Wikileaks wadai Afrika inachunguzwa na CIA kwa kutumia vifaa kama simu za mkononi na runinga

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,398
Siku ya jumanne wiki hii, mtandao wa WikiLeaks ulitoa taarifa za siri zipatazo 8761 ambazo zinaeleza kuhusu shughuli za ujasusi zinazofanywa na shirika la ujasusi la Marekani la CIA kwa kutumia vifaa vya umeme kama simu na runinga za majumbani.

Taarifa hizi ambazo zimebatizwa jina la "Vault 7" zimepatkana baada ya kuwa zinasambazwa na baadhi ya waajiriwa wa zamani wa idara hiyo hasa wale wanaoingilia mitandao ya kompyuta yaani "hackers" na wahandisi.

Mabara ya Afrika, Mashariki ya Kati na Ulaya yametajwa kuwa ni walengwa wakuu wa mpango huu, bara la Ulaya hasa nchi 25 zilizoko kwenye eneo la Schengen zikiwa ndani ya wigo wa udukuzi.

Taarifa hizi zinaonyesha jinsi idara ya ujasusi ya CIA na mwelekeo wake katika kufanya shughuli zake hasa katika karne hii ya 21 ambapo kuna mapambano ya kimtandao baina ya mataifa makubwa na madogo yaani "cyber wars" ushindani wa silaha za kimtandao "cyber weapons" na mpango mzima wa udukuzi duniani au global covert hacking programme.

Vifaa vya simu kutoka katika majina makubwa kama Samsung, vifaa vya kampuni ya Apple vya iPhone na iPad, kampuni ya Microsoft, Linux na simu za mikononi zitumiazo mfumo wa Android zimetajwa kuwa vinahusika kufanya kazi ya udukuzi wa habari za kijasusi kwa kutumia vipaza sauti au "spekers" ambazo ainakuwa zikirekodi mazungumzo pale vifaa hivyo vinapokuwa vimejiunga na mtandao wa internet.

WikiLeaks wanadai kwamba mtoaji siri mwingine maalum "Whistleblower" ambae anafanya kazi katika makao makuu ya CIA yaliyoko mjini Langley katika jimbo la Virginia kitengo kijulikanacho kama Cyber Intelligence ambacho kinashughulika na ujasusi wa mitandaoni ndiey ambae amewapa taarifa hizo ambazo hadi leo hii CIA hawajazithibitisha wala kuzikataa.

Taarifa hizo zinadai kwamba kitengo hicho cha "Cyber Intelligence" lipo mjini Frankfurt nchini Ujerumani na kinashughulika na kudukua na kuchunguza mitandaoni taarifa mbalimbali kutoka barani Afrika, Mashariki ya kati na Ulaya na kinashirikiana na idara za ujasusi za mataifa ya magharibi kutengeneza program maalum iitwayo "weeping angel" ambazo huingizwa katika vifaa vya umeme na kuvigeuza kuwa vipaza sauti ambavyo vinasikiliza mazungumzo ya watu.

Vifaa hivyo vya runinga ambavyo ni zile zenye uwezo wa kuunganisha "internet" za Samsung ambazo huitwa "smart TV" na zenye kuweza kuboresha picha yaani HD au "high definition" zinageuka kuwa vipaza sauti na kurekodi mazungumzo kisha kutuma kwa siri mtandaoni kwenda kwenye server maalum ya Cyber Intelligence iliyopo mjini Frankfurt.

Hali hiyo pia hutokea katika simu za mikononi ambapo baada ya simu kuwashwa na kuunganishwa na mtandao wa "internet", kwa kutumia program iitwayo "Location" endapo inafanywa iwe hai yaani "enabled" basi mwenye simu huweza kufuatiliwa mazungumzo yake na pia mahala alipo yaani "Location".

Program hii ya Location hutumiwa sana kwenye nchi zilizoendelea na baadhi ya makampuni ya masoko na pia huweza kufanywa ifanye kazi kwa kuweka ifanye kazi kama simu inayo injini ya Google ambayo husaidia kutumia internet.

Google inatumiwa na vifaa vya mbalimbali kama simu za mikononi, kompyuta mpakato na tablets na husaidiwa na mfumo wa uendeshaji wa Android ambapo majasusi huweza kupenyeza program za udukuzi ziitwazo "malware" ili kuweza kusikiliza na kudukua taarifa katika mitandao ya Signal. WhatsApp na Telegram.

Taarifa hizo za WeakLeaks zimeenda mbali zaidi na zimedai kwamba CIA pia wanatumia program maalum kuingilia mifumo ya uendeshaji wa magari ya kisasa na malori au vehicle control system jambo ambalo linaweza kulifanya gari lipate hitilafu na ama kupinduka au kuungua moto liwapo katika mwendo mkali.

Bara la Afrika limekuwa ni soko kubwa la vifaa vya umeme vya aina zote hasa Samsung, Huawei ambapo simu zake hutumia program ya Android.

Miaka ya hivi karibuni kampuni ya Samsung imekuwa ikikabiliwa na matatizo ya uongozi ambapo mwezi ulopita mtandaji mkuu wa kampuni ya Samsung bwana Lee- Jae yong alikamatwa kwa makosa ya Ufisadi, utoaji rushwa, matumizi mabaya ya fedha na ufichaji fedha nje ya nchi.

Samsung inamiliki jengo lake la ghorofa 10 katika bonde la Silicon lililopo katika jiji la San Jose lililoko katika jimbo la California, likiwa ni ofisi kwa ajili ya utafiti wa vifaa vidogo vya ndani ya simu viitwavyo semiconductor ambavyo hutengenezwa kwa kutumia silicon.

Kama kuna ukweli wowote kuhusu taarifa hizi basi hakuna uhuru wa faragha kama unaamua kutumia vifaa vya umeme kwa utashi wako vifaa ambavyo vinatoka katika makampuni tajwa hapo juu.

Chanzo: Mbalimbali
 
Its true hiyo program ipo. However kunajinsi ya kuidhibit kwa kubadilisha settings za simu yako
kWENYE teknoilojia Any receiver is a transmmiter and any transmeter is a receiver.Uwe na TV yoyote,radio yote zinakuwa na uwezo wa kupokea vitu hewani na zina uwezo wa kupeleka mbele kwa mbele kutoka ulipo kwenda kokote.TV UNAITAZAMA NA YENYEWE INAKUTIZAMA MTU AWEZA kukuona hadi sebuleni kwako kupitia tv yako akiwa marekani au popote.Huu ulimwengu wa digitali una uzuri wake na mambo yake
 
Kama wewe sio gaidi sioni cha kuogopa hapo,wadukue tu sana sana watakutana na msg za michepuko yangu na call za kuomba nyuchi.uzuri ni kwamba wakiona kiashilia kibaya kwa nchi wanazipa taarifa mamlaka husika ziweze kufatilia.ni kitu kizuri kwa ulinzi wa dunia yetu dhidi matukio ya kikatili ya kigaidi.waendelee tu
 
Hivi wanawezaje kuwafuatilia watumiaji wote wa Simu coz tupo wengi sana zaid ya 1bn kuliko hao wafanyakaz wao
 
Hili jambo liko wazi hasa kwa mtu unaefikiria, Kwa mfano nokia LUMIA zenyewe zina sky drive ambayo inahifadhi kila aina ya taarifa hasa picha na video........
 
Hivi wanawezaje kuwafuatilia watumiaji wote wa Simu coz tupo wengi sana zaid ya 1bn kuliko hao wafanyakaz wao
mbona rahisi tu...wewe mpigie mtu simu,akipokea anzisha mazungumzo halafu chomekea maneno haya

"I'm planning to attack america tomorrow".

"my jihad brothers are on the way to USA to attack the white house".

" the suicide vest is complite".

pia unaweza ukayabadili kwa kiluga chenu almradi tu uwe unayatamka hewani ktk simu.

halafu sikilizia.
 
mbona rahisi tu...wewe mpigie mtu simu,akipokea anzisha mazungumzo halafu chomekea maneno haya

"I'm planning to attack america tomorrow".

"my jihad brothers are on the way to USA to attack the white house".

" the suicide vest is complite".

pia unaweza ukayabadili kwa kiluga chenu almradi tu uwe unayatamka hewani ktk simu.

halafu sikilizia.
Hahaha usimfundishe tabia mbaya mwenzako
 
Back
Top Bottom