Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,539
- 4,856
Leo tarehe 27 september 2014 ni siku ya maadhimisho ya wiki ya viziwi duniani (international week of the deaf) ambayo kitaifa imefanyika mkoani Arusha na hakika nimeshuhudia mambo makubwa na kuamini kuwa kila binadamu anauwezo wa kufanya mambo makubwa bila ya kujali anaulemavu wa aina gani.
Naikumbuka kauli ya mkuu wa wilaya ya arumeru aliemuwakilisha mkuu wa mkoa,alisema kuwa KUSIKIA SIYO KUFANIKIWA,na kweli maajabu na uwezo wa binadamu upo kwa kila mtu.
Ujumbe mmoja katika maadhimisho hayo ulikuwa ukisema JAMII ITAMBUE UMUHIMU WA LUGHA YA ALAMA NA KUITUMIA.
Na ujumbe mwingine ulikuwa ukisema SISI SIO BUBU NI VIZIWI.
Pia walikuwapo wanafunzi wa rika mbalimbali na niliweza kuzungumza kupitia na wanafunzi wawili maandishi kwa kuwa sifahamu lugha ya alama na wanafunzi hao wanajua kusoma na kuandika.
Lugha ya alama ilianza kutumika zaidi ya miaka mia iliyopita huku bwana Juan (John) Pablo akiwa ni mgunduzi wa lugha ya alama ambayo imeleta mabadiliko makubwa katika jamii.
Mwaka 1993 utafiti wa lugha ya alama waanza Tanzania na miaka miwili baadae kamusi ya kwanza ya lugha ya alama yatengenezwa.
Ikumbukwe kwamba wiki ya viziwi duniani ilianza kuadhimishwa mwaka 1958 na kuendelezwa mpaka leo.
Pamoja na kuwa na ulemavu wa kusikia na kuongea lakini viziwi hao waliweza kucheza ngoma ya asili,maigizo na hata kwaito.
Jiulize,ni changamoto kiasi gani wanazopata watu hawa na akili kubwa kiasi gani wanayotumia kwa kucheza muziki hali ya kuwa hawasikii.
Wakipewa nafasi wanaweza na wanauwezo wa kufanya maendeleo katika taifa letu.
Kuna jumla ya vyama vya viziwi 133 duniani.
Ni wakati wa jamii sasa kutambua umuhimu wa lugha ya alama.