#COVID19 WHO: Hakuna dalili za Corona kumalizika mwaka huu

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Ulimwengu unaendelea kushuhudia utolewaji chanjo ya Covid-19 wakati janga la virusi vya Corona likiendelea. Shirika la afya duniani WHO linasema janga hilo halina dalili ya kumalizika mwaka huu.

Na Emmanuel Kasomi
Shirika la afya duniani WHO linaamini kwamba janga la virusi vya Corona halina uwezekano wa kumalizika katika miezi ya karibuni.

Michael Ryan mkurugenzi wa mpango wa dharura wa shughuli za kiafya katika WHO amesema anadhani ni mapema kufikiria kwamba watalimaliza janga hili kufikia mwishoni mwa mwaka.

Amesema kinachoweza kumalizwa ikiwa ulimwengu utakuwa makini ni idadi ya watu kulazwa hospitali kutokana na virusi hivyo au vifo na matatizo mengine yanayosababshwa na janga hilo.

Nchi za ulimwengu zimetolewa mwito kujiepusha kuondowa haraka shughuli za kudhibiti virusi vya Corona, kutokana na kuwepo chanjo.
 
Back
Top Bottom