WHO: Huenda janga la Corona likaisha ndani ya miaka miwili

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema kuwa anamatumaini janga la corona litakomeshwa ndani ya miaka miwili
Akizungumza mjini Geneva, Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema homa ya Spanish flu ya mwaka 1918 ilichukua miaka miwili kudhibitiwa.

Lakini ameongeza kuwa kuimarika kwa teknolojia ya sasa huenda haenda ikasaidia ulimwengu kudhibiti virusi ndani ya "muda mfupi".
"Bila shaka watu wakiendelea kutangamana, watatoa nafasi kwa virusi kusambaa," alisema.

"Lakini licha ya hayo, tuna teknolojia ambayo inaweza kukomesha hali hiyo, na elimu ya jinsi ya kukomesha maambukizi," alisema, akisisitiza umuhimu wa "umoja wa kitaifa, mshikamano wa ulimwengu".

Mafua ya mwaka 1918 yaliwaua watu karibu milioni 50 duniani.

Coronavirus kufikia sasa imewaua karibu watu 800,000 na wengine karibu milioni 23 kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo

Dkt Tedros pia alijibu maswali kuhusu ufisadi unaohusishwa na vifaa ya kinga binafsi (PPE) wakati wa janga la corona, na kutaja ufisadi huo kama "uhalifu".

"Ufisadi wa aina yoyote haukubaliki," alijibu.

"Hatahivyo ufisadi unaohusisha PPE... kwangu mimi binafsi na mauaji. Kwasababu wahudumu wa afya kufanya kazi bila PPE, tuna hatarisha maisha yao. Na pia kuhatarisha maisha ya watu wanaowahudumia."

Japo swali linaohusiana na ufisadi liliangazia zaidi Afrika Kusini, nchi kadhaa zinakabiliwa na suala hilo.

Siku ya Ijumaa, maandamano yalifanywa mjini Nairobi Kenya kufuatua madai ya ufisadi wakati wa janga la corona, huku madaktari katika hospitali kadhaa za umma wakifanya mgomo kwa kutolipwa marupurupu na kukosa vifaa kinga
 
Back
Top Bottom