Why Do We Blame God for Catastrophes? Please Help... What do you Think.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Why Do We Blame God for Catastrophes? Please Help... What do you Think..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by VoiceOfReason, Feb 13, 2011.

 1. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Baada ya kuona watu tunavyomlaumu Mungu kwa makosa yetu wenyewe nimeona nilete hii article Jamvini ili tuijadili

  Why Do We Blame God for Catastrophes?

  Source: Why Do We Blame God for Catastrophes? > The Good News : November/December 2001

  Nimekumbuka na lile Swali Kuna Mdau aliuliza hapa, na nitauliza tena..., Does a Good Wife Really Comes from God..? au All Wives are made good ni uchakachuaji wa binadamu ndio unafanya wapotoke and we should not blame God yakitukuta.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kujipa moyo...kumpa mtu mwingine lawama..kukataa responsibility!Kumtupia Mungu lawama makes us feel better!We don't want to admit our mistakes..wrong doing and feel guilty about it!We would rather blame it on a higher power and feel like there was nothing WE could have done because God wanted and made it happen!
   
 3. LD

  LD JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwa jinsi ninavyofikiria mimi. Tangu mwanzo Mungu aliumba kitu chema duniani tena kwa wakati sahihi,kwa sababu hata kazi ya uumbaji hakuifanya mara moja akamaliza, aliumba kila kitu kwa wakati wake kwa muda wa siku saba.Mwanzo 1:31, Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama ni chema sana.Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.

  Sasa basi kila kitu ni chema kwa wakati sahihi na Mipango ya Mugu ipo kwa wakati sahihi. Ila mwanadamu kwa kutokutii na kutulia na kuwa na kiasi tunaharibu mpango wa Mungu ktk maisha yetu.

  Mwanadamu hana uvumilivu,anapenda short cut na kurahisisha maisha, na Mungu halazimishi, kwa sababu amesema kabisa nimeweka mbele yako laana na Baraka chagua Baraka ukaishi, lakini sisi tunachagua laana.Kumbukumbu la Torati 28:1-44 unaweza kuendelea sura nzima ya 28.

  Kuna nguvu za giza pia, shetani na majeshi yake ktk ulimwengu wa roho, ambazo zinapingana na nguvu ya Mungu, ndio maana tunatakiwa kuomba na kutafuta utakatifu.DANIEL 10:11-13.

  Mwanadamu anafanya mambo kwa kuzitegemea akili zake bila kumshirikisha Mungu hata jambo moja, wakati mwingine nafsi/dhamira inamsuta kabisa lakini anafanya. Likiharibika au likileta matokeo mabaya anamzingizia Mungu, lakini kiukweli Mungu anakuwa hahusiki hapo. Tujaribu tu kufikiria uovu wowote kabla au unapofikiria kuufanya lazima roho ikusute, huyo ndo Mungu anaongea na wewe. Ukitii ndo salama yako, usipotii hasara kwako.

  Narudia kusema tena hakuna mke mbaya, ila kila mwanamke ameumbiwa mume wake na kila mwanaume ameumbiwa mke wake wake. Tunachokosea unamchukua mke wa John unamuacha mke wako naye anachukuliwa na James kamwe hamwezi kuendana. Mfano mwanamke anaweza kuwa mchafu lakini mwanaume ni msafi na anajua kabisa hiki kinakaa hapa na hiki kinatakiwa kikae hapa sasa kama aliyemuoa ni mke wake akimfundisha ataelewa. Lakini kama sio mke wake ataona mwanaume ana gubu, anasema sema, haridhiki na utendaji wake. Hivyo mwisho wa siku na mwanaume naye anachoka anaona kero.

  Mtu anaoa/olewa kwa kuangalia ndugu watasema nini juu ya huyu mwenzangu, ana pesa, ni mzuri, watamkubali. Tunasahau huko ndani mtakuwa peke yenu. Au unanipenda mimi kwa sababu naandika sana unaamua kunioa, lakini humo ndani siji kuandika, au unanipenda kwa sababu umeniona naimba vizuri, navaa vizuri huenda nipo hivo barabarani tu lakini uhalisia wangu sio huo. Katika kuchagua mke kuna vitu vya ndani na vya kiroho zaidi vya kuangalia ambavyo siri anayo Mungu.

  Daa namaliza nafasi ya saver, ngoja niache kwanza.
   
 4. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye BOLD...
  Hakuna mke mbaya.., wala hakuna mtu anayezaliwa na Tabia mbaya yote ni mazingira na malezi, na tukiwa wavumilivu ninauhakika hata mke wa John ninaweza kuishi nae raha mustarehe...

  Sasa ubishi wangu unakuja mtu ndoa inamshinda eti anasingizia Mungu hakunipangia huyu, au anapenda mwingine anasema huyu hakuwa chaguo la Mungu ila huyu ndio anafaa.

  Pia hakuna mtu anapenda kukaa na mzigo, iwe James au John.., na Busara na uvumilivu wa John isiwe kigezo kwamba yeye alipangiwa amuoe mke mvivu, mgomvi na muongo.. au unasemaje?

  Kwahiyo mimi naona wote waliopo wanafaa sana na kipimo cha mke mzuri ni uvumilivu wako wa mangapi unaweza kuyasamehe,
   
 5. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Yes Just pointing a finger... wakati we are our own worse enemies
   
 6. LD

  LD JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  Well, kipimo cha uvumilivu. Nafikiria hivi!! Naweza nikaweza kumvumilia John kuliko ninavyomvumilia James!!

  Mfano nashindwa kuvumilia tabia ya ulevi kwa James, kunijia na domo linanuka pombe na sigara, lakini nikamvumilia John kwa tabia yake yakuingia na viatu vyenye tope hadi bed room. Wakati huo huo mwingine haoni shida hio tabia ya James lakini hii ya john anatamani kuikimbia nyumba. Fikiria hapo!!
   
 7. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  True lakini tukirudi kwenye chanzo, hii issue ya ulevi na uchafu ni kutokuwa na Busara za mtu na sidhani kama Mungu anapenda mtu kutokuwa na busara, pia uvumilivu nadhani inabidi wote tuwe na uvumilivu wa mizigo tuliyonayo...

  kwahiyo naona kulingana na wewe upo wapi hapo ndipo utapata Mwenza wako.., sidhani kama Mungu anaweza akakupangia James wako awe Singida wakati wewe upo Dar.., ila huyo ambaye unaweza ukakutana nae by Chance ni kumuomba Mungu uweze kuvumilia yote mabaya aliyonayo..., na kama nyote mna fikra zinazoendana nadhani mnaweza kuishi kwa kukubali utofauti wenu, na mmoja kutokujaribu kufanya jambo ambalo ni karaha kwa mwingine..., Sababu kwanini uende na viatu vya matope mpaka chumbani wakati mwenzako kapiga deki.... au ukinywa pombe na kuvuta sigara kwanini usipige mswaki...

  Hivyo basi nadhani mke mwema ni Mwenye Busara..., na wake wote wametoka kwa Mungu.., na yataka Mume mwenye Busara au Mke mwenye Busara kuweza kukaa na mke/mme na kumfanya awe mwema. Sababu wema wa John wa kuweza kukaa na Asha mwenye Tabia mbaya hakufanyi Asha awe mwema sababu ya uvumilivu wa John...:popcorn:
   
 8. L

  LAT JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  VOR... mimi naomba niseme .... tunamsingizia mungu ... period
   
 9. LD

  LD JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kweli, nafikiria hivi!! Kwa sababu njia za Mungu sio njia zetu na mawazo yake siyo mawazo yetu hata kama Asha atakuwa Marekani, kama huyo ndo Mungu kanipangia lazima itatokea njia tutakutana!!

  Hapo kwenye busara ni kweli Mungu hauhusiki asilimilia mia moja. Hapo kwenye uvumilivu bado nafikiria moyo wa kuvumilia mambo unatofautiana kati ya mtu na mtu na tabia ya mtu anayehusika.

  Mfano kuna mtu unakuta yeye ni mtu wa kujali sana mambo, jambo dogo litamuumiza hadi analia, akiwa na mume anayemuelewa atambembeleza na kumfanya aone hilo jambo sio kubwa kiivo. Au atamtia moyo. Na huyu mtu anakuwa rahisi kumuelewa kutokana sijui nisime chemistry zao!! Anyway hivo hivo.

  Kuna mwingine hawezi kuvumiliana na moyo wa jinsi hii.Hana muda wa kubembeleza wala kutia moyo, utasikia tu labda tatizo lakoi wewe unakuza sana mambo shauri yako, utajua mwenyewe bwana. Badilika nakwambia!! Unadhani atakuwa na amani akiwa na mtu hivi, maisha yatakuwa magumu kila siku.
   
 10. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #10
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye nyekundu, sababu Mungu ndio anatupangia mwenza huoni kwamba yeyote tutakayempata ndio Mungu ametupangia ?, na tukishindwa kukaa nae ni sisi ndio tumevunja kila Mungu alichotupangia ?

  Kwenye Bold kwahiyo sababu mimi ni mvumilivu.., au sababu wewe ni mvumilivu na unavumilia yote huoni kwamba wewe basi utakuwa mke mwema wa mtu yoyote awe Juma, James, John au Bakari ?
   
 11. LD

  LD JF-Expert Member

  #11
  Feb 13, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nafikiria hivi, sio yoyote utakayempata ametoka kwa Mungu, inaweza kuwa ni nafsi yako tu imeamua. Mfano unaweza kumpenda mtu kwa kuangalia elimu yake na ukamkubali vile alivyo kwa elimu yake, na ukamkataa mtu mwenye elimu ya chini kumbe huyo wa chini ndo alikuwa chaguo la Mungu na huenda Mungu angefanya njia akakubariki na yeye akasoma/ukamsomesha halafu maisha yakaendelea.

  Hapo kwenye uvumilivu naomba tusiseme kuvumilia tuseme kuchukuliana na udhaifu wa mtu. Manake uvumilivu umekaa kisadaka sadaka zaidi. Kwa hiyo naweza nikachukuliana na udhaifu wa mtu B lakini nikashindwa kuchukuliana na udhaifu wa mtu A. Wakati huo huo mwingine akaweza kuchukuliana na mtu A akashindwa kwa mtu B.
   
 12. T

  Topical JF-Expert Member

  #12
  Feb 13, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kumsingizia Muumba kwa majanga yanayotokea ni matokeo ya yafuatayo
  1. "ukosefu wa imani" thabiti..mfano watu wa luti walipokosa imani na kufanya uchafu wao waligharikishwa kwakuwa hawakuwa na imani kwa Muumba...

  2. "Kupenda dunia na starehe zake" kuna mambo yanaweza kukutokea mfano wewe ni mcha mungu lakini inapata misukosuko kuliko mtu mbaya (mchafu)..unaanza kusema why me? mfano kufukuzwa kazi, matatizo ya ndoa n.k. kila mcha mungu atapewa mtihani ili akifuzu vema bila kumlaumu Muumba aende peopni...utakuta anayemlaumu Muumba kwa matatizo yake ni mtu anayependa dunia ..sana hajui hukop akhera kulivyo pazuri (imani yakini)

  3. Sisi kwa Muumba ni vitu vidogo sana kama wewe unavyoona miti mfano wake..kama wewe binadamu unaweza kukata miti yenye uhai na kuua wanyama wengi (sisimiz n.k) ili kujenga nyumba, barabara kwa faida yako..then Muumba anaweza kuleta chochote kwa faida ya kizazi kingine cha watu..

  ntaendelea
   
 13. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #13
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo unataka kusema haya mambo mabaya yanayotokea ni mitihani ya Mungu ? Mfano wewe hufanyi kazi, unachelewa kazini na unatembea na mke wa Boss...., Ukifukuzwa kazi huo ni mtihani au ni uzembe wako mwenyewe na tabia zako mbovu zilizopelekea hii adhabu ambayo inakustahili...?

  Katika issue ya kusafisha ulimwengu kwa majanga kwa faida ya vizazi vijavyo hapo tutakuja baadae kwanza tudeal na hili la mitihani ya Mungu
   
 14. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #14
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo kipimo cha mke/mume kutoka kwa Mungu au kutokutoka kwa Mungu ni furaha au huzuni katika ndoa ?, Kumbuka kuna mambo ambayo hayavumiliki mfano abuse (mental and physical) sidhani kama Mungu atapenda yeyote akumbane na haya majanga, na hawa wanaopiga wake zao nadhani ni ushetani/ukichaa uliowakumba ukubwani

  Je hawa tuseme Mungu amewatenga ili wasipate wenza wao, au atawachagulia watakaovumilia kuwa abused ? Na ninajua kuna Dini haziruhusu Divorce.., je unapogundua kwamba huyu sio chaguo la Mungu utafanyaje ili uombe Mungu akupe chaguo lako?
   
 15. T

  Topical JF-Expert Member

  #15
  Feb 13, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwa hayo niliyo underline...hiyo nistahili ya mhusika na hawezi kumlaumu Muumba

  Kanuni za Muumba ni kuwa ufanye jitahada utapata nusura (msaada wa Muumba) sasa ukikaa hufanyi chochote au mzembe unastahili adhabu...hiyo ndio kanuni

  Pia kanuni za mafanikio duniani na Akhera imewekwa ni kufanya kazi kwa mwisho wa bidii yako na maarifa yako, kusubiri bila kweka dhana mbaya kwa Muumba, kutii amri zake..etc..

  Ikiwa utapata kitu umshukuru given umefanya kanuni niliyosema hapo juu (yaani bidii na maarifa hadi mwisho wako)

  Ikiwa utakosa japo umefanya kila jitahada umshukuru Muumba maana huenda ukapenda kitu sana kumbe hakina faida kwako..huyo ndiyo muumini wa kweli mwenye imani thabiti

  Kwa muumini kukosa ni mtihani (given amafuata kanuni zote) na kupta ni mtihani (siyo kwamba ni ujemadari) eti mimi nimepata kwakuwa nina akili sana au bidii sana ni neema za Muumba na mitihani yake...
   
 16. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #16
  Feb 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Binafsi naamini mambo yote ya heri na ya shari anapanga mungu.
  Ninapofikwa na matatizo huwa simlaumu mungu bali humuomba aniepushe na hayo matatizo.
  Ninapokuwa na faraja ninamshukuru, ninapohitaji kitu ninamuomba.
  Siku zote unapokuwa katika wakati mgumu sana ujue wakati wa neema umekaribia.
  waswahili wanasema hakuna msiba usiokuwa na heri ndani yake.
  Ukiachwa na mpenzi ujue mungu amekuandalia mwingine mzuri zaidi.
  Anapokufa mzazi/mlezi ujue mungu anajua namna utakavyoishi.
  Unapofeli shule ujue mungu amekupangia namna nyingine ya kufanikiwa.
  Kila kitu hutokea kwa makusudi.
  Hebu watu wote mjichunguze wakati mlipokuwa katika wakati mgumu sana sana uangalie nini kilichofata baada ya huo wakati mgumu.
  Jibu ni faraja na neema.
  Kuhusu suala la mke mzuri ni kwamba wake wote ni wazuri isipokuwa wewe mwanaume unaweza ukamfanya awe mbaya kutokana na tabia zako.
  Kama A ni mbaya mbona alivyoachwa na B ameenda kuolewa na C na wanaishi vizuri?
  Inawezekana mbaya ni wewe ila ubaya wako unauona kwa mwenzio.
   
 17. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #17
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hus.., Mfano nimeomba mkopo benki nifanyie biashara lakini, badala ya kufanya biashara nimefuja mali hizo nyumba imepigwa mnada (huyo ni Mungu au Uzembe wangu)?

  Badala ya kulala na Chandarua nimeacha mbu wameniuma nimepata malaria
  Ukiwembe wangu umepelekea nimepata ukimwi
  Kuendesha gari kwangu huku nimelewa kumenifanya nipate ajali na kupooza mwili
  Mapepe yangu yamefanya mke na watoto wanikimbie
  Kuacha jiko la gesi limewaka kumepelekea nyumba yangu na mtaa mzima kuungua moto
  ulevi wangu umepelekea nifukuzwe kazi

  Haya Hus.... hapo kweli tunaweza kusema Mungu ndio kaleta hayo majanga au kauzembe kangu ndio kamesababisha?
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  Feb 13, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Vitu vingine ni matokeo tu ya matendo yetu!Sio adhabu wala mtihani!Kama mtu hasomi kwa bidii siku akifeli ni juu yake..Akiwa na matumizi mabaya akija kuishiwa ni juu yake..Akilima shamba bila kujali sana mazao yake akikosa mavuno ni juu yake!Mungu anaweza kukuongoza ila sio kukufanyia mambo yako!Vitu kama ukame navyo vinaweza kua matokea ya kutojali mazingira yetu (kisayansi zaidi) au kuadhibiwa na Mungu iwapo lawama tutampa yeye!Magonjwa na vita vile vile..Mungu hamkabidhi mtu bunduki akapigane
   
 19. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #19
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mimi ninachoamini ni kwamba Mungu amzibii mtu.., ukifanya jambo kama linavyotakiwa lifanywe basi litafanikia.. (ndio maana hata mafisadi na majambazi na watu wabaya pia wanafanikiwa).. sababu wanafata kanuni za kitu wanachofanya zinavyotakiwa zifanywe...., Imani yangu ni kwamba hata wewe leo ungefata steps zote za Bill Gates kama alivyofanya hatua kwa hatua (with the same attitude) na wewe leo ungekuwa kwenye shoes za Bill Gates..., na Bill angefata yote ambayo wewe umefata mpaka leo dakika hii angekuwa anayo yote ambayo umeyapata wewe....,
  The Choices we Make Today is What Determines the Opportunities and Blessings we will achieve tommorrow.
   
 20. Wakumwitu

  Wakumwitu JF-Expert Member

  #20
  Feb 13, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  Jamani ni swali tuu nauliza, hivi harufu ya sigara na pombe inaweza toka kwa kupiga mswaki??? Sivuti sigara na wala sinywi pombe. Just curious
   
Loading...