Brazili wanacheza na deal ya mass mobilization ya 'will power' collection toka bara Afrika kuwasaidia kushinda. Hizi ndizo zile dili kama za Vodooism, kama wafanyavyo matajiri wa Kidosi, kina Dewji, Manji etc na hata kina Mengi, kufanya wema unaonekana kwa kundi la watu, ili maltitude of people wakushukuru, with genuine intention ya kukuombea mema, ile will power yao, inanyoosha njia yako, ni hivi ndivyo wafanyavyo hata kina Kakobe na wahubiri kibao,kufanikiwa by playing with people minds in giving out their will powers for your advantage.
Wahindi wanavyodhamini timu, wanapoteza mamilioni what for. Manji anapata nini Yanga?, watu hawakijui, lakini Manji anajua na Mengi pia anajua ndio maana Mengi alitaka na yeye kupenyeza mguu wake huko, wale wazee wa Yanga, wakaishia kumlia hela yake na kuendelea kumuabudu Manji, kwani sumu aliyowamwagia, imeshawalewesha kabisa, na juzi ndio imemshukia Madega!.
Kwenye mwili wa binadamu, hakuna kitu chenye nguvu kama 'will power', hii will power iko ndani ya kila mtu, ila wengine inajionyesha zaidi, hivyo kujiita wachungaji, waganga, wachawi, wanajimu, viongozi, au watu wenye vipaji maalum. Wengine haijionyeshi wazi sana, lakini wengi wanayo katika maeneo tofauti wekiwemo wengi wetu humu JF, atashuhudia sio tuu uwezo wao kwenye kukata issue, bali convincing power ya hali ya juu ambapo hata karatasi jeusi, unaliona kwa macho yako mwenyewe kuwa ni jeusi, akikuambia ni jeupe, utaliangalia na hatimaye kuliona kuwa ni jeupe, kumbe wapi!.
Brazili inakusanya will power za Waafrika to rally on its behind kupata ushindi. Kucheza na Zimbabwe wameiteka Southern African region kwa vile wanajua wazi Bafana Bafana ni wasindikizaji ambao sala zote za Bara la Afrika ziko nao. Amini usiamini, baada ya Brazili kukipiga na Zimba, sala zote za Zimba ni kwao na sio Bafana tena. Baada ya kukipiga na sisi, sala zote za nchi za Jumuiya ya Africa Mashariki ni zao, watu wanashangilia zaidi the teams they are close with, hivyo Brazili imejimuvuzisha kuwa close na African Continents kuvuna " will power" zetu kwenye kuitakia ushindi.
Namalizia kwa kuwaambia wana JF wote kuwa kombe hili, linakwenda Brazili, ni Samba Samba mtindo mmoja toka Brazili mpaka Afrika, anayebisha abishe tuu, siku ya siku, wale mnaosoma hapa mtakumbuka.