Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,221
- 2,425
๐ก Whatsapp imefanikiwa kuweka rekodi kwa kuwa mtandao wa kwanza wa kijamii kuwa na watumiaji wengi kila mwezi zaidi ya watumiaji bilioni 3.
๐ก Siku ya jumatano mkurugenzi mkuu mtendaji wa meta Tajiri Mark Zuckerberg Aliweza kutangaza kupitia mkutano wa matokeo ya kifedha ya robo kwanza Q1, kwa kuweza kusema Whatsapp imevunja rekodi ya kipekee.
โก Whatsapp ambao ilianzishwa mwaka 2009 baada ya muda iliweza kununuliwa na kampuni ya Facebook ilikua mwaka 2014 kwa Takribani Zaidi ya Dola bilioni 19, ambapo mpaka kufikia mwaka 2020 Whatsapp ilikua Ina jumla ya watumiaji bilioni 2 kila mwezi.
๐ก Ila mpaka sasa Whatsapp imevunja rekodi kuwa app ya pili kuwa na watumiaji wengi kwa mwezi ambapo inaripotiwa zaidi ya watu bilioni 3 wanatumia Whatsapp kwa Mwezi kama ilivyokuwa mtandao wa Facebook.
โ๏ธ Mitandao mingine yenye watumiaji wengi kwa mwenzi ni kama ifuatavyo;
โก YouTube watumiaji bilioni 3
โก TikTok watumiaji bilioni 1.6
โก Instagram watumiaji bilioni 2
๐ Jambo la muhimu zaidi Kuna hati hati ya mtandao wa Whatsapp kuweza kuwekewa matangazo japo kampuni ya Meta Ina wasiwasi ya kupoteza watumiaji wake.
๐ Je utafurahia mtandao wa Whatsapp siku wakianza kuweka matangazo kwa watumiaji wake tuachie
maoni yako?