Tanzania ifuate mfumo gani katika kusimamia habari zinazochapishwa kwenye mitandao.
Mimi naona tusifuate mfumo wowote, kwa sababu matatizo yetu hayafanani na Marekani au Uingereza. Hao waliofikia kuweka mifumo ya kulinda habari leo walishapitia hapa tulipo sisi leo (uhuru wa habari mtandaoni). Hivyo wacha Watanzania wawe huru kuandika habari. Cha msingi habari ziwe na ukweli, leo tumeona jinsi tunavyoweza kupata habari nyeti mtandaoni. Zenye ukweli first class. Watanzania tumefungiwa uhuru wa uandishi wa habari kwa miaka mingi sana. Kila kitu kuhusucho nchi, utawala au kiongozi ilikuwa ni SIRI KUU.
Huo usiri mkuu umetufikisha kwenye hali hii:
1) poor education system and facilities
2) poor health care system
3) poor infrastructure syatem etc.
Kwa sababu hakuna aliyekuwa na haki ya kuhoji chochote. Tumetawaliwa kama mazumbukuku hadi leo hii. Ni aibu sana.
Usiri ulikomaa na kuzaa uoga miongoni mwa watendaji katika nchi.
Usiri ukashika mimba na kuzaa udikteta mamboleo ambao umeota mizizi na kuzaa mjukuu UFISADI.
Mjukuu Fisadi amelelewa na kumbelezwa hata anatu-cost our life. Lakini bado tumembepa.
Fisadi huyu amefanya maisha ya walemavu (Albino) kuwa hatarini.
Hebu niambie ni Mtanzania gani mwenye uwezo wa kununua viungo vya Albino kwa Milioni 30???? Kama siyo Fisadi mwenye pesa za wananchi?
Fisadi wameshindwa kuwalinda Albino.
Fisadi amesababisha mwananch usilale usingizi kwa sababu ya ujambazi. Kisa yeye ana mitambo ya kumlinda.
Mimi nasema: Asante technologia hii ya tovuti ambayo imeweza kuuanika uchafu wa ufisadi hadharani. ...ni Mtanzania gani angeweza kusimama hadharani na kumnyoshea kidole fisadi??? Ni Wangapi waliojaribu kumnyoshea kidole fisadi na wemeishia kuwa nyama ya udongo???
Vyombo vya habari vingapin vimeadhibiwa kwa kuandika ukweli dhidi ya fisadi?
Tanzania tuna-baby-sit mafisadi. Hasa viongozi tuliowapa dhamana, huenda nao wananufaika na ufisadi huu.
Mimi nasema: HAKUNA KUFUATA MFUMO WOWOTE WA HABARI MPAKA TANZANIA IWE HURU, KIUFISADI.
Huko Uingereza na Marekani tunawaona wanavyowajibika na kuwajibishwa pindi ijulikanapo ufisadi umenukia ktk sekta. TANZANIA TUMEFANYA NINI???
Ni aibu kusema tuige mfumo upi? ni bora tusiige, kwa sababu mengi tunayosema tunayafuata toka njee in reality HATUYATEKELEZI IPASAVYO.
mimi nasema: HAKUNA KUFUATA MFUMO WA HABARI WA UINGEREZA AU MAREKANI.
Ningekushukuru sana maada hii ungeileta namna hii: TANZANIA TUWASHUGHULIKIEJE MAFISADI, KU-UINGEREZA AU MAREKANI.
IKIBIDI HATA KI-ARABU TUTUMIE, HAO MAFISADI WAPIGWE MAWE MPAKA WAFE. NDIO CHANZO CHA GIZA KUKITHIRI Nchini (ktk technologia hii ya leo kwa nini nchi ikae Gizani?) hii inaingia akilini kweli?????, hivi nasi tunajihesabu tunaishi ulimwengu huuu????
Viongozi wetu kila siku wanatembelea nchi za wenzao, hakuna nachojifunza kweli???? hata mikakati ya kuiweka nchi safi? tunahitaji msaada mzungu aje atuambia ndani kwako kuchafu na hali wewe unaona?
Jamani! wakati umefika, kama viongozi waliopo hawawezi kututumikia basi watokeeee. Tupate watu wenye hali ya kuleta mabadiliko ya maendeleo kwa wananchi na nchi kiujumla.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.