Wilaya ya Kibondo ujambazi umekithiri

Wilaya ya Kibondo ujambazi umekithiri

Ni uzembe tu Mkuu, Kama ni kibaoni hapo NDUTA kambini si kuna police wakutosha aise, gari na mafuta wanapewa na UN bure ,
Uko sahihi kabisa mkuu,yaani hapo kila wakati ujambazi unafanyika maeneo hayo. Kwakweli hatuna majibu sisi wananchi. Yaani sasa tunasafiri roho juu na kulala tongo macho maana wakati wowote hao na SMG mikononi!!
 
Kwanini na nyie msiwalaze tu maana tunasikia huko SMG unabadili na gunia la mahindi

Jipangeni na nyie kama hamsaidiwi
Mkuu huo ni utani usiombe kukutwa na hilo janga,kiukweli usiombe uishi kwenye maeneo kama haya. Tunamaanisha kweli mkuu sio utani,hatuna amani katika nchi yetu yaani ni kama tuko Burundi tu!
 
Uko sahihi kabisa mkuu,yaani hapo kila wakati ujambazi unafanyika maeneo hayo. Kwakweli hatuna majibu sisi wananchi. Yaani sasa tunasafiri roho juu na kulala tongo macho maana wakati wowote hao na SMG mikononi!!


Poleni sana mkuu maisha ya huko ni kiumeni sana,
Usafiri wa kibondo,kasulu na kakonko
Vumbi+tope +Ujambazi = kazi mnayo.

Kama upo kibondo mjini wape salamu zangu Pabro wa Africa sana bar na Shekh kinyeo station 1
 
Mkuu huo ni utani usiombe kukutwa na hilo janga,kiukweli usiombe uishi kwenye maeneo kama haya. Tunamaanisha kweli mkuu sio utani,hatuna amani katika nchi yetu yaani ni kama tuko Burundi tu!
Kwani wao wanapata wapi hizo silaha za kila siku kushambulia watu?
Halafu Rais alipeleka wakuu wajeda sehemu hizo na akasema walazeni tu

Natumaini kilio chenu kitasikika wapo wengi humu wanachungulia
 
Nikiwa kama mkazi kutoka Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma kwakweli tunateseka mnooo na suala la ujambazi hasa wa utekaji magari barabarani na uvamizi majumbani.

Hivi viongozi wetu mnalifahamu hili au ndio kwa vile wenzetu mkija huku mna ulinzi wa kutosha hivyo hamjui uchungu wake!?

Kiukweli kwa sasa huwezi kusafiri kwa amani katika barabara kuu hasa katika maeneo yaliyo karibu na kambi za wakimbizi,kukuta magogo barabarani au watu kujitokeza na silaha na kuwateka ni jambo la kawaida. Hivi tuko Tanzania kweli au tumehamishwa hatujijui.

Hilo tamko la Waziri la kutaka Jeshi la Polisi kukomesha ujambazi kwa muda wa wiki 2 ni kituko hicho Mh. Waziri. Hili jambo linahitaji mkakati wa ziada jamani tunatesekaaaaaa!Asilimia zaidi ya 80 ya wahusika wanaotufanyia vitendo hivyo ni wakimbizi kutoka katika makambi ya wakimbizi na wengine kutoka Burundi moja kwa moja angalieni namna ya kufanya jamani tunaangamia.

Pindua hizo takwimu zako; %80 ni waTz
 
Poleni sana sana, nilisha kutana na balaa lao hao warundi ktk ya Kabale na gwarama, walipitia mtaji wangu wotee

Tukiendelea kusema kuwa ni warundi hatutapata suluhu, mimi niliponea chupuchupu kati ya nzega na kahama, wengine walitekwa sekenke
 
Ila waha si wanajisifu kwa uchawi umekuwaje wameshindwa zuia ujambazi kwa tunguli
 
Pindua hizo takwimu zako; %80 ni waTz
Ndugu yangu hiyo takwimu yangu ni sahihi,ni kweli waTz wanatumika pia lakini kuna vikundi kadhaa vinafanya matukio wote ni warundi maana wananchi wengi wanaokutana nao na kufanyiwa ukatili huo wanakiri kuwa ni warundi amini ninachokwambia. Taarifa za uwepo wa waTz wanaoshiriki matukio hayo zipo pia.
 
Pindua hizo takwimu zako; %80 ni waTz
Mfano kuna kikundi cha wakimbizi wasiopungua 6 hadi 8 wanaoonekana maeneo tofauti na SMG kati ya 4 mpaka 5 ambapo wengi wa wananchi wanaotekwa na kikundi hicho wanakiri kuwa ni warundi. Kikundi hicho kinazunguka sana vijijini lakini hapo KIBAONI ndio kinaliza watu kila wakati.
 
Tukiendelea kusema kuwa ni warundi hatutapata suluhu, mimi niliponea chupuchupu kati ya nzega na kahama, wengine walitekwa sekenke
Mkuu Gama huko matukio hayatokei kama huku tulipo,huku kumezidi kwa sasa ni wakati wowote unapigwa tukio. Kwa sasa tumeanza hata kuacha android zetu na vitu vya thamani majumbani unapotoka eneo moja kwenda jingine maana ukienda navyo unakabidhi wakati wowote.
 
Ukichunguza sana huenda sio watanzania hao wanaiba nakuteka magari
 
Poleni sana mkuu maisha ya huko ni kiumeni sana,
Usafiri wa kibondo,kasulu na kakonko
Vumbi+tope +Ujambazi = kazi mnayo.

Kama upo kibondo mjini wape salamu zangu Pabro wa Africa sana bar na Shekh kinyeo station 1
Salam zimefika mkuu kwa hao wadau.
 
kweli kabisa. tokea masoko wakimbizi yafungwe na serikali, ujambazi umeanza upya. si Kakonko si kibondo hali ni tete
 
Hiyo wilaya naijua kwa sifa hiyo ya utekaji wa magari tuu ni hatari na wanakua na siraha nzito...
 
Serikali inatakiwa iweke kambi za FFU kila wilaya katika mikoa ya kanda ya ziwa, jambo dogo hili kama kila mwaka wanaajiriwa vijana karibia elfu kumi au zadi kwenye vyombo vya ulinzi na usalama
 
Mkuu Gama huko matukio hayatokei kama huku tulipo,huku kumezidi kwa sasa ni wakati wowote unapigwa tukio. Kwa sasa tumeanza hata kuacha android zetu na vitu vya thamani majumbani unapotoka eneo moja kwenda jingine maana ukienda navyo unakabidhi wakati wowote.

Aise kazi mnayo nimeongea na jamaa anapiga kazi nduta,,
Nasikia wanapigia pale pale kwenye geti la polisi mbona hatari sasa iyo,
Waziri katoka juzi juzi uko vipi mmemjulisha?
 
Back
Top Bottom