wife anapokulalamikia rafiki yako anamtaka....


Mkuu, jamaa kapataje namba ya wife wako? Anzia hapo kwanza, then endelea.
 
Taka kuona msg alizotumiwa mpaka akatukana. Maana inawezekana hiyo ni cover tu kwaajili ya kukupumbaza wewe, inawezekana wamegombana, au kweli huyo jamaa alikua anamsumbua mpaka mkeo akashindwa kumvumilia.

Ila kama kweli hayuko interested nae ablock namba ya huyo jamaa ili asipate simu na text zake. Kusema tu aignore zikiingia haitoshi maana watu wengine wanaboa kupitiliza.
 
anamwambia asimsumbue yupo na mume wake, lakini si nilimwambia aachane nae?!

Exactly Joji na hakukusikiliza. Ingempasa pale alipogundua anamsumbua kwa nia ya kumtongoza na possibly kumtaka mkeo aende nje ya ndoa yake angeacha kuwasiliana naye. Hata hiyo namba ya simu ya huyo jamaa hangepaswa kuwa nayo baada ya dhamira chafu aliyoonyesha jamaa
 
nashukuru kwa ushauri na kunipa faraja...
nilikuwa nichukue maamuzi mabaya sana
 
Nadhani alikwambia kua jamaa anamtaka ili wewe ukamtukane, ikibidi umdunde. Alipoona wewe unamwambia aachane nae, akajua unamuogopa jamaa ndio akaamua amtukane mwenyewe.
Sasa wewe fanya hivi: mkalishe mke wako na umwambie KWA NINI ulimwambia aachane nae. (mfano: Mwambie sio uoga, ila uliona kukaa kimya ni jibu bora kuliko hata kumtukana).
 
ushauri wenu unahitajika nini nifanye

Pambana na mkeo mbane mpaka aeleze ukweli na btw usimbane kwa nini alimpa namba ya simu. Honestly kutoa namba ya simu haina ubaya kuna kesho na keshokutwa one might need his help. Issue ni pale ambapo aliyepewa namba anaanza kui-abuse na kuleta mambo ya ajabu ajabu kama hayo ya kutongoza mkeo. Na inapaswa mke akiona hivyo aacha mawasiliano naye fasta.
 
Huyo jamaa ni rafiki yako pia (with reference to jina la thread)?
 
kabana na mkeo mpaka kieleweke usisahau kumwambia aache tabia ya kutoa namba za simu ovyo
 
jojipoji, kama ukigundua mkeo amechat uko tayari kuvunja ndoa?
Kama uko tayari mbane hzdi ujue ukweli
kama haukotayari ipotezee ila mwambie mkeo asiwasiliane tena la sivyo unamrudisha kwao.
Sababu kama haupo tayari kuachana afu ukagundua anacheat utaumia mno.
 
au wametibuana ndo akaanza kumtukana?
Kama humtaki wala huna wazo nae hata kumtukana is a favor.
upo very ryt kongosho ,silence z th greatest psychological weapon of all....huyo wife wako anamuentertain huyo jamaa...kuwa serious mbane mkeo ,s'thng fishy z going on hapo na kugombana na mwanaume mwenzio ni kujidhalilisha mwenyewe assume unamfuata jamaa hlf kumbe mkeo ndo anayemtokea....
 

Lazima kieleweke tu.....
dawa chungu lakini inatibu so lazima nivumilie
 

sawa kiongozi ahsante kwa ushauri
 
Kama umekuta msg ya kumtukana nafikiri anaonesha msimamo ila na wewe endelea kudeal na mkeo
Haya mambo ya kuambiwa na mpenzi wako kua fulani anamtaka si ya kuamini sana, mara nyingi utakuta yeye mwenyewe mkeo ndie anaemtaka jamaa ila hiyo inakua ni njia ya kuondoa kile kilichomjaa moyoni mwake kwa kusema eti jamaa anamtaka.
Nakutakia kila la heri "ABIRIA CHUNGA MZIGO WAKO"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…