Wher is Tanzania?

Wher is Tanzania?

oba

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Posts
310
Reaction score
66
Ukifuatilia kwa makini mwenendo wa maisha ya hapa TZ kuanzia kiuchumi, kijamii, kisiasa na kifamilia zaidi utashindwa kulocate wapi tulipo exactly.
taifa la marekani lina malengo yake ya muda mfupi na muda mrefu, malengo hayo si ya republican wala democrat; ni ya wamarekani. Chama hakiwezi kuyabadilisha, leo wakiingia republican wanaendeleza pale wenzao walipoishia kuelekea kule wanakotaka kwenda. Democrat hata kama iongozwe na mwafrika kama ilivyo kwa obama wa sasa, malengo na sera mama kwa africa haiwezi kubadilika. Vyama vyao vya siasa huleta sera ya what to do kuelekea kule tulikopanga kwenda kama taifa, hawaji na kipi watafanya ila namna gani watafanya.
Taifa letu limeachwa mikononi mwa wanasiasa, watu ambao hawana maslahi ya Taifa bali maslahi yao na vyama vyao, sera zao na malengo yao yanalenga mafanikio yao , ya vyama vyao na pengine taifa ni la mwisho. Hatuna mwelekeo kama taifa, hatuna dira kama taifa, hatuna kule tuendako, tunapelekwa mzobe mzobe na wanasiasa, Tumekwisha!
Wanasiasa na vyama vyao hawataweza kutupeleka kokote zaidi ya shimoni.
Taifa la Tanzania liko wapi? mbona sioni utanzania kama ulivyo? hakuna mwelekeo kama taifa. Tumeacha hatima yetu mikononi mwa magenge ya watu wachache kwa mgongo wa vyama vya siasa. Ole wetu!
Tuamke watanzania, tuamke wazalendo, tuandae Katiba itakayoweka kipaumbele cha mtanzania na Tanzania, wanasiasa na vyama vyao hawatatupeleka popote pa maana
Nawasilisha
 
Back
Top Bottom