Why are we still investing into HidroPower?

UrbanGentleman

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2016
Posts
2,584
Reaction score
1,886
Kwa vyanzo vya nishati tuliyonavyo sizani Kama kuna haja ya kutumia nguvu kubwa kwenye mfumo wa umeme unaosua sua kwa muda mrefu Sasa.

Tuna gesi ya asili, nishati ya jua, tuna upepo lakini kwanini tupo kwenye hidro?.

Wengine wanatoka kwenye HidroPower lakini sisi ndio tunakimbilia huko, Kama tumelenga kuboresha vyanzo vyetu vya nishati kwanini tusitumie nishati mbadala? Kwanini tusitumie gasi yetu ya asili na ipo yakutosha?.

Ni kwamba sisi hatuoni umuimu wa kua na umeme wa uhakika katika nchi inayolenga uchumi wa viwanda?
 
For your information, hydropower remains the cheapest and the cleanest energy yet
 
Tuliambiwa kua gas ikianza kutumika tutakua na umeme wa uhakika na wa Bei nafuu ,

Wanasiasa sio watu wa kuamini hata siku moja pambana kivyako bila kuwategemea hawa watu

Over
 
hemb ngoja wenzangu waje, ila kwa mm kdg umenishangaza asee, kuna nchi zinataman hii H.E.P ww unayoiita hidro, ina faida nying sana tofaut na hizo unazotaka, hiv umewaza vzr boss? Au ni swaumu
 
kuliko jua???

kuliko upepo??
Installation ya wind turbines na solar panels kuweza kutengeneza umeme unaoweza kutoa hizo MW sio mchezo. Na lazma kuwe na reliable source. Kwetu hydro ni reliable compare na wind na solar(ofcoz jua linawaka kila mahali lkn si kila mahali unaeza anzisha solar power plant)
 
hemb ngoja wenzangu waje, ila kwa mm kdg umenishangaza asee, kuna nchi zinataman hii H.E.P ww unayoiita hidro, ina faida nying sana tofaut na hizo unazotaka, hiv umewaza vzr boss? Au ni swaumu
Tetea point yako, usisubiri mtu aje akutetee, hebu leta hizo faida
 
Asante! Pia hizo sources (wind, solar), umeme wake si endelevu (intermittent) kutokana na factors mbali mbali kama vile wind speed, air density, weather, cloud cover etc.
 
Bado hydroelectric power inasehemu kubwa sana katika umeme unaozalishwa duniani. Vituo vikubwa zaidi vya umeme duniani ni hidro, katika orodha vituo vitano vikubwa ni vya maji kama three gorges dam 22 500mw hii iko China, Itaipu dam14,000mw Brazil, Xiluodu 13,260mw China, Guri 10,233mw Venezuela, Tukurui 8350mw Brazil, Belo Monte 8176mw Brazil.

Bado kuna vituo vingine viko katika ujenzi mfano wa hivyo ni Beibentan(sina hakika na spelling) China 16000mw na Wudongde 10200mw hivyo baadhi tu.

Kiujumla katika orodha ya vituo vikubwa vya kufua umeme duniani, vituo vingi ni vile vinaendeshwa kwa nguvu za maporomoko ya maji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…