#COVID19 WHO: Imesema bado haina maelezo kutoka Tanzania namna inavyoshughulikia COVID-19

FOCAL

JF-Expert Member
Jun 25, 2019
2,389
3,067
NAIROBI (Reuters)

Leo siku ya Jumapili mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ameisisitiza serikali ya Tanzania kutoa taarifa juu ya hatua zake za kupambana na janga la coronavirus, akisema mamlaka ya huko wamekuwa wakipuuza maombi yake mara kwa mara.

Njia ya wasiwasi/yenye mashaka ya Rais John Magufuli kuelekea COVID-19 imesababisha wasiwasi kwa maafisa wa WHO. Msemaji wa serikali aliiambia Reuters mnamo Februari 12 kwamba Tanzania "ilidhibiti" mlipuko huo, lakini ilisitisha kuripoti maambukizo na vifo vipya vya coronavirus mnamo Mei mwaka jana. Wakati huo ilikuwa imesajili kesi 509 na vifo 21.

Mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema hayo leo Jumapili kuwa idadi ya watanzania wanaopima na kukutwa na COVID-19 nje ya nchi inatia msisitizo wa hitaji la Tanzania kuchukua hatua madhubuti kulinda watu wake na kulinda idadi ya watu katika nchi hizi na kwingineko."

Tedros pia amekumbushia maongezi yake ya simu na Matshidiso Moeti, mkuu wa WHO barani Afrika, mwishoni mwa Januari kwa Tanzania kuimarisha hatua za afya ya umma dhidi ya COVID-19 na kujiandaa kusambaza chanjo.

Aliongeza kuwa tangu wakati huo amekuwa akizungumza na viongozi kadhaa huko bila mafanikio.

"Hali hii inatia wasiwasi sana. Ninarudia tena wito wangu kwa Tanzania kuanza kuripoti kesi za COVID-19 na kushiriki kutoa takwimu," Tedros alisema katika taarifa yake kwenye wavuti ya WHO.

Msemaji wa serikali ya Tanzania Hassan Abbasi hakujibu ujumbe wa Reuters kutaka maoni yake juu ya matamshi ya Tedros.

Katika taarifa baadaye Jumapili, ofisi ya Magufuli ilisema rais alitaka watanzania kufuata hatua za kujikinga dhidi ya coronavirus. Walakini, pia ilisema kwamba:

"Magufuli anataka watanzania ... kumwamini na kumtanguliza Mungu, ikizingatiwa kuwa kuvaa barakoa, kutokusogeleana na kuweka lockdown kumeonekana kuwa haitoshi kwani nchi zilizotekeleza hayo zimepoteza maelfu ikilinganishwa na Tanzania."

Magufuli alihudhuria ibada ya mazishi Ijumaa kwa afisa mwandamizi kutoka ofisi yake ambaye sababu ya kifo chake haikuwekwa wazi, na akatangaza siku tatu za maombi ya kitaifa.

Siku ya Jumapili, Magufuli alisema watanzania wanapaswa kuvaa tu barakoa zilizotengenezwa Tanzania, akisema zile za nje zinaweza kuwa si salama.

Siku ya Jumatatu, waziri wa afya wa Oman alisema nchi yake inafikiria kusitisha safari za ndege kutoka Tanzania, baada ya asilimia 18 ya wasafiri wanaowasili kutoka Tanzania kupimwa na kukutwa na COVID-19.

Thailand iliripoti Jumatatu kesi yake ya kwanza ya aina mpya ya kirusi cha COVID-19 inayoambukiza sana na iliyogunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Afrika Kusini, kwa raia wa Thailandi ambaye aliwasili kutoka Tanzania.

(Ripoti toka chumba cha habari cha Nairobi; Imehaririwa na George Obulutsa na Raissa Kasolowsky)
 
Yaani hapa sio tu kukaa mbali na mabarakoa kutoka nje bali na mpaka na WHO yao.

Ni muziki wa jaymoe.. Wachiteme wachimumunye.

Kama inawauma zaidi watuache kimpango wetu.
 
Tunaweza shinda kwa jeuri ya mwenye kiti, lakini pengine kwa gharama kubwa
Hakuna Cha gharama kubwa hapo,.

Kwanza hata kipozisheni/position mpaka dakika hii huyo unayemuita m/kiti yupo juu.

Ana dangerous attack nyingi kuliko hao ma WHO /mabeberu.

Ana mipira ya kona mingi kuliko hao nyumbu wako.

Na walishajikologa ndani ya box walishika mpira. Mkuru akawaweka penalti tamuuuuu kweli kweli.
 
Hawawezi kuielewa kwa sababu wanacho wanachokielewa juu ya Tanzanja.
Ni vigumu sana kuamini kuwa Shirika hilo kubwa a Afya Duniani halielewi mpango wowote unapendelea Tanzania kupambana na madhila ya janga hili la Dunia.

Hii inanifanya kuafiki bila shaka yoyote kuwa Shirika hilo kuna mpango inaelewa unapendelea Tanzania ila hatutaki kusikia linata kusikia ile lilichopanga kusikia mfano "LOCKDOWN "

Tunapaswa kufika mahali pa kukubali kuwa zipo njia lukuki za kufikia lengo " equifinality" na haipo njia moja tu ya kufikia lengo.
 
Back
Top Bottom