Who cursing our Tanzania!!!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Who cursing our Tanzania!!!?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Aug 7, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nani ameilaani nchi yetu Tanzania,na kama si nchi basi watu wake wameingia kwenye mkumbo huo,haiwezekani kila anaye jaribu kupitia mlango huu wa kichama kupata nafasi ya uongozi uadilifu wake unatia shaka,hata kama alikuwa muadilifu kweli kweli.Tatizo hasa nini Watanzania wenzangu?

  Bunge limetunga sheria kimya kimya,rais naye ameisaini kimya kimya bila hata mbwembwe kama ilivyo desturi yake,leo hii ana simama mbunge na kuleta hoja binafsi kutokana na sheria ambayo walishiriki kuitunga tena kwa kuipinga,kama si mchezo wa kuigiza nini.

  Leo hii kilio cha wafanyakazi kutokana na mafao duni yasiyoweza kufikisha siku kumi na tano hayajaisha serikali kwa kushirikiana na bunge wana shindilia msumari mwingine wa moto kwenye kidonda kibichi kwa kupitisha sheria ambayo ina wabana wafanyakzi kuchukua mafao yao watakapo kuwa wameacha kazi mpaka wafikishi umri wa miaka 55 au 60.


  Mbona linapokuja suala la maslahi yao binafsi kama wabunge wanalipigia kelele mpaka wakati mwingine wanatishia kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais lakini linapofika suala linalo gusa maslahi ya wapiga kura wao wanatia pamba masikioni.Wakati sheria inatungwa mpaka rais ana pelekewa kuisaini wao kama wabunge walikuwa wapi?Tunataka kujua ili tuondokane na mchezo wa kuigiza unao jaribu kufanywa na serikali kwa kushirikiana na bunge ambalo tuliamini ndicho chombo cha kuweza kuwatetea wananchi.

  Pia tunataka kauli ya bunge,yawezekana hatufahamu kanuni na sheria zinazo tumika kuliendesha bunge,ni wakati gani sheria hutungwa na kama kuna uwezekano wa baadhi ya sheria kutungwa kimya kimya bila umma kujua na bila kuingizwa katika ratiba ya bunge.Maana yetu sisi wananchi ni kuwa,tunataka kujua endapo bunge limekiuka na kuvunja katiba kwa kutunga sheria bila wajumbe(wabunge) wake kujulishwa.

  Majibu ya maswali haya ndiyo tu yatakayo tupa picha jinsi nchi yetu inavyoendeshwa kwa kuwaburuza wananchi wake na jinsi nchi isivyo makini katika kutekeleza mambo yenye tija kwa mmustakabali wa maendeleo ya nchi.

  Mambo mengi yamekuwa yakijitokeza lakini serikali yetu imekaa kimya.Hatari ninayo jaribu kuiona hapa,kuna mabo mengi sana yanafanyika shaghalabaghala na si ajabu mfuko huo wa hifadhi ya jamii umefilisika kiasi cha kupelekea serikali yetu kutafuta njia ya kujipanga upya.


  Tumeona ni jinsi gani mfuko huu wa hifadhi jamii unavyotumika vibaya bila idhini ya wanachama ambao ndiyo wadau wakubwa katika kuuchangia mfuko huu.Miradi mingi ya maendeleo imekuwa ikichota pesa za walalahoi hawa bila aibu kiasi kupelekea serikali kuwa mdaiwa mkubwa.

  Napenda kushauriana na wenzangu wa JF kutumia nafasi hii hususani kwa wale wenye ulewa wa sheria kutumia fursa hii tuendelee kuikosoa serikali kila pale inapoteleza kama si kwa makusudi kuwagandamiza wafanyakzi wake.

  Ni mara nyingi serikali imekuwa bingwa wa kukimbilia mahakamani pale panapotokea mgogoro na wafanyakzi wake,lakini linapokuja suala la serikali kusaini na kukubali kuitumia sheria kandamizi hakuna wa kuifikisha mahakamani.Hatari yake ni wananchi kuikatia tamaa serikali na kuto kuwa na imani nayo.Hali kama hii mara nyingi husababisha watu kutokuwa waadilifu wanapo pata nafasi ya kuvisimamia vyombo vya umma.


  Si pendi kuamini kuwa chanzo cha ufisadi kinachochewa zaidi na serikali kutokana na mifumo yake kandamizi katika kuwabana wanyonge japokuwa hali ndio inapelekea huko.

  Imani yetu kwa serikali katika kushughulikia matatizo ya wafanyakazi inazidi kushuka siku hadi siku,mahakama nazo zimeanza kupoteza imani kwa wananchi kuotkna na utendaji wake ambao umekuwa ukiingiliwa mara nyingi kiasi cha kuathiri hukumu.Utendaji wa upendeleo unao fanywa na mahakama ndiyo sababu inayoniaminisha serikali kukimbilia makahamani kila mara.

  Kwa mantiki hii basi,tungependa sasa bunge lijaribu kuliangalia suala kwa makini na kama kuna sheria ina ruhusu serikali ifikishwe mahakamani kwa kubaka haki wafanyakazi kwa kusaini na kuitumia sheria kandamizi.

  Mwisho Tanzania ni ya wote,tujenge desturi ya kuheshimiana toka juu mpaka chini ili kuweza kukuza maadili mema ambayo yameikumba serikali kiasi cha kushindwa kustawisha maendeleo ya wananchi na kudumaza watu wake kwa kutunga sheria kandamizi ili kuwanufaisha wachache.
   
 2. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  mi na 'like' tu napita
   
Loading...