Mwaka huu, mfumo mpya wa Wireless wa Wi-Fi 7 utaanza kuchukua nafasi na wiki hii kampuni nyingi zimetangaza zitaanza kutengeneza vifaa na chip ambazo zitakuwa zinakubali mfumo mpya wa Wi-Fi 7 ikiwemo kampuni ya Qualcomm.
Kwa sasa dunia ipo katika WiFi 6 na WiFi 6E; ila tayari WiFi inaanza kuingia sokoni na itakuwa na uwezo mkubwa kuliko mifumo ya Wireless ya zamani.
Katika upande wa Mabadiliko, WiFi 7 itakuwa na sifa zifuatazo:
1️⃣ WiFi 7 itakuwa inafanya kazi katika masafa ya 2.4GHz, 5GHz, na 6GHz bands kama WiFi 6E.
2️⃣ Itakuwa na speed ya 30GB kwa sekunde, ambapo ni speed kubwa kuliko speed ya 9.6GB ya WiFi 6.
3️⃣ Itakuwa na performance kubwa kwa sababu itakuwa inatumia channel bandwidth ya 320MHz mpaka160MHz.
Mfumo mpya wa Wireless unakubali hata vifaa vya zamani hivyo bado inaweza kufanya kazi na kuboresha speed ya vifaa vingi ambavyo vinatumika sasa.