Wifi anasema anampenda daktari aliyemsaidia kujifungua

mamkuu5

JF-Expert Member
Nov 24, 2014
1,139
716
Habari za siku wadau,

Mwenzenu hivi nimepata kibarua kigumu cha kuuguza mzazi. Nina wifi yangu kiumri ni kama anamiaka 25 huyu amejifungua kama ana siku 14 hivi,alisaidiwa na Dr mmoja mkaka na amejifungua kwa njia ya kawaida.

Kinachonishangaza ni pale anapoamua kusema anavyojiskia ,alianza kulia nikambembeleza aniambie akasema ntakwambia ila usimwambie mchumba wangu,nampenda Dr alienizalisha nampenda sana sina jinsi ya kumwambia ila naumia wifi nampenda.Anasema yupo radhi kwa lolote simuelewi hataa.

Naomba ushauri maana sina pa kuanzia hata.
 
Habari za siku wadau,mwenzenu hivi nimepata kibarua kigumu chakuuguza mzazi.
Nina wifi angu kiumri ni kama anamiaka 25 huyu amejifungua kama ana siku 14 hivi,alisaidiwa na dr mmoja mkaka na amejifungua kwa njia ya kawaida ,
Kinachonishangaza ni pale anapoamua kusema anavyojiskia ,alianza kulia nikambembeleza aniambie akasema ntakwambia ila usimwambie mchumba wangu,nampenda Dr alienizalisha nampenda sana sina jinsi ya kumwambia ila naumia wifi nampenda.
Anasema yupo radhi kwa lolote simuelewi hataa ,
Naomba ushauri maana sina pa kuanzia hata...
Dah!! Huyo itakua ni uzazi bado inamsumbua..atalua sawa tu...
 
wanawake wengi huwa wanakuwa hawapo sawa mapema baada ya kujifungua, wengine huwa na hisia za chuki mno, wengine kulia bila sababu, hasira na mengineyo.
hivyo basi mshauri huyo wifiyo asubiri baada ya siku 40 kisha mtaliongelea hilo swala.
nina uhakika hatokuwa tena na hisia hizo baada ya hizo siku.
 
wanawake bana. Wanakoroga mambo akiachwa anaanza kulalamika
Hiv huwa mnajisikia raha kuzaa kila mtoto baba yake?
Mwambie atulie atakosa vyote.
 
Dk wakati anamsadia kumzalisha,akawa anamshika mashine na kumchua kitaaalam na maneno mazuri ya kumtia nguvu Ili ajifungue kwa usalama...yeye Ana mawazo tofauti...basi hata kupona bado Ana mawazo hayo!...hizi ndoa hizi majanga.
 
Back
Top Bottom