Who is Happygod Naftali?

Fortunatus Buyobe

JF-Expert Member
Nov 9, 2011
463
1,127
Wakati wa amshaamsha juu ya upotevu wa makontena 349 Azam ICD na mengine zaidi ya 2000 kwengineko, huyu jamaa alikuwa ni jipu la kwanza lililotumbuliwa kwani alikuwa ni msimamizi wa ICD's na alisimamishwa kazi.

Lakini leo nilipopata taarifa za kumhusu mtu huyu huyu kuhusishwa tena kwenye upotevu wa makontena mengine 11,884 niliona ni kama radi iliyonguruma ghafla kipindi cha juakali. Mbaya zaidi tunaambiwa huyu mtu hajakamatwa eti "anatafutwa na polisi" This is completely insanity.

WHO IS HAPPYGOD NAFTAL? Kwa nini hakuwekwa chini ya ulinzi tangu mwanzo aliposimamishwa? Hakuwa mtu nyeti kushikiliwa hata kwa dhamana wakati uchunguzi unaendelea? Sasa asipopatikana sie washagiliaji wa "operation majipu" tutaendelea kuaminishwa kuwa serikali yetu iko serious isisahau mkasi ndani ya mgonjwa?

Has TAKUKURU reformed to copy with #hapakazitu slogan? Kitengo cha organized crimes cha polisi kipo kazini? Ninaatach taarifa ya mwanzo ya upotevu na ya pili ya upotevu kumuhusu huyu HAPPYGOD NAFTALI ili tuwaze wote kwa sauti. Jumatano njema

Maamuzi mengine ya Rais Magufuli kuhusiana na Upotevu wa Makontena na TRL
December 7, 2015 suleiman

Mnamo tarehe 27 Novemba, 2015 nilifanya ziara ya kushitukiza Bandari ya Dar es Salaam ambapo nilifichua mwanya wa ukwepaji kodi kwa makontena 329 yaliyopitishwa bandarini kinyume cha utaratibu.

Mtakumbuka pia tarehe 4 Desemba, 2015 nilirudi tena kufanya ufuatiliaji wa hatua ya udhibiti wa upitishaji wa bidhaa mbalimbali kinyume cha utaratibu.

Ziara yangu ilinipitisha hatua zote za upitishaji mizigo ambazo pia kwa mujibu wa Taarifa ya Ukaguzi wa Ndani wa tarehe 30 Julai 2015 Mamlaka ya Bandari uligundua kuwepo kwa mianya mingi ya ukwepaji kodi ikiwemo na makotena 2387 yaliyopitiahwa kati ya Machi – Septemba 2014 kinyume cha utaratibu, vitendo hivi vinaonyesha kuwa bandari yetu hupitisha makontena mengi bila ya kulipiwa kodi na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa.

Upotevu huo unaenda sambamba na mfumo usiokidhi wa kupokelea malipo (BILLING SYSTEM) ambao unatoa mwanya mkubwa wa kupoteza mapato ya Serikali. Bandari ni eneo muhimu ambako kama panasimamiwa vizuri panaweza kukusanya fedha nyingi na kuchangia Pato la Taifa.

Serikali haitavumilia kuona watu wachache au kikundi chochote kilichojipanga kuhujumu mifumo au kuiibia Serikali kwa namna yoyote ile kwa manufaa ya wachache.

Matokeo ya ziara hizo ni haya yafuatavyo:-
1. Nimeagiza mfumo wa kupokelea malipo ubadilishwe kutoka Billing System na uwekwe mfumo wa e-payment ambao tayari ulianza kuwekwa na uwe umekamilika kufikia tarehe 11 Disemba 2015.
2. Kwa kuwa ripoti iliwataja waliohusika na upitishaji makontena hayo na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa, kuanzia muda huu nawasimamisha kazi wale wote waliohusika kupitisha makontena kinyume na utaratibu.

1. Wasimamizi wa Bandari Kavu (ICD)
(i) Happygod Naftari
(ii) Juma Zaar
(iii) Steven Naftari Mtui
(iv) Titi Ligalwike
(v) Lydia Prosper Kimaro
(vi) Mkango Alli
(vii) John Elisante
(viii) James Kimwomwa – ambaye amehamishiwa Mwanza.

2. Wafuatao ni Viongozi wa sekta zilizotoa ruhusa ya makontena kutoka ndani ya Bandari ambao hawamo kwenye ripoti ila ni wahusika wakuu.

1. Shaban Mngazija – Aliyekuwa Meneja Mapato ambaye kwa sassa amehamishiwa Makao Makuu kitengo cha Fedha.
2. Rajab Mdoe – Aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Mkuu wa Bandari Kavu (ICD) – ambaye amehamishiwa Makao Makuu kwa Naibu Mkurugenzi Co-operate Services.
3. Ibin Masoud – Kaimu Mkurugenzi wa Fedha.
4. Apolonia Mosha – Meneja Bandari Msaidizi – Fedha.
5. James Kimwomwa.

Kutokana na utendaji mbovu wa Mamlaka ya Bandari kwa muda mrefu na kwa kitendo cha kutochukua hatua kwenye vyanzo.

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amevunja Bodi yote ya Bandari na kutengua uteuzi wa wafuatao:-

1. Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari – Prof. Joseph Msambichaka.
2. Mkurugenzi Mkuu wa Bandari – Bw. Awadhi Massawe.

Ndugu Waandishi wa Habari mtakumbuka pia nilifanya ziara pia TRL ambako kwa awali nimegundua matumizi mabaya ya fedha Shilingi Bilioni 13 nje ya utaratibu ambako uchunguzi unakamilishwa.

Mheshimiwa Rais, pia ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaban Mwinjaka kuanzia tarehe ya leo na atapangiwa kazi nyingine.
 

Attachments

  • eb2b31bae6379d4957515a7bff02875a.jpg
    eb2b31bae6379d4957515a7bff02875a.jpg
    30.6 KB · Views: 143
  • Screenshot_2015-12-30-04-18-55.jpeg
    Screenshot_2015-12-30-04-18-55.jpeg
    159.8 KB · Views: 71
Last edited by a moderator:
Aiseee uko sahihi kabisa. Haiwezekani mtu mmoja apotee kama shilingi kwenye bahari. Ila kwa style ya upotevu wa makontena na magari kutolipiwa kodi kama tuko serious kweli basi Wakurugenzi, Mawaziri na baadhi ya Waliokuwa Mameya watakamatwa (kama tuko serious lakini)
 
Hivi TRA sina wana kitengo cha ndani cha anti fraud and embezzlement(FAST) kina jipima kweli na Monitoring and evaluation kwa haya yaliyotokea?
 
Back
Top Bottom