Who made space,universe and our world

Pure_sapiens

JF-Expert Member
Dec 25, 2016
2,197
2,025
Habari wana jf natumai ni wazima.Sijawahi kuanzisha katika jukwaa hili(home of great thinker) Leo ndo my first time.Hili huwa najiuliza lakini nakosa majibu.Soma kisa hiki hapa chini

Mwanasayansi wa elimu ya viumbe Athanasius Kircher(1601-1680)alikuwa na tufe leñye sura ya dunia lililofanywa kwa ustadi sana.Siku moja rafiki yake aliyekuwa haamini kuwa kuna Mungu,alipoona tufe hilo na kuvutiwa na uzuri wake,aliuliza Nani aliyeufanya mfano huu wa dunia hivi?Kircher akajibu"Hakuna mtu,umejifanya wenyewe".Rafiki yake akasema"Unanichekesha aliyeufanya mfano huu lazima awe mstadi mkubwa,Jinsi gani Kircher akahoji.Hautaki kukubali ya kuwa mfano huu dhaifu wa tufe la dunia la dunia umejifanya wenyewe,lakini unakaza mafundisho yako ya kuwa dunia kubwa jinsi hii imejifanya yenyewe.
Swali linebaki pale pale.Who made space,unirves and the world?
 
Nasubiri kuona wazee wa dini ambao wanaamini dini yao for some reason ni special kati ya dini zaidi ya 4000. Na hakuna hata moja inayokuja na proof ya kitu chochote kile wanachokisema. Science pekee ndiyo imekuja na proof toka enzi hizo hadi leo, na ndo kitu pekee kilichotuletea maendeleo leo hii tupo JF tunawasiliana. Maduduwasha mengine mlijazwa tu utotoni mmeshindwa kujitoa kwenye hicho kifungo kwa sababu mlitishwa kuna moto. Hahaha moto my ass.
 
GOD
 
Naona umepata nafasi ya kutoa kilichomo moyoni mwako. Ujahilia at its best.
 
Kuna pande mbili 1. Elimu na uvumbuzi 2. Dini

Kwenye elimu kuna wachambuzi weengi sana kila mmoja alikuja kwa theory zake kutokana na uelewa wake kwamba mwanzo hapakua na kitu zaidi ya gasi kama H He n.k hii inaonekana kwenye theory kama big bang theory ambayo ndio inayo kubalika sana , planetesemal theory n.k kwa kuchambua evidence zinazoonekana. So moja kwa moja chanzo kinaweza kuwa ni energy as defined kuwa energy can neither be created nor destroyed but only transform from one form to another.

Ya pili ni kwenye upande wa dini, dini ni imani na binadamu lazima kuna upande unaouamini ata kama ni mti mkubwa basi usahihi utatokana na kitu uaminicho,

Mtoa mada wewe fwatilia kila pande, itakayo kuingia akilini basi hiyo hiyo ifwate ndio kitakua chanzo cha space, universe and our world
 
Nasubiri kuona wazee wa dini ambao wanaamini dini yao for some reason ni special kati ya dini zaidi ya 4000. Na hakuna hata moja inayokuja na proof ya kitu chochote kile wanachokisema. Science pekee ndiyo imekuja na proof toka enzi hizo hadi leo, na ndo kitu pekee kilichotuletea maendeleo leo hii tupo JF tunawasiliana. Maduduwasha mengine mlijazwa tu utotoni mmeshindwa kujitoa kwenye hicho kifungo kwa sababu mlitishwa kuna moto. Hahaha moto my ass.
dini haipo kwa ajili ya uvumbuzi..dini IPO kwa ajili ya kutoa muongozo wa namna ya kuishi kama watu na mazingira yanayotuzunguka
 
Kama ipo kutoa muongozo wa namna ya kuishi basi imefeli vibaya mno maana inapotosha.
 
Mungu ndiye aliye umba Ulimwengu, na vyote viujazavyo. Mungu aliyejitambulisha kwa Musa kwa Jina la
MIMI NIKO AMBAYE NIKO. Kutoka 3 : 14

Hao miungu wengine nao wameumbwa na huyo, na hao miungu hawasemi kuwa waliumba kitu chochote.

Soma Biblia, kitabu cha Mwanzo, sura ya kwanza na kuendelea.

Biblia pia ni kitabu cha Sayansi nashanga kwanini badhi ya watu wanakiona ni kitabu cha kiimani pekee.

Biblia imeandika mambo ya Kisiasa, Kijamii na Kiutamaduni pia.
 
Nasubiri kuona wazee wa dini ambao wanaamini dini yao for some reason ni special kati ya dini zaidi ya 4000. Na hakuna hata moja inayokuja na proof ya kitu chochote kile wanachokisema. Science pekee ndiyo imekuja na proof toka enzi hizo hadi leo, na ndo kitu pekee kilichotuletea maendeleo leo hii tupo JF tunawasiliana. Maduduwasha mengine mlijazwa tu utotoni mmeshindwa kujitoa kwenye hicho kifungo kwa sababu mlitishwa kuna moto. Hahaha moto my ass.
Science inachojaribu kufanya ni kusafiri kwenye bahari (Dunia iliyoumbwa na Mungu) na kujaribu kutafuta maana ya vitu inavyoviona (Uumbaji wa Mungu) huku ikiwa haina compass wala ramani (Neno la Mungu). Tuhuma za sayansi kuukataa uwepo wa Mungu unaupa wakati mgumu sana pale maswali yanapozuka na ndio maana kila mwanasayansi ana jibu lake na mtazamo wake kuhusu ayaonayo.
Wanazuoni wa zamani hawakuwa na sintofahamu za leo lakini kwao Theology au ujuzi wa Neno kwao ndio iliyokuwa mama wa tafakari zote za sayansi yaani ilibidi umjue Mungu kwanza ndipo uanze kujadili na kuuchunguza uumbaji wake.
 
Unajua kuna watu wagumu kweli kuelewa yaani mpaka leo hawajui science ni nini? eti wanaamini science wakati wamesahau science ni kitu kando na dini ni kitu kando. Hii science wanayoiamini hawajui kuwa ni maarifa tu! ambayo haiendi mpaka pawepo fikra fulani. Mfano huwezi tengeneza silaha ya kivita mpaka pawepo fikra inayokusukuma kwa nini unatengeneza hiyo silaha. Ndio utakuta unatengeneza silaha kwa lengo la kupambana na adui yako ili uhifadhi uhai, hapa sasa unatumia maarifa ni vipi hiyo silaha itaundwa? na hapa sasa ndio tunaita science. Na ndio maana kila zama zilitofautiana maendeleo ya science, kwa sababu fikra zilizotawala watu zilikuwa tofauti tofauti. Haya ni kwa watu wenye uelewa wa hari ya juu. Tukija katika dini sasa hapa kila mtu anamtazamo wake kuhusu maana ya dini, wengine wanasema dini ni njia ya maisha yaani ina muundo wa kisiasa wengine wanasema dini inahusiana na mambo ya kiroho tu! hapa kila mtu huwa na hoja zake. Kwa hiyo tukiangalia asili ya ulimwengu tuangalie kwa upana zaidi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom