Wife kagoma kusali Jumapili ya Oct 25, anataka 24 Oct

Wife kagoma kusali Jumapili ya Oct 25, anataka 24 Oct

1st AID

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2014
Posts
1,079
Reaction score
523
Wasalam

Kuna vitu hufikia mahali nashindwa kumshurutisha mtu ikiwa ni pamoja na hili la kiimani, huyu ni mke wangu anadai yeye uchaguzi mkuu ni muhimu kwa sababu it will be once in five years, but Jumapili zitakuwepo 52 kwa mwaka mara 5 sawa na Jumapili 260 kabla ya uchaguzi mwingine.

Mimi msimamo wangu ulikuwa Imani haihusiani na maswala ya uchaguzi hivyo kuailisha ibada eti kwa ajili ya kuwahi foleni sikuona kama ni swala la kuingiliwa. Tungetoka church na kuelekea huko kumchagua atakae tufaa, sasa jana kapata nguvu ya kunivimbishia mashavu baada ya kuona maaskofu kadhaa wameidhinisha vibali ya misa kuwa Jumamosi! Eti mapadri hawatakuwepo!...

Najiuliza hili kanisa linaongozwaje? Siku maalum za ibada zinaweza kubadilishwa tu? Hii siku ya kuabudu J2 hasa ilichaguliwa na nani? Kirutilijia imekaaje? Wajuzi mnisaidie ili nimsaidie wife pia kufanya maamuzi sahihi!
 
Nimesoma kuna kanisa limeambia waumini ibada zitakuwa jumamosi ili jumapili wakachanje sawa sawa.
Ila short cut, mruhusu akasali kwa gwajima jumamosi usiku ili jumapili akapige nae kura.
 
Kwani hiyo ibada anayoenda ni kanisa analosali siku zote au kabadilisha kusali tu kwa ajili ya 25 oktoba?

Kama ni kanisa la kila siku sioni tatizo kwa wife ila tatizo liko kwa uongozi wa kanisa.
 
Au anaenda kuliombea taifa na wakulu :ranger::msela:
 
Mada zinazoletwa humu siku hizi ni kizungumkuti kitupu, binafsi sijaelewa suala ni mke wako kusali jmosi au kanisa kuruhusu sala hiyo jmosi? naona umejitahidi kuunganisha visa na matukio hatimae ukapata story isiyokua na kichwa wala mkia. Mpaka uchaguzi uishe tutaskia mengi hahaha
 
Hilo lisikusumbue bro. Imani ni kitu kingine kabisa,huenda akakutii kwasababu u mume ila kwa ndani haendi kuabudu. Muache afanye analoona kwake ni sawa kwa siku hiyo ya upigaji kura. Lamuhimu km unaona kwenda kanisani ni lazima siku hiyo ,amkeni fanyeni Ibada hapo nyumbani ya familia. Nenda ibadani aende kwenye kura. Jioni atakaporudi Luna makanisa yenye vipindi jioni aende kusali akiwa na amani. Kuna haja gani yakulumbana kwa jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wenu? Amani ikikosekana ndani kwa siku moja kitanda chenyewe kinakuwa kichungu. Mruhusu aende na km jmos anaenda ibadani msindikize kwaamani. Mm mwenyewe natamani siku hiyo nisiongoze Ibada ili niwe guru zaidi,lakini kwasababu ya Alienituma sinabudi kufanya kazi yake kwa Upendo na Raha.
 
Head of the house is always a man ,unless you decide otherwise. For this case your order was the final and has to be followed not discussed.
 
Siku iliyopangwa na mungu na kuandikwa katika biblia, katika amri kumi za mungu zisizobadilika, ni siku ya saba, sabato, yaani jumamosi. Soma biblia kitabu cha kutoka sura ya 20:8-11.kwa nini sasa tusali jumapili? Kila mwenye akili atafakari kupitia maandiko matakaifu.
 
Naamini hakuna ibada ya kulazimishana, ikiwa ametaka hivyo kuna ubaya gani, Wewe nenda J2 na yeye mwache J1, lazima mjue kucompromise saa nyingine.
 
Umeoa ukiwa na umri gan mkuu?
Na mmedum kwa mda gan kwny ndoa?
Maana nadhan hizi ndoa za digital kufuata fasheni ni shiiiiidah!
 
Ibada ni kila siku sio jumapili tuu na kura ya Rais na Wabunge ni mara 1 baada ya miaka 5. Kwani asipoenda siku hiyo kunanininiii kama nawe sio gubuuuu limekujaa???? Punguza bangi changaa wewee tena za kutafunia chooni. But sorry!
 
Nimesoma kuna kanisa limeambia waumini ibada zitakuwa jumamosi ili jumapili wakachanje sawa sawa.
Ila short cut, mruhusu akasali kwa gwajima jumamosi usiku ili jumapili akapige nae kura.
Point that muzzle to the safe direction then we may continue... Gwajima ukimzungumzia au kumtajataja yatakukuta ooh! ana helicopter ya ajabu.
 
Point yako ni ipi sasa?

KANISA NDIO LILILOCHUKUA UAMUZI HUO
MKEO AKIWA KAMA MWANAKANISA HANABUDI KUKUBALIANA NA KANISA.
 
Hello Mwanamabadiliko Mwenzangu, Tarehe 25 Octoba ndo siku ya kulikomboa Taifa letu toka mikononi mwa maccm. WAPIGIE SIMU BABU NA BIBI, MASHANGAZI NA WAJOMBA, NDUGU JAMAA NA MARAFIKI wa Vijijini na Mijini waambie juu ya TAARIFA za UKOMBOZI HUU.
Wampigie KURA ✌EDWARD LOWASSA na WABUNGE na MADIWANI wa vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR MAGEUZI na NLD tu.
 
Back
Top Bottom