WHO: Kwa sasa dunia ina Watu wenye Ukichaa Milioni 55, mwaka 2030 watafikia Milioni 78 na mwaka 2050 watakuwa Milioni 139

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Kwa Ripoti / Taarifa hii ya Shirika la Afya Duniani ( WHO ) Mightier Mimi wala siwakatalii, kwani nina uhakika kuna Mtanzania Mmoja kwa Kujichanganya Kwake kuhusu Yesu Kristo badala ya Nabii Yusuph nae piga ua katika hawa Milioni 55 ya Watu wenye Ukichaa ( Dementia ) nae yumo.

Na kilichonishangaza kama siyo hata Kunishtua ni kwamba katika Taarifa / Ripoti hii ya Shirika la Afya Duniani ( WHO ) kuhusu Watu Milioni 55 kuwa na Ukichaa ( Dementia ) ni kwamba 8.1% ni Wanawake na 5.4% ni Wanaume.

Nakumbuka miaka ya nyuma Watu / Jinsia iliyokuwa ikiongoza kwa kuwa na Watu wenye tatizo hili la Ukichaa (Dementia) walikuwa ni Wanaume ila sijajua ni nini kimetokea ghafla mpaka Wanawake wanaongoza hivi.

Shirika la Afya Duniani ( WHO ) imezitaka nchi zote Ulimwenguni kupambana na tatizo hili ambalo kwa mujibu wa Utafiti wao wanasema linaongezeka tena kwa Kasi mno na huenda hata nguvu Kazi ikapotea na kupelekea kuathiri hata Uchumi wa Mataifa yao na Umasikini Kukithiri zaidi.
====

Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO iliyotolewa hii leo mjini Geneva, Uswisi yenye jina 'Hali ya ulimwengu kuhusu hatua za afya ya umma dhidi ya tatizo la kusahau', inasema ni robo tu ya nchi zote ulimwenguni ambazo zina sera, mkakati au mpango wa kitaifa wa kusaidia watu walio na ugonjwa wa shida ya akili unaosababisha kupoteza kumbukumbu na hali nyingine kama kushindwa kufikiria vizuri.

Ripoti hiyo kifafanua zaidi imeeleza kuwa nusu ya nchi hizi ziko katika Kanda ya Ulaya ya WHO na sehemu iliyobaki imegawanyika kati ya maeneo mengine ya ulimwengu. Wakati huo huo barani Ulaya mipango mingi iliyokuwepo kushughulikia tatizo hili la kupoteza kumbukumbu au dementia, imekwisha muda wake na hivyo ikionesha hitaji la serikali kujitolea upya kuweka mipango madhubuti ya kupambana na hali hii.

Mkurugenzi wa WHO, Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus, amenukuliwa akisema, "ugonjwa wa kusahau unawaibia mamilioni ya watu kumbukumbu zao, uhuru na utu, lakini pia unatuibia sisi watu tunaowajua na tunaowapenda. Ulimwengu unawaangusha watu walio na shida ya akili, na hiyo inatuumiza sisi sote. Miaka minne iliyopita, serikali zilikubaliana malengo ya wazi ya kuboresha huduma za dementia. Lakini malengo pekee hayatoshi. Tunahitaji hatua za pamoja ili kuhakikisha kuwa watu wote walio na shida ya akili na kupoteza kumbukumbu wanaishi na msaada na hadhi inayostahili.”

Aidha, WHO inaeleza kuwa idadi ya watu wanaoishi na ugonjwa wa shida ya akili na hivyo kupoteza kumbukumbu na uwezo wa kufikiri, inaongezeka ikikadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 55, ikiwa asilimia 8.1 ya wanawake na 5.4% ya wanaume wenye zaidi ya umri wa miaka 65 wanaishi na shida ya dementia. Idadi hii inakadiriwa kuongezeka watu milioni 139 ifikapo mwaka 2050.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na WHO, Ugonjwa wa kusahau husababishwa na magonjwa tofautitofauti na majeraha ambayo huathiri ubongo, kama ugonjwa wa Alzheimers au hata kiharusi. Ugonjwa huu unathiri kumbukumbu na kazi nyingine za utambuzi, pamoja na uwezo wa kufanya kazi za kila siku

Chanzo: Mtandao wa WHO
 
Tatizo wazungu ukichaa sio lazima uokote makopo. Yaani kwa definition yao ya Insanity wakija bongo wote tunaumwa.
 
Back
Top Bottom