Kila chenye mwanzo lazima kiwe na mwisho. Tuliumbwa ili TUISHI halafu ndo tufe. Hapo kwenye kuishi ndo kwenye majibu au sababu za sisi kuumbwa. Ili tuishi, yaani tufanye kazi, tuibadili dunia na kuwa mahali pazuri pa kuishi kwa wale wanaokuja; tujenge mahusiano mazuri kati yetu wanadamu na kati yetu na Mwumba ili tutakapokufa - kwa sisi tunaoamini katika Mungu - tukakae na Mwumba milele. Tukiishi hovyo hatutakuwa na faida kwa dunia hii wala kwa 'dunia' ya roho tunayoiendea. Kwa mantiki hii hakuna aliyeumbwa au kuzaliwa kwa bahati mbaya, bali kila mtu kaumbwa kwa MALENGO, NA MAKUSUDI maalum ya kutekeleza hapa duniani. Kumbe tekeleza hayo, nawe UTAISHI si hapa duniani tu bali pia kule kwa Mola wetu.