mzee wa kijiwe
JF-Expert Member
- Jun 25, 2012
- 947
- 685
Sina uhakika ni nani aliyeubadilisha upepo huu kwa namna ya ajabu kidogo! Upepo ulionekana kuwaendea vizuri mwezi mzima wa January na wiki mbili za mwanzo za February. Upepo ulionekana Kama utazidi kuvuma kwa kasi na kuwa favor Lumumba haswa baada ya kamatakamata iliyoasisiwa na David Bashite. Vijana wa Kinondoni yalipo makao makuu ya CDM walikuwa wanyonge sana hata uvivu uliwajaa kujibu hoja humu ndani na hata kwingine kwenye mitandao.
Leo hii ninapoandika Lumumba wanatafutana kwa tochi humu ndani, hawaamini game changer ameweza kuwageuzia kibao tena kwa speed ya ajabu! Upepo ni mbaya kwa Lumumba sijui Kama hawatashikana uchawi maana hawajui ni nani wa kumkamata?
Je ni Wema? Ni Mbowe? Ni Gwajima?
Wamebaki vinywa wazi wanamwona Mbowe anadunda mtaani walitamani alale central hata siku moja imeshindikana, sasa wameitwa mahakamani, wanajiuliza waende wasirnde? Wameitwa bungeni wanajiuliza twende?
Majaji watatu wa mahakama ya juu nchini bila kupepesa macho wameishambulia serikali, haswa ofisi kubwa kuliko zote inayotakiwa kutoa na kusimamia haki, wameambiwa kuwa wao ni vinara wa unyanyasaji, wanawaaibisha wanasheria wote nchini na mahakama inavuna aibu kutokana na ofisi yao!
Upepo huu umeambatana na kejeli, nyingi ukienda kwenye fb, Instagram, jf vijembe njenje!
Nasikia waalimu wanaanza mgomo!
Upepo huu je ni majibu ya maombi ya watu wa Mungu? Labda lkn hali sii ya kawaida, Kama upepo ukivuma namna hii na Kama Lema atapata dhamana wiki hii natabiri nahodha kutosa abiria baharini mapema vinginevyo meli itazama!