HNIC
JF-Expert Member
- Sep 6, 2011
- 1,898
- 2,195
Wiki imepita na kwa kweli ninapenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mungu kwa Jamiiforums na hasa Max kwa kutuwekea hii kitu while he's paying the price ili sisi tupate platform ya kujadili issues bila woga. Kwa kuwa Jamiimedia imefungua kesi ya uhuru wa vyombo vya habari naomba sana muweke links za kuchangia ili tuendelee na hiyo kesi ambayo itatusaidia sote.
Baada ya kusema hayo. Nimeshikwa na butwaa kuhusu yanayosemwa kuhusu Katibu Mkuu kiongozi Ombeni Sefue ambaye:
1. Ametajwa na kutuhumiwa kuhusika kwenye kashfa ya Ukabila kwani anahusika kushinikiza kazi zitolewe kwa watu wa kabila lake la waPare.
2. Ametuhumiwa kuhusika kwenye kashfa na kampuni ya wa China ya Ujenzi ya CRJE
3. Sefue anatuhimiwa kuwa ndiye mhusika mkuu wa kwenye uvurandaji wa MSD
5. Alipokuwa balozi wa Tanzania kule Washington DC, Marekani alikuwa kinara wa kutetea afisa Ubalozi (Alan Mzengi) ambaye alihukumiwa na mahakama ya Marekani kwenye kesi ya kumfanya mfanyakazi wao wa ndani (Zipora Mazengo)waliyemtoa Tanzania kuwa MTUMWA wao. Ikumbukwe kuwa Serikali ya Tanzania ilitia sahihi mikataba mbali mbali ya:
a) Kulinda haki za binadamu
b) Kulinda haki za wafanyakazi
c) Kupiga marufuku utumwa
Sasa huyu huyu sefue kwenye kesi ya binti wa Kitanzania aliyefanywa mtumwa na afisa wa Ubalozi, Katibu mkuu kiongozi aliamua kuchukua upande wa dhulma
Mwenye kutaka kusoma zaidi hii kesi asome hii WIKILEAKS Cable:
Cable: 10STATE7269_a
Siamini kuwa Sefue alikuwa akifanya yote hayo kwa sababu alikuwa anatetea maslahi ya nchi ya Tanzania hata kidogo na hasa pale alipokataa katakata huyo binti aliyefanywa mtumwa asilipwe fidia.
Zaidi soma aliyokuwa anayasema balozi wa Marekani Tanzania (Mark Green) juu ya Ombeni sefue:
US embassy cable - 07DARESSALAAM1539
Kwa wanaomjua sefue wanasema alibebwa na Rais Mkapa alakini Mzee Mkapa naye kashamchoka na haya ma kashfa na jinsi alivyo kuwa tainted na hizi kashfa is he really the right person kuwa katibu mkuu kiongozi wa rais msafi na mwenye uruma kama Dr. John Pombe Magufuli?
Na pia ilikuwaje mpaka a mere speech writer ambaye hajawahi kuwa katibu mkuu kokote kuwa kupaishwa mpaka akawa mkubwa wa makatibu wakuu wote nchi hii?
Sasa swali kwa wana Jamiiforums, Who is the real Ombeni sefue ambaye ndiye Katibu mkuu kiongozi wa Rais Magufuli?