WHO Wanasema corona waliujua ni ugonjwa X tangu 2018

MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
5,011
6,542
Virusi vya corona: WHO ilijua kuhusu virusi vya corona miaka miwili iliopita

Ugonjwa uliopewa jina X ulisemekana kuwa na hatari na huenda ungelisababisha janga la kimataifa

Ugonjwa uliopewa jina X ulisemekana kuwa na hatari na huenda ungelisababisha janga la kimataifa

Mnamo mwezi februari 2018, kundi la wataalam wa shirika la Afya duniani WHO lilichapisha orodha ya magonjwa ambayo yanapaswa kupewa kipau mbele katika uangalizi na utafiti kutokana na tisho kubwa yanayotoa.

Orodha ya magonjwa manane ilishirikisha Ebola, Zika, homa ya Lasa, Homa ya Rift Valley, Homa ya Crimean Congo, ugonjwa wa nipha na magonjwa ya mapafu ya SARS na MERS,
Lakini ugonjwa mmoja zaidi ulikuwepo na ukapewa jina X.

Ugonjwa huo WHO ilisema kwamba utatoa mlipuko hatari wa kimataifa na utasababishwa na viini visivyojulikana vinavyoweza kusababisha maambukizi miongoni mwa binadamu.

Miaka miwili baadaye, tukiwa na ugonjwa uliosababisha maambukizi ya takriban watu milioni 2, swali ni je, tunaishi na ugonjwa X ambao WHO ulitarajia?

''Kweli Covid 19 ndio ugonjwa uliopewa jina X'', alisema Dkt Josie Golding, mkuu wa magonjwa ya milipuko katika shirika la kufanya tafiti mjini London akizungumza na BBC.

''Ugonjwa X lilikuwa wazo ambalo liliwakilisha kitu kisichotarajiwa ambacho hatukukijua'', anaongezea.
Na sasa vile tumeona jinsi visa vya wagonjwa vilivyoongezeka baada ya kutambua na kufanya utafiti kujua ni ugonjwa wa aina gani, nadhani Covid 19 ndio ugonjwa X.

Chanzo BBC Swahili
 
Back
Top Bottom