima kimya kimya bila kushirikishwa, mchoro ukaenda hadi Wizarani na kupitishwa.

Mhe. Waziri; Mwaka huu wa 2019 tena baada ya agizo lako kuwa watu wapimiwe maeneo, upimaji shirikishi ukapita tena kwa kufuata taratibu zote, tukaitikia wito, viwanja tumeanza kulipia ili tupewe hati miliki. Cha ajabu ni kwamba tunambiwa kuwa baadhi ya maeneo haya yameshapimwa siku nyingi, na baadhi ni MOSOKO YA UMMA, MAJALALA, MAKABURI, OPEN SPACE, NK BILA FIDIA, na bado tumelipia hewa. Maana yake ardhi ilipimwa bila ridhaa yetu, mafisadi wakauza na kutuachia open space?

HITIMISHO; Hakika hili litamfikia Rais Magufuli mapema wiki ijayo atakapofika Mwanza tarehe 9 Disemba 2019.

NAOMBA KUWASILISHA, TUSAIDIWE SISI WANYONGE!
 
Huyu mnyama Nyasebwa ni shida... sio mwanadamu bali mnyama wa porini tena mbwa mwitu anasumbua sana watu pasipo kujali umri wao... kauza viwanja vya watu kwa dhuruma kanunua kiraum cha blue bahari... chuo alichosoma huyu mnyama wanatakiwa wamvue hilo gamba

Tena bora kaondoka yule ndongo walikua ni shida utatu wa dhuluma ( Ndongo, Nyoka na Nyasebwa) wezi wakubwa hawa
 
Asante sana ndugu yangu Msukuma_De_Great. Tupaze sauti kwani serikali ya awamu ya 5 kuna viongozi wazuri kama Waziri na Mhe. Rais anaweza kutusaidia

Mhe. Rais anakuja na nitaomba kikosi cha ulinzi wa Rais waniruhusu niongelee hili. Nitawandaa wananzengo walioathirika na hii tabia chafu.
Asante sana ndugu yangu Msukuma_De_Great. Tupaze sauti kwani serikali ya awamu ya 5 kuna viongozi wazuri kama Waziri na Mhe. Rais anaweza kutusaidia
 
Back
Top Bottom